Loading Content...

Brian alikuwa

Loading...


Unique profiles
1
Most used tags
Total likes
0
Top locations

Average media age
720.8 days
to ratio
“Namna gani nitamwokoa mwanangu lakini?” akalia Mrs Garett. A;lijikuta anatamani hata kumwona ...
Media Removed
“Namna gani nitamwokoa mwanangu lakini?” akalia Mrs Garett. A;lijikuta anatamani hata kumwona huyo ‘mwanaume’ ambaye amemshikilia mtoto wake huko eneo ambako palikuwa panaitwa ulimwengu wa walio wafu. . . Lakini Brian akamwonya. “Sidhani kama unataka kufika huko.” wakati Brian ... “Namna gani nitamwokoa mwanangu lakini?” akalia Mrs Garett. A;lijikuta anatamani hata kumwona huyo ‘mwanaume’ ambaye amemshikilia mtoto wake huko eneo ambako palikuwa panaitwa ulimwengu wa walio wafu.
.
.
Lakini Brian akamwonya. “Sidhani kama unataka kufika huko.” wakati Brian akisema haya, alikuwa ni mtulivu sana. Anajua anachokiongelea. Anajua kilichopo kule.
.
.
“Si mahali salama hata kidogo. Panatisha, na kuna uwezekano hafifu wa kurudi hai.”
.
.
Mrs Garett akakabwa na kilio cha gubi. Mama yake Brian akajitahidi kumpooza na kumtuliza. Punde kidogo Olivia akaamka. Hakuwa anajielewa. Aliambazaambaza macho yake huku na kule na kukutana macho kwa macho na Brian! Bado Brian alikuwa na hofu juu ya binti huyo.
.
.
“Olivia!” Mrs Garett akamkumbatia mwanawe. Akambusu kwenye paji la uso na kumuuliza wapi alipokuwa. Nini anachokumbuka. Hamna kitu! Olivia hakuwa anakumbuka chochote kile zaidi ya mara ya mwisho kusinzia baada ya kutazama runinga kwa muda mrefu.
.
.
**
.
.Saa tatu usiku …
.
.
Walikuwa sebuleni wanakula chakula cha usiku. Walikuwa wamekawia kula leo maana chakula kiliandaliwa kwa kuchelewa. Kulikuwa ni kimya mbali na sauti ya vijiko vikigonga sahani na midomo ikitafuna.
.
.
Brian alikuwa anamtaza Olivia mara kwa mara. Macho yake hayakukaa muda pasipo kuangukia kwa mtoto huyo. Bado alikuwa na hofu naye. Alidhani pengine aweza badilika kuwa kama alivyokuwa muda ule, lakini haikuwa hivyo mpaka wanaelekea kumaliza kula.
.
.
“Brian,” mama akaita. Yeye alikuwa ashamaliza kula. “Vipi msiba? Kila kitu kilienda sawa?”
.
.
Brian akatikisa kichwa pasipo kutia neno. Akaendelea kula.
.
.
“Tulitoka leo, kwenda nje kabisa ya mji. Ni kwasababu ya haya mambo yanayotokea, ila bahati haikuwa kwetu, hatukufanikisha!” mama alizungumza. Maongezi haya yakamvutia Brian, akamtazama mamaye na kumpa miamko yote impasayo mtu aliye makini.
Read more
Loading...
“Brian,” Wisconsin akaita kwa kunong’oneza. “Hakikisha macho yako yanamtazama Padri Alfonso ...
Media Removed
“Brian,” Wisconsin akaita kwa kunong’oneza. “Hakikisha macho yako yanamtazama Padri Alfonso muda wote, sawa?” Kabla Brian hajajibu, Padri Alfonso akageuka na kuwatazama kwa kuwakazia macho, na kisha akarejesha uso wake mbele. . . Brian akauliza, “Atakuwa amesikia?” Kabla Wisconsin ... “Brian,” Wisconsin akaita kwa kunong’oneza. “Hakikisha macho yako yanamtazama Padri Alfonso muda wote, sawa?” Kabla Brian hajajibu, Padri Alfonso akageuka na kuwatazama kwa kuwakazia macho, na kisha akarejesha uso wake mbele.
.
.
Brian akauliza, “Atakuwa amesikia?” Kabla Wisconsin hajajibu, wakamwona Padri Alfonso akitikisa kichwa. Wakashtuka na kutazamana kisha hawakuongea tena. .
.
Basi tangu hapo, Brian akawa anamtazama Padri Alfonso kwa woga. Kweli hakubandua macho yake. Hata alipoyafumba, akayafumbua upesi na kuendelea kukodoa.
.
.
Muda kidogo Wisconsin akampatia kikaratasi kidogo chenye ujumbe. Akaikichukua na kukisoma.
.
.
“Tutawasiliana kwa maandishi,” ujumbe ulisomeka vivyo. Akamtazama Wisconsin na kumtikisia kichwa kama ishara. Wisconsin akamwandikia pia Mama ujumbe kuwa watakuwa wanasiliana kwa maandishi, naye Mama akaelewa.
.
.
Muda ukasonga zaidi. Ilipopita lisaa limoja, shughuli za mazishi zikaanza rasmi baada ya ujio wa mwakilishi mkubwa wa serikali. Jeneza likafunguliwa, na watu wakaanza zoezi la kumuaga Brewster kwa mara ya mwisho kabla hajamezwa na udongo. .
.
‘Utaenda kuaga?’ Wisconsin akaandika ujumbe wake kwa peni na kumpatia Brian. .
.
‘Hapana, sitaenda,’ Brian akajibu na kurejesha karatasi. .
.
‘Kwanini?’
.
.
‘Naogopa.’
.
.
‘Umekuwa ukimtazama Padri Alfonso?’
.
.
Kabla Brian hajaandika kujibu, akarusha tena macho yake kumtafuta Padri Alfonso. Hakumwona. Akaangaza kushoto na kulia, hakumwona. Akastaajabu atakuwa ameenda wapi, mara yake ya mwisho kumwona alikuwa amesimama kandokando na jeneza.
.
.
Alipomkosa, akarejesha macho yake kwenye karatasi apate kumwandikia Wisconsin ujumbe. Ajabu alipotazama karatasi hiyo, akaikuta tayari ina maandishi. Haukuwa mwandiko wa Wisconsin!
.
.
‘Unanitafuta?’ Maandishi yalisomeka hivyo. Brian akahofia sana. Akarusha tena macho yake kuangaza, hakuona kitu. Aliporejesha tena macho yake kwenye karatasi akaukuta ujumbe mwingine, ‘Nipo nyumbani kwenu.’
Read more
“Usijali, Mrs Garett. Karibu.” . . “Brian, nina shida sana. Nahisi maisha yangu yapo hatarini.” . . Kauli ...
Media Removed
“Usijali, Mrs Garett. Karibu.” . . “Brian, nina shida sana. Nahisi maisha yangu yapo hatarini.” . . Kauli hii ya upesi na iliyosikika vema ilimfanya Brian na mama yake wawe wasikivu zaidi. . . “Baada ya mume wangu kufa, ni mimi ndiye yuaja. Naombeni mnisaidie.” Mrs Garett akaanza ... “Usijali, Mrs Garett. Karibu.”
.
.
“Brian, nina shida sana. Nahisi maisha yangu yapo hatarini.”
.
.
Kauli hii ya upesi na iliyosikika vema ilimfanya Brian na mama yake wawe wasikivu zaidi.
.
.
“Baada ya mume wangu kufa, ni mimi ndiye yuaja. Naombeni mnisaidie.” Mrs Garett akaanza kububujikwa na machozi. “Kecie anataka kuniua kama alivyomuua baba yake. Anawinda roho yangu!”
.
.
Brian na mamaye wakatazama kwa puzo. “Kwanini Kecie akuue?” Briana akauliza. “Na kwanini alimuua baba yake?”
.
.
Mrs Garett kwa kujikaza, akasema kila kitu. Hakutaka yale ya mficha maradhi. Alikuwa anataka msaada haswa. Alipomaliza kueleza, akajikuta anatoa machozi zaidi na kupaliwa na kilio. Alikuwa anamwomba msamaha mwanaye.
.
.
Lakini kwanini alidhani Brian anaweza kumsaidia kwenye hilo?
.
.
“Ni wewe tu na sisi ndiyo hutokewa na Kecie. Lakini akija kwako hukuomba msaada. Akija kwetu hudai roho zetu,” alisema Mrs Garett akitoa macho yake mekundu. “Kama Kecie hukuskiza wewe, naomba utuombee msamaha, Brian!”
.
.
Mama Brian akamtazama mwanaye na kumuuliza, “Kecie, hukuomba umsaidie?”
.
.
“Ndio,” Brian akajibu na kuongezea, “Huniomba nimwokoe!”
.
.
“Umwokoe wapi? Kutoka kwa nani?”
.
.
Brian akamtazama mama yake na kumwambia, “Toka kwa Helo.”
.
.
“Ndiyo nani huyo?”
.
.
Kabla Brian hajajibu, akaona kitu dirishani.
.
.
.
***
.
.
LAKO JICHO
Read more
ILIPOISHIA . . “Ndio, naahidi hilo,” Brian akajibu. Basi Wayde akaingiza tena mkono wake mfukoni ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . “Ndio, naahidi hilo,” Brian akajibu. Basi Wayde akaingiza tena mkono wake mfukoni na kutoa ufunguo wa ziada. Ufunguo mdogo wa shaba. Akafungua mlango mwingine ndani ya chumba hicho cha siri, humo Brian akaona jambo lililomshangaza. . . Maiti za watu watatu! . . “Wayde, ... ILIPOISHIA
.
.
“Ndio, naahidi hilo,” Brian akajibu. Basi Wayde akaingiza tena mkono wake mfukoni na kutoa ufunguo wa ziada. Ufunguo mdogo wa shaba. Akafungua mlango mwingine ndani ya chumba hicho cha siri, humo Brian akaona jambo lililomshangaza. .
.
Maiti za watu watatu!
.
.
“Wayde, ni nini hicho?” Brian akastaajabu. Wayde akamjibu huku akimtazama, “ni watoto wa Helo!”
.
.
ENDELEA
.
.
Brian aliyekuwa amepigwa na tahamaki, akajikaza kisabuni kutazama maiti zile. Hakuwa anazifahamu, na hapo ndipo akagundua ya kuwa, Brewster na Alfonso hawakuwa watoto wa Helo, kitu ambacho alikuwa anakiwaza muda wote huo.
.
.
“Nahisi hii ndiyo sababu familia yetu imekuwa salama dhidi ya Helo,” alisema Wayde huku akijongea zile maiti. Zilikuwa zimehifadhiwa kwenye kioo baada ya kukaushwa. Kama maiti hizi zingekuwa zimefungua macho basi ungeweza dhani bado ni watu waliohai.
.
.
Wayde akampatia Brian karatasi fulani na kumwambia, “Nadhani unatakiwa kuliona na hili.” Brian akaitazama karatasi aliyopewa. Ilikuwa ni barua ya kale ambayo baba yake Wayde alitumiwa na mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Magreth Woodland. Katika barua hiyo, huyo mwanamke alikuwa anamweleza baba yake Wayde, seneta wa Massachusetts, namna gani anavyompenda lakini pia akiwa hatarini kutokana na mapenzi yake kwake. .
.
Ya kuwa mume wake anaonekana kuyajua mahusiano yao, amemuuliza mara kadhaa akakanusha, inawapasa wawe makini kuanzia muda huo kwa usalama wao kwani asingependa kumharibia picha ya kisiasa ya mwanaume huyo kwani ni mtu mkubwa kwenye siasa za Marekani. Kipindi hicho bado baba yake na Wayde hakuwa seneta, bali mwenye mipango ya kuwa.
.
.
Brian akamuuliza Wayde, “Magreth ni nani?” Kabla Wayde hajajibu, akampatia tena Brian barua ya pili, hii ilikuwa fupi tofati na ile ya kwanza, pia ilikuwa imetokea kwa Magreth Woodland akimshukuru baba yake Wayde kwa kumletea zawadi ya mkufu wa thamani.
Read more
Brian akatazama pembeni kwa mafikirio, alafu akaurudisha uso wake kwa Wisconsin na kuuliza, “Ina ...
Media Removed
Brian akatazama pembeni kwa mafikirio, alafu akaurudisha uso wake kwa Wisconsin na kuuliza, “Ina maana hamna kabisa namna?” kabla hajajibiwa, akaongeza, “Olivia ni msichana mzuri sana. Natamani angelikuwa kwenye ulimwengu wetu.” . . Wisconsin akamshika mkono na kumminya kidogo. ... Brian akatazama pembeni kwa mafikirio, alafu akaurudisha uso wake kwa Wisconsin na kuuliza, “Ina maana hamna kabisa namna?” kabla hajajibiwa, akaongeza, “Olivia ni msichana mzuri sana. Natamani angelikuwa kwenye ulimwengu wetu.”
.
.
Wisconsin akamshika mkono na kumminya kidogo. “Najua, Brian. Hata mimi natamani ikawa hivyo … ila tutafanya kadiri ya uwezo wetu.” Brian akanyamaza. Kuna jambo alikuwa anawaza kichwani. Wisconsin akamtazama na kumwambia, “Inabidi unyanyuke hapa tukaonane na yule binti. Sawa?”
.
.
.
**
.
.
Saa nane mchana, nje ya uzio wa shule …
.
.
Wanafunzi walikuwa wanatoka kwenda majumbani. Kandokando ya geti, alikuwa amesimama Brian pamoja na Wisconsin. Walikuwa wanatazamia wanafunzi wapungue ili wazame ndani. .
.
Baada ya muda kidogo, wakaingia na kabla hawajaenda mbali wakaliona gari la Wayde likiwa linasonga kwenda zake. Brian akalipungia mkono na kwenda moja kwa moja kulifuata.
.
.
Wakaingia ndani ya gari, Wayde akaendesha kuacha nyuma shule. Alipotembea kwa dakika kadhaa, akaegesha gari kando na kumtaka Brian amwelezee kinachoendelea. .
.
“Huyu ni Wisconsin, yeye ni mtaalamu wa yale mambo tuliyokuwa tunayazungumzia. Anahitaji kuona vile vitu ulivyonionyesha jana.”
.
.
Wayde akamtazama Wisconsin na kumsalimu, kisha akarejesha uso wake kwa Brian na kumwambia, “sidhani kama itawezekana, Brian.”
.
.
“Kwanini?”
.
.
“Leo baba anarejea tokea Carolina. Hapa tuongeapo, yupo safarini kurudi. Ni hatari!” Wayde alizungumza akiwa amekodoa macho. Wisconsin akaingilia maongezi,
.
.
“Kama kuna nafasi, basi ni hii! Yatupasa kufanya kila jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu. Tukishindwa leo, basi tutakuwa tumeshindwa milele. Kitakuwa ni kiama cha Boston.”
.
.
Brian akamtazama Wayde. Wakatazamana kwa kama sekunde tatu kisha Wayde akashusha pumzi ndefu na kutazama mbele akiwa ameshika usukani. Akakuna kichwa chake kwanguvu. Akatulia kwa muda kidogo na kusema, “Sawa.”
.
.
Alafu akawatazama wageni wake na kuwaambia, “ila sitaweza kwenda nanyi wote.”
Read more
Baada ya kusema hivyo, Karen akaanza kujieleza na hakuchukua muda mrefu macho yake yakaanza kumimina ...
Media Removed
Baada ya kusema hivyo, Karen akaanza kujieleza na hakuchukua muda mrefu macho yake yakaanza kumimina machozi. Sauti yake ilikuwa nyembamba inayotetemeka. . . “ … amekuja kunifuata. Nimekuta jumbe zake kwenye dawati la kazini akiniambia ni mimi ndiye nitafuata kufa.” Karen akiwa anatumia ... Baada ya kusema hivyo, Karen akaanza kujieleza na hakuchukua muda mrefu macho yake yakaanza kumimina machozi. Sauti yake ilikuwa nyembamba inayotetemeka. .
.
“ … amekuja kunifuata. Nimekuta jumbe zake kwenye dawati la kazini akiniambia ni mimi ndiye nitafuata kufa.” Karen akiwa anatumia mkono wake unaotetemeka, akawapatia Brian na Wisconsin karatasi mbili. Wakazisoma na zote zikiwa na jumbe moja, “ NI WEWE NDIYE UTAFUATA.” karatasi zote zikiwa zimefanana na zile zile ambazo yule mtangazaji wa awali alikuwa anazipata. .
.
Lakini, .
.
“Msichana yule aliyefanyiwa mahojiano, yupo wapi?” Wisconsin akauliza maana walikuwa wametingwa sana na hoja za yule mtangazaji na yale yanayotokea mpaka kusahau kabisa kuwa kuna yule binti ambaye naye anaweza kuwa muhimu kwao.
.
.
“Sijui,” Karen akajibu. “Mimi ni mdada wa mapokezi tu, siyajui mengi kuhusu mengine.”
.
.
"Umewaambia utawala juu ya tishio lako? Umewataarifu polisi?” Wisconsin akaongezea swali. .
.
“Sijamtaarifu yeyote yule,” Karen akajibu. “Hamna atakayeniamini. Najua, hamna atayesadiki maneno yangu. Ni nyie tu!”
.
.
Wisconsin akamtazama Mama Brian. Hawakutia neno. Basi Karen akakaribishwa kwenye nyumba ile kulala mpaka hapo atakapohisi kuwa yu salama. Lakini je hilo litamwokoa dhidi ya ahadi ya muuaji?
.
.
Mshale wa saa ulipokomea kwenye majira ya saa nane usiku, Brian aligutuka toka usingizi. Hakujua ni nini kilimwamsha, ila alijikuta akihisi upepo wa baridi. Kando yake alikuwa amelala Wisconsin ambaye alimpisha Karen alale kwenye chumba chake. .
.
Brian akaangaza kushoto na kulia, kisha akaamka na kusimamia miguu yake. Akajongea dirisha na kutazama nje. Kulikuwa kimya, kumetulia haswa. Akiwa hapo, akasikia mlango unafunguliwa. Haraka akageuka na kutazama mlango wa chumba chao. Haukuwa huo!
Read more
Loading...
Wayde alilipeleka kushoto na kulia, kushoto na kulia. Bado Olivia alikuwa darini. Akalichochea ...
Media Removed
Wayde alilipeleka kushoto na kulia, kushoto na kulia. Bado Olivia alikuwa darini. Akalichochea kwa usawa, kisha akaminya breki kali, hapo Olivia akatupiwa kwa mbele kama mzigo, ila ajabu mikono yake ikawa imebaki imeng'ang'ania dari! . . Wayde hakupoa, akaminya mafuta na kumsigina ... Wayde alilipeleka kushoto na kulia, kushoto na kulia. Bado Olivia alikuwa darini. Akalichochea kwa usawa, kisha akaminya breki kali, hapo Olivia akatupiwa kwa mbele kama mzigo, ila ajabu mikono yake ikawa imebaki imeng'ang'ania dari!
.
.
Wayde hakupoa, akaminya mafuta na kumsigina kiumbe huyo. Kama haitoshi, akarudisha tena gari nyuma na kumkanyaga, kisha akapeleka tena mbele na kumkanyaga. Olivia akawa chapati! .
.
Wakatoka zao msituni.
.
.
.
**
.
.
.
"Ni lazima usiku huu uwe wetu!" Alisema Wisconsin. Alifungua kitabu upesi Brian na Wayde wakiwa kando, na mara kidogo Mama Brian akaungana nao akitokea chumbani.
.
.
"Karen yupo wapi?" Brian akauliza.
.
.
"Hajarudi tokea kazini," Mama akamjibu akiketi. Wisconsin akawaagiza walete mshuma na wafunge madirisha na milango yote. Maagizo yake yakatiiwa upesi basi akaanza kusoma kile alichokuwa anakitazama kwenye kitabu.
.
.
.
**
.
.
.
Bado kulikuwa kimya ndani ya chumba. Hakuwa amepata msaada wowote tangu mwanaye, Wayde, amwache hapo chini. Macho yake yaliyokuwa yanarembua yalikuwa yanatazama kile kioo kilichohodhi miili ya wafu. Hakuwa anayatoa macho hapo. Hata alipoyafumba, akayafumbulia papo hapo
.
.
Ni kana kwamba kuna kitu alikuwa anangoja.
.
.
Akiwa anaendelea kutazama, mara akaanza kuona kioo hicho kikichipua ufa!  Akakoroma akitaka kusema jambo lakini hakuwa anaweza. Kioo kikaendelea kuchipua ufa zaidi na zaidi. Na mmoja wa mwili uliokuwemo ndani ukaanza kujigusa. Ukachezesha kidole!
.
.
Ukafuatiwa na mwingine, ukachezesha jicho!
.
.
.
**
.
.
Lako jicho!
Read more
ILIPOISHIA . . “Umwokoe wapi? Kutoka kwa nani?” . . Brian akamtazama mama yake na kumwambia, ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . “Umwokoe wapi? Kutoka kwa nani?” . . Brian akamtazama mama yake na kumwambia, “Toka kwa Helo.” . . “Ndiyo nani huyo?” . . Kabla Brian hajajibu, akaona kitu dirishani. . . ENDELEA . . Alikuwa ni mtoto akiwa amesimama na mwanaume mweusi asiyeonekana lakini ... ILIPOISHIA
.
.
“Umwokoe wapi? Kutoka kwa nani?”
.
.
Brian akamtazama mama yake na kumwambia, “Toka kwa Helo.”
.
.
“Ndiyo nani huyo?”
.
.
Kabla Brian hajajibu, akaona kitu dirishani.
.
.
ENDELEA
.
.
Alikuwa ni mtoto akiwa amesimama na mwanaume mweusi asiyeonekana lakini wenziwe walipoangazia huko, hawakuona kitu! Kila kitu kilikuwa kimepotea katika kasi ya kufumba na kufumbua.
.
.
“Kuna nini, Brian?” Mama yake akauliza.
.
.
“Kulikuwa na mtoto akiwa amesimama pale na kando yake kuna mtu!” akasema Brian akinyooshea kidole kule dirishani. Ila hakukuwa tena na kitu! Na si kwamba watu hawakumwamini, la hasha. Ni kwamba tu hawakufanikiwa kushuhudia.
.
.
“Brian! Kecie atakuwa ananifuata mimi!” akasema Mrs Garett akijawa na woga. Aliangazaangaza huku na huko. Hakuwa na amani. Hofu aliyokuwa nayo ilikuwa ni ile iliyo kuu. .
.
“Usijali, Mrs Garett!” Mama Brian akamfariji. “Leo utalala hapa wewe pamoja na Olivia. Nadhani msiba wa mumeo utakuwa umekuathiri.”
.
.
Mama hao wakakumbatiana. Mama Brian akaendea chai ya Brian na ya kwake wakaendelea kukaa hapo wakiteta. Lakini kila saa Mrs Garett akawa anamsisitizia Brian ya kwamba endapo Kecie akijiri basi amwambie ya kwamba anaomba msamaha. Ambakizie roho yake.
.
.
Usiku ukazidi kukua na mwishowe kabisa wakaenda kulala. Mrs Garett alienda kulala na Mama Brian huku Olivia na Brian kila mmoja akilala chumba chake. .
.
Usiku huo wakati watu wakipambania kupata usingizi, Brian yeye akawa ndiyo anautumia huo muda kusoma zile nyaraka za Dkt Hamill. Zilikuwa ni za kuogopesha lakini hakuwa anataka kuzieka chini mpaka kumaliza. Haikuwa kazi nyepesi. .
.
Basi na sehemu ya nyaraka hii yasomeka kama ifuatavyo …
.
.
“… Kifo kina wivu sana. Kinatutenga na wale tuwapendao. Kimeniacha na kidonda kikubwa sana kwani kichwa changu kimekuwa hakikomi kuwaza na kukumbuka matabasamu ya mke na watoto wangu. Waliniacha kipindi nawahitaji sana. Pengine waweza kuwa unanionea huruma, lakini utakapomaliza kusoma haya, labda utaniona mimi ni mkatili sana. Mtu asiyestahili huruma hata lepe.
.
Read more
Loading...
ILIPOISHIA . . “Mimi sikuwa wa kuletwa hospitalini,” Dkt Hamill akasema kwa shida. Akageuza ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . “Mimi sikuwa wa kuletwa hospitalini,” Dkt Hamill akasema kwa shida. Akageuza shingo yake kumtazama Brian. Akamtazama kwa sekunde kadhaa alafu ‘lips’ yake kavu ikasema, “Brian, sasa nitakuwa nimelaaniwa.” . . “Na nani?” Brian akauliza kwa pupa. Dkt Hamill akakohoa ... ILIPOISHIA
.
.
“Mimi sikuwa wa kuletwa hospitalini,” Dkt Hamill akasema kwa shida. Akageuza shingo yake kumtazama Brian. Akamtazama kwa sekunde kadhaa alafu ‘lips’ yake kavu ikasema, “Brian, sasa nitakuwa nimelaaniwa.”
.
.
“Na nani?” Brian akauliza kwa pupa. Dkt Hamill akakohoa kwanza kisha akatafuta hewa yake na kusema, “Nitakuwa nimelaaniwa na Helo … Brian, maisha yangu hayatakuwa sawa tena.”
.
.
ENDELEA
.
.
Brian akashangazwa na maneno hayo. Akamuuliza Dkt Hamill kwanini anasema hivyo? Je kuvunja tu dirisha ndiyo imekuwa ya kupata laana?
.
.
“Hapana, Brian!” akasema Dkt Hamill kisha akakohoa kidogo. Ilikuwa ni ngumu kuamini kama ameletwa hospitali leo. Ungeweza kudhani ni mgonjwa wa muda.
.
.
“ … Ni damu. Ni damu yangu iliyobaki kule,” akasema Dkt kisha akatulia kama mtu anayeishiwa pumzi, sasa anaitafuta. “Nilijua toka nilipokuwa nimejakata pale. Hayakuwa mazingira ya kawaida. Lakini bado tulifanya busara kuondoka mapema. Huenda mambo yangekuwa mabaya zaidi.”
.
.
“Nisamehe, Dkt Hamill,” Brian akalia. “Kama isingalikuwa mimi yote haya yasingejiri. Laiti ningekusikiliza …”
.
.
“Ssshhh! …” Dkt Hamill akamnyamazisha Brian. “Huna haja ya kulia Brian. Hakuna kosa lolote ulilolifanya kwani kama mimi nisngetaka kwenda mule ndani basi nisingelikwenda.” akamshika Brian mkono na kumminya akimtazama kwa sura inayojitahidi kuumba tabasamu.
.
.
“Brian, wewe ni kijana mwerevu lakini pia shupavu sana. Nimefurahi mno kukutana na wewe. Si vijana wengi wako kama wewe. Una kitu ndani yako. Najua unataka kuyajua mengi sana. Ila …” akakohoa. “Tazama yasije yakakugharimu.”
.
.
Aliposema hayo akatulia kwa dakika moja, alikuwa anatazama chumba alicholaziwa kana kwamba ni kipya machoni. Aliporejesha macho yake kwa Brian, akasema, “Ni bora nikafa.”
Read more
Kauli hiyo ikamshtua Brian, “Kwanini unasema hivyo, Dkt Hamill? Tafadhali usiseme hivyo!” . . Dkt ...
Media Removed
Kauli hiyo ikamshtua Brian, “Kwanini unasema hivyo, Dkt Hamill? Tafadhali usiseme hivyo!” . . Dkt akatabasamu. Akamtazama Brian aliyekuwa na sura ya hofu kisha akasema, “Brian, mimi ni mzee sasa. Si kama wewe. Wewe bado damu yako yazunguka, mwili wako una joto na hata akili yako inayoendelea ... Kauli hiyo ikamshtua Brian, “Kwanini unasema hivyo, Dkt Hamill? Tafadhali usiseme hivyo!”
.
.
Dkt akatabasamu. Akamtazama Brian aliyekuwa na sura ya hofu kisha akasema, “Brian, mimi ni mzee sasa. Si kama wewe. Wewe bado damu yako yazunguka, mwili wako una joto na hata akili yako inayoendelea kukua inafanya kazi upesi. .
.
Hutonihitaji tena mimi, Brian. Niliyokupa yanatosha. Nashukuru sana kwa kuwa na mimi japo kwa kipindi kifupi, umenipa faraja na ‘kampani’ ya rafiki.”
.
.
Hapa ndipo Brian akajifunza ya kuwa Dkt Hamill hana familia. Yu mpweke sana na amekuwa akiishi hivyo kwa miaka mingi sasa. Mke na watoto wake wote walikufa lakini hakumwambia Brian nini kiliwaua. .
.
Kauli yake ya mwisho alimwagiza Brian aende nyumbani kwake, akamwelekeza wapi atapata ufunguo, azame ndani na kumletea nyaraka zake tatu kwenye kabati.
.
.
Brian akitumia gari la Dkt Hamill, akaelekea huko, kulikuwa ni kingoni mwa mji wa Boston. Akaukuta ufunguo alipoelekezwa, akazama ndani na kunyookea kwenye kabati. .
.
Ilikuwa ni nyumba kubwa yenye vyumba takribani vitano ila vyote vikifungwa isipokuwa kimoja tu alimokuwa anaishi Dkt Hamill mwenyewe. Nyumba hiyo ilikuwa kubwa na kimya sana. Pia pweke. Brian alishangazwa namna gani Dkt Hamill alikuwa anaweza kuishi mwenyewe hapo.
.
.
Asipeleleze sana, akarudi kwenye gari na kuanza safari ya kurudi hospitali. Alichukua takribani dakika kumi tu kutokana na mwendo wake wa kasi. Alipofika, ajabu hakumkuta Dkt Hamill. Dokta akamwambia tayari mzee huyo amekufa, amehifadhiwa mochwari.
.
.
Akashindwa kuzuia chozi. Akajihisi kuishiwa na nguvu. Aliketi kwenye benchi kama mtoto yatima akiwa na kujiona mpumbavu kwa namna alivyofanya mzee huyo akafariki. Alijiona muuaji. Alijiona mwenye makosa.
.
.
Macho yake yakiwa yamejawa na machozi yaliyomfanya asione vema, Dokta akamjia na kumgusa bega. Akamkabidhi karatasi fulani na kumwambia, “Ni ujumbe wako alinambia nikupatie punde utakaporudi hapa.”
.
.
Kabla Dokta hajaondoka akamshika Brian begani mara mbili kumpa pole.
Read more
Basi Dkt Hamill akatabasamu na kisha akalaza mgongo wake kwenye kiti. Akamtazama Brian kwa sekunde ...
Media Removed
Basi Dkt Hamill akatabasamu na kisha akalaza mgongo wake kwenye kiti. Akamtazama Brian kwa sekunde kadhaa na kumwambia, “Kwasababu umetaka kuyafahamu, basi n’takujuza … Ila, ni kheri ukachunga sana mdomo wako. Najua kwenu vijana ni ajabu na ni ngumu sana kufanya hilo. Punde mjuapo jambo, ... Basi Dkt Hamill akatabasamu na kisha akalaza mgongo wake kwenye kiti. Akamtazama Brian kwa sekunde kadhaa na kumwambia, “Kwasababu umetaka kuyafahamu, basi n’takujuza … Ila, ni kheri ukachunga sana mdomo wako. Najua kwenu vijana ni ajabu na ni ngumu sana kufanya hilo. Punde mjuapo jambo, basi mwataka mji mzima ufahamu. Lah! .
.
Si kila kitu ni cha kuwa bayana, Brian. Na naomba sana ushike hilo neno. Nimesemaje? …”
.
.
“Si kila kitu cha kuwa bayana, Dokta.”
.
.
“Sawasawa. Basi nami nitakueleza mambo hayo ya kale na ya kutisha. Na nitakueleza hayo kwa siku na siku, siwezi kuyamaliza yote kwa siku moja. Huenda si simulizi ndefu sana, ila ni kwasababu ya muda wangu. Sina muda wa kutosha. Hata haya nafanya kwakuwa wataka sana kufahamu.”
.
.
Aliposema hayo, akanyamaza kwa sekunde kadhaa. Akasafisha koo lake na kisha akatazama chini. .
.
“Ni zamani sana ndani ya Boston. Bila shaka ni watu wachache sana walioshuhudia hayo wapo hai mpaka sasa. Hapa hakukuwa na watu wengi kiasi hiki cha leo. Kulikuwa na watu wachache hapa na pale na pia makazi.
.
.
Basi miongoni mwa familia hizo zilizokuwapo hapa, kulikuwa kuna familia moja ya kilatini ya bwana maarufu aliyekuwa anaitwa Hernandez Lorenzo, ama wengi wakimwita Helo kwa ufupi. .
.
Bwana huyo alikuwa maarufu kwa michezo yake ya mazingaombwe katika eneo hili zima la Boston na hata Massachusetts nzima. Kila mtu alikuwa anampenda na kumtukuza. Banda lake lilikuwa linajaa kila mwisho wa wiki wa ajili ya kutumbuiza kiasi kwamba lilikuwa linatanuliwa kila mwisho wa mwezi kukidhi idadi ya watu.
.
.
Mitaani na hata huko barabarani watu wakawa wanaita jina lake. Helo! - Mtu wa maajabu!! Helo - Mtu wa maajabu!! Mtu huyo akavutia watu wengi sana kuja Boston, kumjua na hata kumfurahia. Familia yake ikawa maarufu sana, na si tu hivyo, wakawa matajiri sana.
Read more
Basi Brian akaona shughuli imetiwa doa, akafunga kila kitu na kwenda zake nyumbani, akiwa na maswali ...
Media Removed
Basi Brian akaona shughuli imetiwa doa, akafunga kila kitu na kwenda zake nyumbani, akiwa na maswali juu ya Brewster. . . Alipofika, kwakuwa alikuwa na njaa, akaendea jikoni na kupakua chakula. Alimkuta Olivia pekee sebuleni anatazama televisheni. . . “Wapo wapi hawa?” akamuuliza ... Basi Brian akaona shughuli imetiwa doa, akafunga kila kitu na kwenda zake nyumbani, akiwa na maswali juu ya Brewster. .
.
Alipofika, kwakuwa alikuwa na njaa, akaendea jikoni na kupakua chakula. Alimkuta Olivia pekee sebuleni anatazama televisheni. .
.
“Wapo wapi hawa?” akamuuliza akitafuna. .
.
“Wametoka,” Olivia akamjibu kwa ufupi.
.
.
Hapa ndipo Brian akakumbukua kuwa gari halikuwapo nje. .
.
“Wameenda wapi?”
.
.
Olivia akapandisha mabega juu pasipo kutia neno, hakuwa anamtazama Brian. Basi Brian akaendelea kula, lakini ghafla kuna kitu kikamjia kichwani. Hakujua kwanini, ila alijikuta akikumbuka tukio la ajali ya Mr Garett!
.
.
Aliyakumbuka yale maneno ya Mrs Garett kuwa bwana wake alimwambia kuwa Kecie anawinda roho yao kabla hajafariki, punde ndogo baada ya kupata ajali ya gari. .
.
Basi Brian akajikuta anakosa amani. Hata chakula hakukimaliza, akakiweka kando.
.
.
“Wametoka muda mrefu?” Akauliza.
.
.
“Tangu asubuhi,” Olivia akajibu, bado akiwa anatazama televisheni. Ila sauti yake ilikuwa tofauti kidogo. Hili kwa kiasi likampa mashaka Brian. Akaita, “Olivia!”
.
.
Olivia akaitikia. Hakumtazama Brian. Uso wake ulikuwa umeng’ang’ania kutazama televisheni.
.
.
“Olivia, nitazame.”
.
.
Olivia akakaa kimya. Hakutikisika wala kupepesuka. Brian akarudia kumwambia akimtaka ageuke. Mara hii Olivia akajibu kwa swali, “Kwanini nigeuke?” .
.
Sasa mara hii sauti yake ndiyo ilikuwa tofauti kabisa. Sauti nzito ya kiume! Brian akajikuta akishtuka mno. .
.
.
***
.
.
.
LAKO JICHO
Read more
Loading...
“Unadhani watakuwa wapi?” Brian akauliza. Mkononi alikuwa amebebelea kijitabu na mkufu. . . “Sijajua ...
Media Removed
“Unadhani watakuwa wapi?” Brian akauliza. Mkononi alikuwa amebebelea kijitabu na mkufu. . . “Sijajua wapo wapi,” akajibu Wisconsin, “Ila nahisi watakuwa wazima.” . . “Kwanini unahisi hivyo?” Brian akauliza. “Dkt Hamill ameandika hilo kwenye diary yake?” . . “Hapana, hajaandika. ... “Unadhani watakuwa wapi?” Brian akauliza. Mkononi alikuwa amebebelea kijitabu na mkufu.
.
.
“Sijajua wapo wapi,” akajibu Wisconsin, “Ila nahisi watakuwa wazima.” .
.
“Kwanini unahisi hivyo?” Brian akauliza. “Dkt Hamill ameandika hilo kwenye diary yake?”
.
.
“Hapana, hajaandika. Lakini pia hajaandika watoto hao wapo wapi. Kwanini amzike mkewe ndani ya eneo la nyumba, na watoto wasijulikane kawapeleka wapi?”
.
.
Brian hakuwa na majibu. Wisconsin akavuta kiko chake na kutia neno, “Ni ajabu, maana hata hilo amelifanya kuwa siri ndani ya siri. Siri ambayo hata yeye hakutaka kuiandika ikajulikana kwa watu.”
.
.
“Sasa tutafanyaje kujua hilo?” Brian akauliza.
.
.
“Hatuna namna, Brian!” Wisconsin akatikisa kichwa. “Kwa sasa tuna kazi nyingi za kufanya, visa huwa haviishi ndani ya mji. Nilitaka tu kukuweka bayana juu ya hilo ila hatutadiriki kuhangaika nalo. Tumalize kwanza hili kumi lilipo mikononi mwetu.”
.
.
Basi baada ya maongezi hayo, Wisconsin akabadili mada na kumwambia Brian ya kwamba tangu Brewster alipofariki, hakuna mtoto yeyote aliyepotea ndani ya mji wa Boston. Hiyo ni ishara kuwa Helo atakuwa amedhoofu kwa mtu huyo kufa. Na endapo watafanikiwa kummaliza na Padri Alfonso, basi kazi itakuwa imekwisha. Atakachokifanya, yeye Brian, ni kwenda kule kwenye ulimwengu wa wafu, akamkabili na kummaliza Helo. .
.
“Lakini tutammalizaje Alfonso?” Brian akauliza. “Anaonekana ni mwenye nguvu, pengine kumzidi Brewster!”
.
.
“Ni kweli,” akajibu Wisconsin, “lakini lazima kutakuwa na njia. Mpaka kufikia kesho nitakuwa nimejua cha kufanya. Twende sasa, tumekaa sana hapa.”
.
.
**
.
.
“Afadhali mmekuja!” Alisema Mama akiwa amekodoa macho. Akawafungulia mlango Wisconsin na Brian kuingia ndani. Wakamwona Karen, dada wa mapokezi, akiwa amejaa kwenye kiti cha pekee, uso wake umeshikwa na wasiwasi.
.
.
“Karen amefika hapa muda si mrefu,” Mama akasema kwa pupa, “ameniletea ujumbe mzito sana. Naomba mumsikize.”
Read more
ILIPOISHIA . . Olivia akakaa kimya. Hakutikisika wala kupepesuka. Brian akarudia kumwambia ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . Olivia akakaa kimya. Hakutikisika wala kupepesuka. Brian akarudia kumwambia akimtaka ageuke. Mara hii Olivia akajibu kwa swali, “Kwanini nigeuke?” . . Sasa mara hii sauti yake ndiyo ilikuwa tofauti kabisa. Sauti nzito ya kiume! Brian akajikuta akishtuka mno. . . ENDELEA . . Moyo ... ILIPOISHIA
.
.
Olivia akakaa kimya. Hakutikisika wala kupepesuka. Brian akarudia kumwambia akimtaka ageuke. Mara hii Olivia akajibu kwa swali, “Kwanini nigeuke?” .
.
Sasa mara hii sauti yake ndiyo ilikuwa tofauti kabisa. Sauti nzito ya kiume! Brian akajikuta akishtuka mno. .
.
ENDELEA
.
.
Moyo wake ukaenda mbio na mwili wake ukaanza kutetemeka kwa fujo! Kufumba na kufumbua, Olivia akageuza shingo yake kumtazama Brian! Lakini namna ambavyo alikuwa amegeuza kichwa hiko ilikuwa ni ya ajabu haswa! Mwili wake bado ulikuwa unatazama upande ilipo runinga, lakini uso wake ukiwa umegeuka nyuma kabisa!
.
.
Kwa mtu ambaye ni mzima, hawezi kufanya hivi, labda tu awe amevunjika ajalini. Macho yake yalikuwa meusi ti! Mdomo wake ulikuwa mkavu kana kwamba muhogo uliotelekezwa juani.
.
.
“Nini unataka kujua, Brian?” Olivia akauliza kwa sauti yake ya ajabu. Brian akabaki akiwa ametoa macho. Anahema kana kwamba mbwa aliyetoka kukimbizwa.
.
.
“Nini unaogopa? Si umetaka nigeuke?”
.
.
“Wewe ni nani?” Brian akauliza. Alikuwa amejiminyia kochini nusura atokee upande wa pili.
.
.
“Mimi? - wataka kunijua mimi?” Olivia akauliza. Kwa haraka mwili wake ukageuka kufuata uso wake, akasimama na kumtazama Brian huku shingo yake ikiwa inakunjikakunjika hovyo kupeleka kichwa huku na kule.
.
.
“Mimi ni mwenyeji wako, Brian! Hunijui?” Olivia akauliza. Brian akiwa anatweta kwa hofu kuu, akatikisa kichwa chake upesi. Paji lake la uso lilikuwa linatiririsha jasho.
.
.
“Sikujui!” akasema. “Sikujui wewe ni nani!”
.
.
Olivia akaangua kicheko na mara akakunja tena sura yake kwa hasira. Akamtazama Brian kiupande. “Mimi ni mwenyeji wako!” akamwambia kwa sauti yake ya mashine. Macho yake yaliyokoza uweusi yakiwa yametoka nje mithili ya balbu!
.
.
“Ulikuja kwenye himaya yangu kun’tembelea … Je nataka kumtorosha mwanangu?”
.
.
“Mimi hata simju-!” Brian hakumalizia kauli yake, akasombwa yeye pamoja na kiti. Ilikuwa ni nguvu ya ajabu. Alibamiziwa ukutani pasipo hata kuguswa, akaja kujikuta akiwa chini anagugumia na maumivu.
Read more
ILIPOISHIA . . “Ndio,” akajibu Dokta, “Hiyo ndiyo maana yake, ndiyo maana nikashangazwa sana ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . “Ndio,” akajibu Dokta, “Hiyo ndiyo maana yake, ndiyo maana nikashangazwa sana na mahali ulipoyatolea hayo maneno. Ebu niambie uliyasikia wapi? Kuwa mkweli, pengine naweza kukusadia.” . . Dkt Hamill alimtazama Brian kwa macho ya kidadisi na hamu. Kabla Brian hajatia ... ILIPOISHIA
.
.
“Ndio,” akajibu Dokta, “Hiyo ndiyo maana yake, ndiyo maana nikashangazwa sana na mahali ulipoyatolea hayo maneno. Ebu niambie uliyasikia wapi? Kuwa mkweli, pengine naweza kukusadia.”
.
.
Dkt Hamill alimtazama Brian kwa macho ya kidadisi na hamu. Kabla Brian hajatia neno, akamuuliza, “Umeyasikia maneno hayo ndotoni au msituni?”
.
.
ENDELEA
.
.
“Sijayasikia huko,” Brian akatikisa kichwa chake. “Ni kutoka kwa rafiSki yangu anaitwa Faris. Yeye amekuwa mgonjwa hivi sasa, hawezi kusema jambo lolote akaeleweka. Niliona akiwa ameandika maneno hayo kwenye kingo yake ya kitanda!”
.
.
Dkt akanyamaza asitie neno. Aliminya tu lips zake na kuendelea kumtazama Brian.
.
.
“Dokta,” Brian akaita. “Waweza kunambia maana yake ni nini? Kwanini ameandika maneno hayo?”
.
.
Dokta akameza kwanza mate, kisha akamwambia Brian, “Muda wangu umekwisha. Sina muda tena wa kuongea na wewe. Tuonane kesho majira haya, sawa?”
.
.
“Lakini Dokta,” Brian akataka kuongea. Dkt Hamill akamzuia na kumkumbusha makubaliano yao ya mwanzoni kuwa maongezi hayo ni marefu na vivyo hatoyamaliza yote kwa siku moja. Basi Brian, kishingo upande, akanyanyuka na kuuendea mlango. Dokta akamkumbusha, “Usisahau kuja kesho. Uwe ndani ya muda.”
.
.
Akatikisa kichwa chake kuitikia na kisha akaenda zake. Siku hiyo alikuwa amegundua kitu kikubwa lakini kilichompa hofu zaidi. Alijikuta akitaka kufahamu zaidi kuhusu Halo, na je kuna mahusiano gani kati ya Halo na Faris? Na labda kupotea kwa Kecie msituni?
.
.
Wakati anajiuliza hayo akaona ni vema kama asipomficha kitu Dkt Hamill. Inabidi amweke wazi, labda atakuwa anfahamu kila shaka alilo nalo kichwani. Basi akaapa kesho yake atakapopata fursa ya kuonana na Dkt Hamill atahakikisha analifanyia kazi shauri lake.
Read more
Loading...
ILIPOISHIA . . Akiwa anaendelea kutazama, mara akaanza kuona kioo hicho kikichipua ufa!  Akakoroma ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . Akiwa anaendelea kutazama, mara akaanza kuona kioo hicho kikichipua ufa!  Akakoroma akitaka kusema jambo lakini hakuwa anaweza. Kioo kikaendelea kuchipua ufa zaidi na zaidi. Na mmoja wa mwili uliokuwemo ndani ukaanza kujigusa. Ukachezesha kidole! . . Ukafuatiwa ... ILIPOISHIA
.
.
Akiwa anaendelea kutazama, mara akaanza kuona kioo hicho kikichipua ufa!  Akakoroma akitaka kusema jambo lakini hakuwa anaweza. Kioo kikaendelea kuchipua ufa zaidi na zaidi. Na mmoja wa mwili uliokuwemo ndani ukaanza kujigusa. Ukachezesha kidole!
.
.
Ukafuatiwa na mwingine, ukachezesha jicho!
.
.
ENDELEA
.
.
Baba yake Wayde akatamani kunyanyuka azuie anachokiona, ila hakuwa anaweza. Hata kusogeza tu mwili wake ulikuwa ni mtihani, angewezaje kunyanyuka? Akabaki akigugumia, macho yakimtoka machozi zaidi na zaidi kutengeneza mto. Ni punde, kioo kikavunjika na wale walio wafu wakawa wazima!
.
.
Wakasimama kwa miguu yao. Wakatazama kwa macho yao! Ajabu ni kwamba viumbe hivi havikuwa vikipumua, wala mapigo yao ya moyo hayakuwa yanaita. Miili yao ilikuwa ya baridi na macho yao yalitingwa na mboni zenye rangi ya maziwa yaliyoharibika.
.
.
Wakamtazama yule mzee pale chini, wasiwe na habari naye, wakajiendea isijulikane wapi wanaelekea.
.
.
**
.
.
Wakiwa wameshikana mikono, kwa pamoja wakamalizia kusoma kifungu cha mwisho ambacho Wisconsin alielekezea. Wakiwa wanasoma kifungu hicho, mshumaa ukaanza kufifia, mapazia yakapeperuka kwa upepo, na milango ikaanza kucheza yenyewe.
.
.
Hawakukoma, wakamaliza kusoma kabisa, kisha Wisconsin akamchanja Brian kidole gumba na kuchuruzia damu kwenye ukurasa ule waliokuwa wameusoma. Ajabu pakaanza kufuka moshi mweusi karatasi likijifinya kuwa jivu.
.
.
Moshi huo Brian alipoutazama kwa sekunde kadhaa, akahisi anapoteza akili yake. Akahisi anapotelea moshini. Hata mwili wake ukaanza kupungukiwa nguvu. Alijishangaa kichwa chake kikidondoka kwa uzito na kujikuta chini!
.
.
Akiwa anapata fahamu, akasikia sauti za wadudu, na ngozi yake ikahisi kukalia majani. Akafungua kope zake nzito na kuangaza. Alikuwa kizani, na zaidi alikuwa msituni!
.
.
Akanyanyuka upesi na kutupa macho yake huku na kule. Akavuta pumzi ndefu na kujikuna kwa kuwashwa na majani, kisha akaanza kusonga kufuata mwanga anaouona kwa mbali.
Read more
ILIPOISHIA . . “Sasa tunafanyaje na ameondoka na vitu vile?” Dada Magdalena akauliza akiwa ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . “Sasa tunafanyaje na ameondoka na vitu vile?” Dada Magdalena akauliza akiwa na shaka. Padri Alfonso akatabasamu, “tunafanyaje? Yani unauliza tunafanyaje? Kwani hujui huwa tunafanyaje?” . . Dada Magdalena naye akatabasamu. . . Hawakutia tena neno lingine. . . ENDELEA . . Basi ... ILIPOISHIA
.
.
“Sasa tunafanyaje na ameondoka na vitu vile?” Dada Magdalena akauliza akiwa na shaka. Padri Alfonso akatabasamu, “tunafanyaje? Yani unauliza tunafanyaje? Kwani hujui huwa tunafanyaje?”
.
.
Dada Magdalena naye akatabasamu. .
.
Hawakutia tena neno lingine. .
.
ENDELEA
.
.
Basi afisa Randall akaenda kuonana na familia ya wakina Brian na kuwapa mrejesho wa kilichotokea, nao akawaambia wafike kituo cha polisi kesho asubuhi na mapema, alafu akaenda zake kupumzika.
.
.
Afisa Williamson alimshushia nyumbani na kutokomea kwenda kulaza usafiri wa polisi. Randall alikuwa amechoka sana kutokana na kazi za siku nzima. Baada ya kuingia nyumbani kwake, akala na kutulia kidogo sebuleni pamoja na mkewe, alafu muda si mrefu akaenda kupumzika kwa kujimwaga kitandani.
.
.
Hata hakuoga. Na muda si muda, akasombwa na usingizi kwa mkupuo. Hakusikia hata mkewe alipozima kila kitu na kuja kulala. Alikuwa usingizini haswa akikoroma na kuachama kinywa. .
.
Kwa mujibu wa saa yake ya sebuleni, mshale ukasonga na kujongea kwenye kituo cha nane usiku. Ulipofika hapo, Afisa Randall akajikuta anaamka toka usingizini asijue nini kimemwamsha kwani bado alikuwa na usingizi mzito. .
.
Akatazama kushoto kwake, akamwona mkewe akiwa amejilalia. Taa ilikuwa imezimwa na hali ilikuwa imetulia tuli kabisa. Hakusikia sauti ya kingine chochote kile zaidi ya pumzi ya mkewe ambaye aliyekuwa anahema kwa uzito.
.
.
Akarudisha kichwa chake kitandani na kufumba macho aendelee kulala, usingizi haukuja. Akajitahidi kuyafumba macho kwanguvu, lakini bado hakukuwa na kitu. Macho yaligoma kudaka usingizi abadani, .
.
Muda si mrefu, akasikia harufu fulani ambayo ilimfanya afungue macho na kutazamatazama chumbani. Ni kama kitu kinaungua ila kinanukia. Akanusanusa kama paka jikoni apate kutambua kitu hicho ni nini lakini hakufanikiwa.
Read more
ILIPOISHIA . . Mbali na hivyo, watu kadhaa, haswa majirani, walikuwa wametoka nje ya makazi ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . Mbali na hivyo, watu kadhaa, haswa majirani, walikuwa wametoka nje ya makazi yao wakitazama eneo la tukio kwa macho ya maulizo na nyuso za mashaka. Kulikuwa na zogo fulani midomoni mwao. . . Muda si mrefu gari ya wagonjwa ikawasili eneoni na kujitengenezea vema. Kutoka ... ILIPOISHIA
.
.
Mbali na hivyo, watu kadhaa, haswa majirani, walikuwa wametoka nje ya makazi yao wakitazama eneo la tukio kwa macho ya maulizo na nyuso za mashaka. Kulikuwa na zogo fulani midomoni mwao. .
.
Muda si mrefu gari ya wagonjwa ikawasili eneoni na kujitengenezea vema. Kutoka ndani ya nyumba, ikatolewa miili mitatu ambayo imefunikwa gubigubi, ikatiwa ndani ya gari la wagonjwa na kisha gari hilo kutimka. .
.
ENDELEA
.
.
Baadae ikaja kuwekwa bayana ya kuwa afisa Randall alikuwa amefariki, pia mke na mtoto wake mdogo aitwae Bestie. Na kama haitoshi, baadae taarifa zaidi zikaja juu ya kifo cha afisa Williamson. Alikutwa amekakamaa ndani ya chumba chake mwili wake ukiwa mweusi kabisa kana kwamba mtu aliyekitwa na shoti kubwa ya umeme.
.
.
Vifo vikawekwa bayana kwenye vyombo vya habari na karibia Boston nzima ikajuzwa. Misiba miwili iliyotokea ndani ya usiku mmoja. Na yote ikiwa imefanana mtindo, yaani muuaji hakuwa anajulikana.
.
.
Ila hakuwa anajulikana kweli?
.
.
“Padri Alfonso atakuwa ameshamuua,” alisema Brian aliyekuwa ameketi nyuma ya gari hili liendalo. Kwa mbele alikuwa ameketi Wisconsin na Mama ambaye alikuwa ameshikilia usukani. .
.
Katika majira haya ya asubuhi, walikuwa wanaelekea msibani. Msiba wa Brewster. Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mazishi yake kwa mujibu wa taarifa. Jana yake hawakupata muda wa kwenda msibani kutokana na kutingwa na shughuli zile za hapa na pale polisi.
.
.
“Mbaya zaidi amewaua wote,” akasema Mama. “Ameona awamalize kabisa kufuta ushahidi.”
.
.
Kidogo Wisconsin akasema, “ebu twendee kule kwenye kituo cha habari!” Mama akamtazama na kisha akarejesha uso wake haraka barabarani akiuliza, “kufanya nini huko?”
.
.
“Nahisi yule dada atakuwa mashakani,” Wisconsin akaeleza. “Kama wale polisi wameuawa wote, basi huenda pia akamuwinda na yule mwanamke ammalize!”
Read more
Loading...
. . ** . . . “Una uhakika?” Wisconsin aliuliza akiwa anamtazama Brian kwa kukodoa. . . “Ndio, ...
Media Removed
. . ** . . . “Una uhakika?” Wisconsin aliuliza akiwa anamtazama Brian kwa kukodoa. . . “Ndio, kila kitu nimekiona na kuhakikisha,” Brian akajieleza. Wisconsin akatulia kidogo akiwaza. Akanyanyua kikombe cha chai na kunywa mafundo matatu kisha akasafisha koo lake. . . “Kwanini ... .
.
**
.
.
.
“Una uhakika?” Wisconsin aliuliza akiwa anamtazama Brian kwa kukodoa. .
.
“Ndio, kila kitu nimekiona na kuhakikisha,” Brian akajieleza. Wisconsin akatulia kidogo akiwaza. Akanyanyua kikombe cha chai na kunywa mafundo matatu kisha akasafisha koo lake. .
.
“Kwanini Dkt Hamill aliwaua wanae?” Brian akauliza. Bado Wisconsin alikuwa amenyamaza kimya, anatazama huku na kule akiwaza. Baada ya sekunde kadhaa, akasema akinyanyuka, “Twende kwenye nyumba ya Dkt Hamill.”
.
. **
.
.
Baada ya dakika kumi na mbili …
.
.
“Ndiyo hapa,” akasema Wisconsin. Walikuwa tayari wapo ndani ya nyumba ya marehemu Dkt Hamill upande wa nyuma. Hapo walikuwa wamesimama kwenye kaburi la Magreth Woodland, mke wa Dkt Hamill. Mikononi mwao walikuwa wamebebelea chepeo za chuma na mikono yao imefunikwa na glovu nyeusi. .
.
Wakaanza kuchimba na kuchimba. Wakanyoosha migongo yao, wakakung’uta jasho, na kuendelea kuchimba. Haikuwa kazi nyepesi maana udongo ulikuwa mgumu wenye kujawa na kokoto. Waliweka vituo mara tatu kabla hawajafika chini kabisa. Ajabu hawakukuta kitu, si mabaki wala kitu chochote bali udongo mwekundu tu. Wisconsin akasema, “Dkt Hamill hakuwa amemzika mkewe ndani kama alivyoeleza kwenye diary.”
.
.
Brian akauliza, “Sasa atakuwa amemzika wapi?”
.
.
Wisconsin akanyamaza kidogo akiweka sawa mambo yake kichwani, alafu akasema, “Ndiyo maana Dkt Hamill aliwapoteza watoto wake, sasa napata maana.” Akamtazama Brian usoni na kusema, “Dkt Hamill atakuwa alienda kumtupia au kumfukia mkewe kule msituni. Na kwasababu hiyo basi, mkewe akaanza kutumika na Helo mpaka pale alipowatoa sadaka watoto wake watatu kumtumikia Helo.”
.
.
“Umeyajuaje hayo?” Brian akamuuliza. .
.
“Ni Magreth pekee ndiye aliyeuawa,” Wisconsin akasema akitikisa kichwa. “Na ndiyo maana kaburi lake lipo, au ndiyo maana Dkt Hamill akadanganya kuwapo kwa kaburi lake. Ila kuhusu wanawe, hao hawajauawa, bali walipotea. Hakuna namna nyingine ya kumtuliza Helo isipokuwa kwa sadaka tu, naye Hello aliwatoa sadaka wanawe.”
Read more
“Sawa,” Wisconsin akaitikia. “Nenda na Brian!” bado Wayde akawa anasita. Alilaza kichwa chake ...
Media Removed
“Sawa,” Wisconsin akaitikia. “Nenda na Brian!” bado Wayde akawa anasita. Alilaza kichwa chake kwenye kiti akiwaza, mwisho wa siku akasema yampasa aende mwenyewe. . . “Ni hatari kwenda na yeyote. Mama yu nyumbani pamoja na wageni wengine. Endapo nikirudi na yeyote, basi italeta shida. ... “Sawa,” Wisconsin akaitikia. “Nenda na Brian!” bado Wayde akawa anasita. Alilaza kichwa chake kwenye kiti akiwaza, mwisho wa siku akasema yampasa aende mwenyewe. .
.
“Ni hatari kwenda na yeyote. Mama yu nyumbani pamoja na wageni wengine. Endapo nikirudi na yeyote, basi italeta shida. Naomba niende mwenyewe.”
.
.
Brian akamtazama Wisconsin.
.
.
“Sawa,” Wisconsin akajibu na kuongeza, “Basi itabidi twende kwanza nyumbani.”
.
.
Wakaelekea nyumbani kwa wakina Brian, Wisconsin akampatia Wayde kitabu chake cha maarifa na kumwelekeza cha kufanya pindi atakapokuwa karibu na maiti zile zilizotiwa komeoni. Alipomaliza na Wayde kujiridhisha kuwa ameyashika maelekezo hayo, akaenda zake.
.
.
Wakamtazama msichana huyo akiishia. .
.
“Unadhani ataweza?” Brian akauliza wakiwa wanatazama barabara.
.
.
“Ataweza,” Wisconsin akamjibu. “Anaonekana ni msichana mwerevu sana, pia mwenye kujiamini … nadhani ataweza.”
.
.
Brian hakuongeza neno. Aliendelea kuangalia barabara. Wisconsin akamtazama na kumwambia, “inaonekana anakupenda sana.”
.
.
“Kwanini?” Brian akamuuliza akimtazama. Wisconsin akatabasamu na kumshika bega, “Ameyafanya haya kwakuwa anakupenda. Si kingine.”
.
.
** .
.
Saa kumi jioni …
.
.
Baada ya kutazama mazingira na kuyaona yapo salama, Wayde alizama ndani ya chumba cha wazazi wake na kuiba ufunguo, kisha akanyata kutoka, na upesi akakimbia kupandisha kule juu ilipo maktaba. Akafungua mlango wa kwanza, akazama ukumbini, akaufungua tena ule wa pili, wa siri, akazama ndani, kisha akaelekea ile miili ya wafu. .
.
Hapo akaitazama, akavuta na kushusha pumzi ndefu kisha akayafumba macho yake na kunyamaza kwa sekunde tano. Akivuta hewa na kushusha. Kabla hajafungua mdomo wake kunena, akasikia honi huko nje! Akashtuka na kukurupuka. .

Akatoka ndani ya chumba kile upesi na kurudi kule maktaba kutazama kupitia dirishani. Akaona gari la baba yake likiingia ndani. Kwa uhakiki zaidi, akangoja mpaka amwone akishuka. Kweli akamwona. Baba yake alikuwa amerudi.
Read more
Punde gari lilipokamta breki, likiwa limetumia dakika nane tu kufika hapo, Wisconsin na Brian ...
Media Removed
Punde gari lilipokamta breki, likiwa limetumia dakika nane tu kufika hapo, Wisconsin na Brian wakawa wa kwanza kushuka, nyuma wakifuatiwa na Mama yao. Wakagonga mlango, ulipokawia kufunguliwa, Wisconsin akausukuma kwanguvu akitumia bega lake pana. Mlango ukafunguka wakazama ndani. . . Kutazama ... Punde gari lilipokamta breki, likiwa limetumia dakika nane tu kufika hapo, Wisconsin na Brian wakawa wa kwanza kushuka, nyuma wakifuatiwa na Mama yao. Wakagonga mlango, ulipokawia kufunguliwa, Wisconsin akausukuma kwanguvu akitumia bega lake pana. Mlango ukafunguka wakazama ndani.
.
.
Kutazama sebuleni hakukuwa na mtu, ila punde kidogo, Karen akatokea akiwa amefungia taulo lake jeupe kifuani. Mwili wake ulikuwa umejawa na maji na macho yake yakiwa yamebebeba mashaka. .
.
Mama Brian akatahamaki kumwona, akaita, “Karen!” na kisha akamkimbilia na kumjulia hali. Karen akasema yu sawa, hakukumbana na tatizo lolote. Ndipo Mama Brian na wenziwe wakaketi na kumweleza kwanini walikuwa wanahofia mpaka kukimbia kuja hapo.
.
.
“Kuwa makini sana,” Wisconsin akamhusia. “Huenda muuaji akakufuata na wewe pia.”
.
.
Karen, akiwa aliyejawa na woga na mkanganyiko, akatikisa kichwa chake kupokea taarifa hiyo. Akaenda ndani na kujivesha nguo kisha akawaomba wageni wake hao wa dharura wampeleke kazini kwani hana usafiri.
.
.
.
**
.
.
.
“Madam, tunaomba uegeshe upande wako wa kulia, huko kuna nafasi zaidi!” alisema mwanaume aliyevalia sare ya suti nyeusi na mikononi mwake akiwa amevalia glovu nyeupe. Alikuwa hapa maalum kwa ajili ya kazi ya kuwalekeza wageni, aidha wenye vyombo vya usafiri ama lah, waliofika hapa kwenye mazishi. .
.
“Nashukuru.” Mama Brian akakunja kona kufuata maelekezo. Alipoegesha gari na kulizima, wakashuka na kuelekea kwenye viti kadhaa ambavyo viliwekwa kwenye uwanja wa makaburi. Wakaketi na kuchambua eneo. .
.
Hapo kulikuwa na watu takribani thelathini na tatu na magari kumi. Jeneza la Brewster lilikuwa limeshawekwa karibu kabisa na shimo lake na mbele kabisa, kwenye mpangilio wa viti, walikuwa wameketi watu wa karibu wa Brewster, haswa wafanyakazi wenziwe kwani hakuwa na marafiki.
.
.
Miongoni mwao, Padri Alfonso na watumishi wawili wa kike waliovalia sare zao kama ilivyo ada wakati wowote.
Read more
Na zaidi alipokuwa anamsogelea ndiyo akahisi kabisa anaelekea kufa. Kama angeliweza kupotea ...
Media Removed
Na zaidi alipokuwa anamsogelea ndiyo akahisi kabisa anaelekea kufa. Kama angeliweza kupotea kimazingara hapo, basi angelishapotea. . . Baba akamdaka koo. Akamtazama kwa macho yanayoogofya akisema, "Umeenda mbali ya mipaka, Wayde. Sina budi kukumaliza!" Akamminya koo kwanguvu, ... Na zaidi alipokuwa anamsogelea ndiyo akahisi kabisa anaelekea kufa. Kama angeliweza kupotea kimazingara hapo, basi angelishapotea.
.
.
Baba akamdaka koo. Akamtazama kwa macho yanayoogofya akisema, "Umeenda mbali ya mipaka, Wayde. Sina budi kukumaliza!" Akamminya koo kwanguvu, Wayde akiwa anapapatika,  akapapasa meza aloegemea, mara mkono wake wa kuume ukadaka 'vase' nzito rangi ya zambarau. .
.
Hakujiuliza mara mbili akampachika nayo baba yake kichwani, paah!! Baba akalalamika akimimina damu. Akatazama kiganja chake, kilikuwa kimelowa damu. Akamtazama Wayde kwa hasira pomoni, ila hakukaa vema, akabamizwa tena na vase ya pili. Sasa akawa mlegevu, mtepetevu, akadondoka chini na kutulia tuli.
.
.
Wayde akashika mdomo wake na kukodoa macho. "Mungu wangu, nimefanya nini hiki?" Alihisi ameua. Aliinama na kumgeuza baba yake, kisha akaweka mkono wake kifuani kuhisi mapigo ya moyo. Alipohisi yapo sawa, angalau akahema.
.
.
"Ahsante, Mungu!" .
.
Baba alikuwa anahema kwa mbali. Kichwa chake kilikuwa kinavuja damu taratibu toka kwenye majeraha. Macho yake hakuwa ameyafumba, bali yanayorembua. Alikuwa anamtazama Wayde akimwona kwa mbali, akimwona kimaruweruwe.
.
.
Mwili wake haukuwa na nguvu ya kupambana tena. Kichwa kilikuwa kinamgonga akijihisi mzigo.
.
.
"Samahani, baba. Inabidi nifanye hivi kwa ajili ya Boston!"
.
.
Jicho la kulia la baba yake likadondosha chozi. Akamfuta kwa kiganja chake na kisha akakiendea kile kioo kinachotunza wafu. Kabla hajaanza kunena, akamtazama baba yake alafu akanong'ona, "Samahani, baba."
.
.
.
**
.
.
.
Saa kumi na mbili na robo ...
.
.
Wisconsin alitazama saa yake ya mkononi alafu akaminya lips zake. Brian akamtazama na kumuuliza, "ni muda mrefu, sio?" Wisconsin akashusha pumzi ndefu na kusema, "kutakuwa kuna kitu, si bure. Si zoezi la kuchukua muda wote huo!"
Read more
Akiwa amebakiza hatua moja kumkabili mtu wake, Wayde akamrukia na kumganda mgongoni. Kabla hajamwondoa ...
Media Removed
Akiwa amebakiza hatua moja kumkabili mtu wake, Wayde akamrukia na kumganda mgongoni. Kabla hajamwondoa binti huyo, akastaajabu akichomwa na vioo usoni, tena mara nyingi asizoweza kuhesabu. Kumbe Wayde alikuwa ameteka baadhi ya vipande vya runinga. Na japo naye vilikuwa vinamkata ... Akiwa amebakiza hatua moja kumkabili mtu wake, Wayde akamrukia na kumganda mgongoni. Kabla hajamwondoa binti huyo, akastaajabu akichomwa na vioo usoni, tena mara nyingi asizoweza kuhesabu. Kumbe Wayde alikuwa ameteka baadhi ya vipande vya runinga. Na japo naye vilikuwa vinamkata kiganjani, hakuwa anajali!
.
.
Alimtofoatofoa yule dubwana na kumfanya alalamike kwa kunguruma. Macho yake ambayo hayakuwa yanaonekana, yakavuja damu akihangaika huku na kule kumtoa Wayde mgongoni. Mithili ya chombo kilichokumbwa na dhoruba, akawa anapepesuka, anajigonga na kutaka kuanguka.
.
.
Alipofanikiwa kumtia Wayde mkononi, akamvuta kwanguvu kisha akamminya shingo yake akitaka kumvunja na kummaliza moja kwa moja, ila hakuwa na nguvu hizo tena. Sasa alijihisi mdhaifu kuliko hata mara ya kwanza. Magoti yalishindwa kumbeba kabisa akaangukia chini kama mtu anayesujudu.
.
.
Mikono yake ikamwachia Wayde, ambaye naye alidondoka akiwa amechoka, amejeruhiwa. Haraka Wisconsin akaenda kumjulia hali binti huyo, na asipoteze muda, akamwagiza aweke presha kwenye jeraha la Brian ingali yeye akienda kutafuta huduma ya kwanza.
.
.
Kidogo akarejea akiwa na mkoba wa huduma hiyo, akatoa bandeji na dawa, upesi akamtia dawa Brian na kumfunga kisha akamwendea Mama. "Upo sawa?"
.
.
Mama akatikisa kichwa kuafiki. Wisconsin akamnyanyua ampeleke kumlaza kochini, lakini kabla hajasonga, akamwona dubwana lile likiwa limeamka! Tayari alishakusanya nguvu zake kama hapo awali!
.
.
"Mungu wangu!" Mama Brian akanong'ona. Upesi Wisconsin akapaza sauti, "Wayde, zima mshumaa!" Haraka Wayde akapuliza mshumaa na kuzimika.
.
.
Kidogo Wisconsin, akauwasha tena, na mara hii ulipowaka, mlangoni wakawa wamesimama watu watatu! Kutokana na mwanga hafifu, hawakuwa wanaonekana vema ila Wisconsim aliwatambua. Ni wale watoto wafu wa Helo.
.
.
Basi akasema maneno ya ajabu, na mara wale wafu wakamvamia dubwana yule na kumteketeza wakihodhi haki yao kama watoto wa Hernandez Lorenzo. Haki ambayo watoto hawa wa kuasili; Alfonso, Brewster na Olivia waliiteka kwa muda!
.
.
**
Read more
“ … Tulienda kumtafuta mtaalamu wa mambo ya majini, ila hakuwapo. Inaonyesha ni mtu wa ratiba nyingi. ...
Media Removed
“ … Tulienda kumtafuta mtaalamu wa mambo ya majini, ila hakuwapo. Inaonyesha ni mtu wa ratiba nyingi. Tungempata pengine angesaidia.” . . Mama alipomaliza kusema hayo, Brian akaendelea kula. Hakuona kipya. Alikuwa anatafuna lakini asihisi ladha ya chakula. Mawazo yake hayakuwapo ... “ … Tulienda kumtafuta mtaalamu wa mambo ya majini, ila hakuwapo. Inaonyesha ni mtu wa ratiba nyingi. Tungempata pengine angesaidia.”
.
.
Mama alipomaliza kusema hayo, Brian akaendelea kula.
Hakuona kipya. Alikuwa anatafuna lakini asihisi ladha ya chakula. Mawazo yake hayakuwapo hapo kabisa. Mama akamtazama na kisha akasafisha koo lake, Brian akampatia macho.
.
.
“ … kwahiyo tukaona itakuwa kheri endapo tungetafuta namna nyingine, hivyo tukaenda kanisani kumwona padri aje kutusaidia kwa maombi.”
.
.
“Padri Alfonso?” Olivia akauliza kwa macho yalojawa woga. Mrs Garett akamtazama na kumtikisia kichwa kuafiki. Olivia akakunja uso wake na kulalama. “Simtaki padri Alfonso!” akarudia tena, “Simtaki padri Alfonso!” alafu akaangua kilio.
.
.
“Usijali, Olivia,” akasema Mrs Garett. “Kila kitu kitakuwa sawa!” akambeba binti huyo na kumweka mapajani mwake akimbembeleza. Brian hakutia neno, akaishia kutazama tu. Na alipomaliza kula, akaenda zake chumbani. .
.
Alipojilaza, akatazama zile nyaraka tatu alizoachiwa na Dkt
Hamill. Akainyaka ile ambayo alishaanza kuisoma. Akatafuta eneo alipoishia na kuendelea kuipitia taratibu …
.
.
“ … Jasmine kabla hajanieleza kule alienda kufuata nini, akatikisa kwanza kichwa chake,” Dkt Hamill aliendelea kuhadithia kwenye nyaraka. “ … alifuma mafundo matatu alafu akaniambia kama unataka kujua basi kesho tuongozane kwenda huko. Nilihofia. Japo nilikuwa nataka kujua nini kipo kule, bado nilikuwa na hofu kifuani mwangu. Basi hapo akawa amenikata hamu, na pasipo kuaga nikajiendea.
.
.
Kesho yake nikamfuatilia, hakwenda kule msituni. Wala keshokutwa, wala mtondogoo. Ila siku iliyofuata, majira ya jioni, akapotea nyumbani. Nilimtafuta kila kona pasipo mafanikio basi nikajua ya kuwa atakuwa ameenda kule msituni.
.
Read more
Hewa inakuwa nzito sana. Hata harufu nayo pia inabadilika na kumfanya Brian apige chafya na kukurupuka. ...
Media Removed
Hewa inakuwa nzito sana. Hata harufu nayo pia inabadilika na kumfanya Brian apige chafya na kukurupuka. Hakuwa kwenye mazingira anayoyajua. Hapa chumba kilikuwa ni chembamba na kuta zake zilikuwa hafifu, kukuu. . . Mwanga ulikuwa hafifu sana. Mwanga ulioshindwa kupambana na giza. ... Hewa inakuwa nzito sana. Hata harufu nayo pia inabadilika na kumfanya Brian apige chafya na kukurupuka. Hakuwa kwenye mazingira anayoyajua. Hapa chumba kilikuwa ni chembamba na kuta zake zilikuwa hafifu, kukuu.
.
.
Mwanga ulikuwa hafifu sana. Mwanga ulioshindwa kupambana na giza.
Brian akatazama kushoto na kulia. Hakumwona mtu. Alikuwa anatamani kunyanyuka, lakini mwili haukuwa na nguvu kabisa. Ni shingo tu ndiyo ilikuwa na uwezo wa kupeleka kichwa huku na kule.
.
.
Punde mlango ukafunguliwa, Brian akatazama huko. Akamwona Kecie na gauni lake. Mkononi alikuwa na mdoli. Binti huyo akamsogelea karibu na kumtazama machoni.
.
.
“Brian, naomba niokoe,” akasema kwa sauti ya upole.
.
.
“Nikuokoe na nini, Kecie?” Brian akauliza.
.
.
“Mimi ni mfungwa, Brian,” Kecie akasema. Mkono wake wa baridi ukamshika Brian. “Nipo kifungoni, nataka kutoka roho yangu iende kwa amani.”
.
.
“Nani amekufunga, Kecie?” Brian akauliza. Kecie akatazama mlangoni na kupanyooshea kidole pasipo kusema kitu. Ajabu, Brian akapata nguvu ya kunyanyuka. Akatoka kitandani na kuuendea mlango, akaufungua na kutazama nje.
.
.
Kulikuwa na korido ndefu sana. Sakafu yake haikuwa inaonekana kwani imetwaliwa na moshi. Kutani kulikuwa na fremu za picha na kwa mbali kulikuwa kunasikika sauti nzito ya mwanaume ikinena na hata kucheka.
.
.
** **
.
.
.
LAKO JICHO!
Read more
“Unahisi nini, Wayde?” Brian akauliza akimtazama mlengwa. Mara Wayde akasimama na kumwambia, ...
Media Removed
“Unahisi nini, Wayde?” Brian akauliza akimtazama mlengwa. Mara Wayde akasimama na kumwambia, “Twende!” . . Wakatoka nje ya darasa kwenda kulikuta gari la Wayde, wakajipaki na msichana huyo kutimka. Brian hakuwa anajua wapi wanaelekea, pia alikuwa na hofu ya kukutwa na baba yake Wayde ... “Unahisi nini, Wayde?” Brian akauliza akimtazama mlengwa. Mara Wayde akasimama na kumwambia, “Twende!”
.
.
Wakatoka nje ya darasa kwenda kulikuta gari la Wayde, wakajipaki na msichana huyo kutimka. Brian hakuwa anajua wapi wanaelekea, pia alikuwa na hofu ya kukutwa na baba yake Wayde ambaye ashampiga marufuku ya kuonana na binti yake.
.
.
“Wayde, naona hili litakuwa na hatari kwangu.”
.
.
“Usijali, baba yangu hayupo,” Wayde akamtoa hofu. Wakaenda na usafiri huo mpaka nyumbani kwa wakina Wayde, nyumba kubwa ya ghorofa mbili. Sakafu ya chini ilikuwa ni ya watoto, ya pili ya wazazi na ile ya tatu ikikaliwa na maktaba.
.
.
Wayde akampandisha Brian mpaka juu kabisa kwenye maktaba kisha akamwambia, “Keti hapa.” alafu yeye akarudi chini na muda si mrefu akarejea na funguo, akamwambia Brian, “Nifuate huku.”
.
.
Wakaendea chumba fulani ndani ya maktaba. “Chumba hiki ni siri kukiingia. Baba yangu amekuwa akizama humu mara kadhaa tu na kujifungia. Pale nilipopata muda wa kusoma baadhi ya vitabu ambavyo vipo katika maktaba nikaja gundua kuwa upotevu wa watoto ndani ya mji wa Boston ni kitu ambacho kilitarajiwa kwa maana ni adhabu anayotupatia bwana Helo.”
.
.
Wayde aliposema hayo, akamtazama Brian na kumuuliza, “Ninachokisema ni uongo?”
.
.
Brian akatikisa kichwa. “La hasha.”
.
.
“Lakini kwanini hukunambia Brian?” Wayde akauliza. “Ulikuwa unayajua yote hayo, sio?” Brian hakusema jambo. “Ulikuwa unayajua yote hayo na ukaamua kunificha, kwanini Brian?”
.
.
Wayde akafungua chumba wakazama ndani, humo kulikuwa na vitabu vingine vya ziada tofauti na vile ambavyo vipo kwenye ukumbi mwingine. Akampatia Brian baadhi ya vitabu na barua kadhaa takribani sita, kisha akamwambia, “visome, nawe uniambie ni nini umeona, Brian.”
.
.
Brian akachukua muda kuvipitia. Macho yake yalikuwa mepesi kwakuwa alikuwa mzoefu wa kupenda kusoma. Baada ya muda wa dakika arobaini na tano tu, akawa amaemaliza. Akamuuliza Wayde, “Ina maana baba yako ana mahusiano na seneta yule aliyemuua na kumchoma Helo?”
Read more
ILIPOISHIA . . Akasonga hatua taratibutaratibu akisogelea hicho chumba. Alipofunga mlangoni, ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . Akasonga hatua taratibutaratibu akisogelea hicho chumba. Alipofunga mlangoni, akarusha macho yake ndani. Kama macho yake yalikuwa sahihi, alimwona Olivia akiwa kandokando ya kitanda. Mkononi mwake alikuwa ameshikilia kisu kirefu. . . Akajikuta akisema, “Olivia!” ... ILIPOISHIA
.
.
Akasonga hatua taratibutaratibu akisogelea hicho chumba. Alipofunga mlangoni, akarusha macho yake ndani. Kama macho yake yalikuwa sahihi, alimwona Olivia akiwa kandokando ya kitanda. Mkononi mwake alikuwa ameshikilia kisu kirefu.
.
.
Akajikuta akisema, “Olivia!” kwa kunong’oneza. Hamaki, Olivia akageuka na kumtazama. Macho yake yalikuwa yanang’aa kana kwamba taa.
.
.
ENDELEA
.
.
Brian hajakaa sawa, Olivia akakimbia upesi na kumvamia mpaka chini. Binti huyo akawa anataka kumchoma kisu. Brian akapambana kwa kuudaka mkono wenye kisu akitumia nguvu zote asijeruhiwe. .
.
Ajabu Olivia alikuwa ni mwenye nguvu sana, hata Brian hakuwa anaweza kufua dafu, ncha ya kisu ilikuwa inajongea taratibu kufuata kifua chake. Aling’ata meno akikazana kujitetea, alipoona juhudi zake zinaelekea ukingoni na huku akiwa anashindwa, akajikakamua kwa mwili wake wote kumtupia Olivia kando amweke chini, kisha akadaka mkono wa Olivia wenye kisu, akaubondea ukutani kwanguvu mara tatu , kisu kikadondoka chini!
.
.
“Nitakuua, Brian!” Olivia akang’aka. Sauti yake ilikuwa inatetemeka kana kwamba inatoka kwenye ‘tape recorder’. Macho yake yalikuwa mekundu na mdomo wake umekauka kuwa mweusi.
.
.
“Olivia, nini kimekutokea?” Brian akauliza. Alimtazama Olivia kwa huruma na mshangao. Katika namna ya ajabu akaanza kudhoofu. Kadiri alivyotazama macho ya Olivia akawa anajihisi kupoteza nguvu mwilini. Mwishowe Olivia akamtupia pembeni na kuteka tena kisu, akamfuata.
.
.
“Acha Olivia!” Brian akasihi. “Usifanye hivyo tafadhali!” .
.
Olivia hakusikia, akaendelea kutembaa kumfuata. Brian akiwa chini, akawa anajivuta kusonga mbali na Olivia.
.
.
“Tafadhali, Olivia! Wewe ni msichana mzuri, usifanye hivyo,” Brian akaendelea kunena. Olivia asijali, akamsongea na kisha akainama kutaka kumchoma kisu Brian. Alikuwa na nguvu maradufu. Na ubaya ni kwamba Brian alikuwa anaishiwa na nguvu mwilini kila alipomtazama Olivia machoni.
Read more
Haraka Brian akafungua mlango na kutazama nje kwa tahadhari ya gongo lake. Alitazama kushoto na ...
Media Removed
Haraka Brian akafungua mlango na kutazama nje kwa tahadhari ya gongo lake. Alitazama kushoto na kulia. Mikono yake yote ilikuwa imeshikilia gongo lake kwanguvu. Hakuona kitu. Akiwa anasonga kuelekea kwenye milango ile miwili ambayo ipo wazi, akawa anatupa macho yake aliyoyakodoa. . . Kumbe ... Haraka Brian akafungua mlango na kutazama nje kwa tahadhari ya gongo lake. Alitazama kushoto na kulia. Mikono yake yote ilikuwa imeshikilia gongo lake kwanguvu. Hakuona kitu. Akiwa anasonga kuelekea kwenye milango ile miwili ambayo ipo wazi, akawa anatupa macho yake aliyoyakodoa.
.
.
Kumbe Olivia alikuwa darini. Alikuwa amejishikiza katika namna ya ajabu akimtazama Brian anayetembea kwa hatua za pole. Brian aliposonga akiwa amebakiza hatua chache kuufikia mlango wa Karen, Olivia akaanguka toka darini na kumvamia, akamdondosha chini!
.
.
Akamchoma Brian kisu cha ubavuni. Brian akapiga kelele kali za maumivu. Akatupa kiwiko chake kwanguvu kikamkita Olivia usoni, Olivia akadondokea kando. Brian akajivuta mbali na Olivia kisha akatazama jeraha lake. Lilikuwa linamwaga damu. Alikuwa anasikia maumivu makali sana. .
.
Olivia akalamba damu kwenye kisu kisha akatabasamu na kusema kwa sauti yake ya ajabu, “ni tamu mno, Brian. Nataka tena!” akanyanyuka na kuanza kumfuata Brian kwa kasi. Akaruka juu akitaka kumkita, upesi Brian akamzaba kichwa kwa gongo lake. Alimzaba kwanguvu mno mpaka damu kuruka. Olivia akatupiwa ukutani na kudondoka chini akiwa amelala kifudifudi, akatulia tuli.
.
.
Brian akamtazama kwa mashaka. Akanyanyuka akiwa ameuweka mkono wake wa kushoto kwenye jeraha kuzuia damu zisitoke zaidi. Akahema akimtazama kile kiumbe. Amekufa ama amezirai? Akajiuliza.
.
.
Kidogo, akasikia sauti ya Olivia akigugumia, mara akaanza kulia. Alikuwa akilia akivuta makamasi na kubanwa na kwikwi. Sauti yake ya kulia ilikuwa ndogo ila kwakuwa usiku sauti husafiri kiwepesi, Brian aliisikia vema.
.
.
Olivia akalia kwa takribani sekunde tano kisha sauti yake iliyobanwa na kilio ikauliza, “Nimekukosea nini Brian kuniadhibu kiasi hiki?” Mara hii sauti ilikuwa ni ya Olivia tunayemjua. Sauti ndogo ya kike ya msichana asiye na makosa. Sauti inayotia huruma.
Read more
“Kamwe!” Akasema Olivia akipeperusha kidole chake kushoto na kulia. “Kamwe … kamwe … usije kuthubutu!” . . Aliposema ...
Media Removed
“Kamwe!” Akasema Olivia akipeperusha kidole chake kushoto na kulia. “Kamwe … kamwe … usije kuthubutu!” . . Aliposema hayo akakunja ngumi ya mkono wake wa kuume, Brian akaanza kukabwa na mkono asiouona. Akadaka shingo yake akijitahidi kuhema. Mishipa ya shingo imemshupaa. Olivia ... “Kamwe!” Akasema Olivia akipeperusha kidole chake kushoto na kulia. “Kamwe … kamwe … usije kuthubutu!”
.
.
Aliposema hayo akakunja ngumi ya mkono wake wa kuume, Brian akaanza kukabwa na mkono asiouona. Akadaka shingo yake akijitahidi kuhema. Mishipa ya shingo imemshupaa. Olivia akaendelea kuiminya ngumi yake. Brian akaendelea kuteseka maradufu, sasa hewa akiwa hapati! Jasho jingi lamchuruza. Macho yamemtoka nje! Alikuwa anaelekea kufa.
.
.
Uso wake ulibadili rangi kuwa mwekundu, na kila mshipa uliokuwapo kichwani ukasimama dede! Kwa sekunde tatu tu za mbele, kijana huyu alikuwa anaiacha dunia. .
.
Kheri, huko nje sauti za watu zikajongea. Walikuwa ni watu wawili wanaongea na huku wakiwa mwendoni kufuata makazi ya wakina Brian. Hapa ghafla, Olivia akanyong’onyea na kudondoka chini akiwa hana fahamu! Hiyo ikawa ahueni ya Brian ya maisha yake yaliyokuwa yamebakia kwenye nyuzi nyembamba!
.
.
Punde mlango ukafunguliwa, akaingia Mama yake Brian pamoja na Mrs Garett. .
.
“Mungu wangu!” Wakahamaki. Brian alikuwa ameegemea ukuta, yu hoi, na kwake pumzi ikiwa ni bidhaa yenye thamani kubwa akihangaika kuitafuta. Hata nguvu hakuwa nayo. Jasho limemvaa uso wake gubigubi. Anakohoa kwa pupa.
.
.
Olivia alikuwa hayupo hata kwenye ulimwengu huu. .
.
“Brian, nini kimetokea?” Mama Brian akauliza akimkimbilia mwanaye upesi kumtazama. Mrs Garett naye akamsongea Olivia na kumpekua. “Amezirai!” akasema kwa mshangao. Baada ya muda kidogo, wakawa wamemweka Olivia juu ya kiti, na Brian naye amepumzishwa papo.
.
.
Nyuso za wanawake hawa zilikuwa na taharuki na hofu juu. Walikuwa na kiu kikubwa cha kufahamu nini kilichojiri.
.
.
Baada ya muda wa takribani dakika sita, Brian, akiwa ametulia na kurudi kwenye hali yake mbali na maumivu aliyokuwa anayahisi kwa mbali shingoni, akaelezea namna ambavyo mambo yalitokea. Habari hizo zikawashtua sana Mrs Garett na mama yake.
.
Read more
Akatabasamu na kuendelea na kazi yake ya kufuma nguo. Nikadhani labda atakuwa aliniona nilivyokuwa ...
Media Removed
Akatabasamu na kuendelea na kazi yake ya kufuma nguo. Nikadhani labda atakuwa aliniona nilivyokuwa namfuatilia, basi nikaona niwe mpole, nikamuuliza kule alikuwa ameenda kufanya nini?…” . . Hapa ndipo Brian alikuwa ameishia kusoma kabla hajasikia kelele kali zilizomshtua. Alidhani ... Akatabasamu na kuendelea na kazi yake ya kufuma nguo. Nikadhani labda atakuwa aliniona nilivyokuwa namfuatilia, basi nikaona niwe mpole, nikamuuliza kule alikuwa ameenda kufanya nini?…”
.
.
Hapa ndipo Brian alikuwa ameishia kusoma kabla hajasikia kelele kali zilizomshtua. Alidhani pengine ni masikio yake, ila alipotulia vema akasikia sauti zingine. Hapo akaamini kuwa ni uhalisia! Kelele zote hizo usiku za nini?
.
.
Haraka akafungua mlango na kutoka nje. Akaenda chumbani kwa mama yake alipomkuta Mrs Garett akipiga makelele na mama yake akiwa anamtuliza. Akauliza nini kimejiri.
.
.
“Mrs Garett amemwona Kecie bafuni!” Mamaye akamjibu. Uso wake ulikuwa umeelemewa na usingizi, mshangao na woga.
.
.
“Yu kwapi Olivia?” Brian akauliza. .
.
“Chumbani huko!” mama yake akajibu. Kwa haraka Brian akapata wazo la kwenda kumwona binti huyo. Alifungua mlango pasipo hata kubisha hodi, akatupa macho yake kitandani. .
.
Olivia hakuwapo!
.
.
Akatafuta kwenye kabati, chini ya kitanda na nyuma ya mlango. Olivia hakuwapo! Haraka akarudi kule kwenye chumba cha mama na kuwaambia kuwa Olivia hayupo! Wakamtafuta nyumba nzima, kweli hakuwapo.
.
.
Wakiwa sebuleni, kwa mbali huko nje, Brian akamwona binti akiishilia na barabara! Akapayuka, “Yule kule!” haraka akafungua mlango na kumkimbilia binti huyo.
.
.
“Olivia! … Olivia!” alimwita lakini Olivia hakuitikia. Aliendelea kutembea akitazama mbele. Brian akamfikia na kumnyanyua juu, akamwita, “Olivia! Olivia!” akiwa anampigapiga makofi shavuni kumwamsha.
.
.
Macho ya Olivia yalikuwa yanatazama kule mbele alipokuwa anaenda. Kuna kitu alikuwa anaona. Akakinyooshea kidole. Lakini Brian alipotazama hakuona jambo. .
.
“Kuna nini Olivia?”
.
.
Olivia hakuwa mtu anayejielewa. Bado macho yake yalikuwa yanaangazia kule mbele. Hakuonekana kama anasikia hata kile anachoambiwa. .
.
Baada ya muda fulani ndipo akamtazama Brian. Macho yake yalikuwa yanatisha. Na Brian asifahamu kinachoendelea, akajikuta anadondoka chini na kupoteza fahamu!
Read more
ILIPOISHIA . . Kulikuwa na korido ndefu sana. Sakafu yake haikuwa inaonekana kwani imetwaliwa ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . Kulikuwa na korido ndefu sana. Sakafu yake haikuwa inaonekana kwani imetwaliwa na moshi. Kutani kulikuwa na fremu za picha na kwa mbali kulikuwa kunasikika sauti nzito ya mwanaume ikinena na hata kucheka. . . ENDELEA . . Brian akapata shaka na walakini. Akatazama ... ILIPOISHIA
.
.
Kulikuwa na korido ndefu sana. Sakafu yake haikuwa inaonekana kwani imetwaliwa na moshi. Kutani kulikuwa na fremu za picha na kwa mbali kulikuwa kunasikika sauti nzito ya mwanaume ikinena na hata kucheka.
.
.
ENDELEA
.
.
Brian akapata shaka na walakini. Akatazama nyuma kumwangalia Kecie, Kecie akamnyooshea kidole huko huko mbele. Lakini Brian hakuwa anajua cha kufanya. Alinyanyua miguu yake kwenda mbele akiwa hafahamu anaenda kukutana na nani.
.
.
Sakafu ilikuwa ya baridi kupita kiasi. Ilimfanya atetemeke na akunjekunje vidole vyake kila alipokuwa anakanyaga. Kwenye kuta, zile picha zilizokuwa zimetundikwa, zikawa zinanyamaza na kumtazama Brian alipokuwa anapita.
.
.
Picha hizo zilikuwa ni za sherehe. Zilikuwa ni za vifijo cha kipindi kile ambapo Helo alikuwa anatumbuiza. Bado picha hizo zilikuwa hai. Watu walikuwa wanafurahia na kushangilia mazingaombwe ya Helo, lakini Brian akitazama zilikuwa zinaganda na kuwa picha kamili!
.
.
Brian akazitazama akisonga. Moyo wake ulikuwa unapiga kusema hofu iliyomtawala. Kadiri alivyokuwa anasonga kwenda mbele, ndivyo sauti ile aliyokuwa anaisikia kwa mbali ikawa inamjongea na hata kuleta maana.
.
.
Kuna muda ilikuwa ni wimbo waimba. Na kuna muda kulikuwa na sauti ya mwanaume ikifoka ama kuteta. Mwanaume huyo ni nani? Na wimbo huo - ngoja! Atakuwa ni Helo. Brian alikuwa na kikao kichwani mwake. Na huyo anayemfokea ni nani? .
.
Hakukuwa na majibu zaidi ya yeye kusonga na kutazama kwa macho yake. Japo alikabwa na woga, hakika alitaka kujua. Alipofika kwenye mwisho wa korido, taratibu, akachomoza kichwa chake kuchungulia sebuleni.
.
.
Kwa macho yake akamwona mwanaume fulani mzito aliyekuwa amevalia kofia ndefu kichwani yenye michirizi mekundu kwenye kingo zake. Mwanaume huyo alikuwa amevalia nguo za sherehe, zinazometa na kuvutia.
Read more
Brian alikuwa makini akisikiliza, macho yake mekundu yalikuwa tenge na kwa muda mfupi, usingizi ...
Media Removed
Brian alikuwa makini akisikiliza, macho yake mekundu yalikuwa tenge na kwa muda mfupi, usingizi ulimtoweka kichwani japo kichwa chake bado kilimgonga kwa mbali. . . “… swali lake la kwanza kuniuliza ni wapi alipo mtoto wako? Nikamwambia sifahamu, ametoka muda mrefu. Akaniambia ulipo ... Brian alikuwa makini akisikiliza, macho yake mekundu yalikuwa tenge na kwa muda mfupi, usingizi ulimtoweka kichwani japo kichwa chake bado kilimgonga kwa mbali.
.
.
“… swali lake la kwanza kuniuliza ni wapi alipo mtoto wako? Nikamwambia sifahamu, ametoka muda mrefu. Akaniambia ulipo na mwishowe akanipa onyo pasipo kunielezea mambo mengi. Kama nataka uwe hai, basi nikusihi uache mambo unayoyafanya na uishi maisha yako.”
.
.
“Kwanini alisema hivyo?” Brian akauliza.
.
.
“Sijui!” Mama akajibu. “Hakunieleza mambo mambo mengi zaidi ya hayo, na hakukaa muda mrefu akaenda zake … sikufahamu alijuaje ulipo, na sijui ana nini kichwani kuhusu wewe.”
.
.
“Alikueleza nitakuwa naota na kuona mambo ya ajabu?” .
.
“Alichoniambia ni kwamba, endapo usipofuata anachokisema basi maisha yako yatakuwa ya taabu sana. Utaishi kwa masumbuko, hofu na woga … Brian, sijui kama anachokisema ni kweli au lah! Ila nahisi kuna kitu hakipo sawa. Naomba uachane na mambo ya Kecie. Sawa?”
.
.
Brian akatazama chini. Hakujibu, ikabidi mama yake arudie kuuliza. .
.
“Sawa, Brian?”
.
.
“Sawa, mama … nitafanya hivyo.”
.
.
“Nenda kapumzike sasa. Najua usiku haukulala.”
.
.
Brian akanyanyuka na kwenda zake chumbani. Kulikuwa na mambo kadhaa yanampitia kichwani ila alipojitupia kitandani hakupata wasaa wa kuyafikiria, usingizi ulimnyaka na kumpoteza. .
.
.
***
.
.
.
.
Saa kumi jioni …
.
.
.
“Oliviiia!” Sauti ya Mrs Garett ilitikisa nyumba. Alikuwa amekunja sura, ametoka chumbani anaelekea sebuleni akiwa ameweka mkono wake kiunoni. .
.
.
Akaendelea kuita na kuita, hakusikia wala kuona kitu. Alikasirika sana, akaketi kitini akiwaza Olivia atakuwa wapi. Alimkataza asiende kucheza pasipo kumwomba ruhusa. Alimkataza kwenda popote pale. Ina maana amekaidi agizo lake.
Read more
** . . . Saa moja jioni … . . . Brian alikuwa amejifungia chumbani kwake, uso wake ukiwa mwekundu, ...
Media Removed
** . . . Saa moja jioni … . . . Brian alikuwa amejifungia chumbani kwake, uso wake ukiwa mwekundu, macho yake bado yanachuruza machozi. Kitandani kulikuwa kuna zile nyaraka tatu ambazo Dkt Hamill alimwambia akazichukue, pamoja pia na ujumbe aliopewa na Dokta kule hospitalini. . . Alitazama ... **
.
.
.
Saa moja jioni …
.
.
.
Brian alikuwa amejifungia chumbani kwake, uso wake ukiwa mwekundu, macho yake bado yanachuruza machozi. Kitandani kulikuwa kuna zile nyaraka tatu ambazo Dkt Hamill alimwambia akazichukue, pamoja pia na ujumbe aliopewa na Dokta kule hospitalini.
.
.
Alitazama nyaraka zile na ule ujumbe. Sijui alikuwa anawaza nini kichwani mwake. Kwa muda kidogo hakuwa anajua cha kufanya ilhali kila kitu kipo bayana ya kwamba yampasa atazame vilivyomo ndani.
.
.
Baada ya kutulia kidogo ndipo akachukua ule ujumbe kwenye karatasi, akaanza kuusoma. Uso wake ulikuwa umepooza. Macho yake yalikuwa yanatia huruma. .
.
Taratibu akawa anapitisha macho kwenye ujumbe uliokuwa unasomeka kama ifuatavyo,
.
.
“Inabidi niende, Brian. Sidhani kama nitakuwa nimekuacha mpweke. Nimeenda kwenye ulimwengu wa pili. Ulimwengu ambao siujui moja wala kumi yake. Nimekamilisha maisha yangu huku duniani. Lakini nakusisitizia Brian, mimi nimekwenda. Ni hivyo tu. Endapo ukiniona tena muda wowote mahali popote, basi jua si mimi.
.
.
Kwenye hizo nyaraka tatu, tafuta muda usome kwa makini. Tafadhali usipuuze. Nakutakia kila la kheri ukatimize haja yako. Usiogope, Brian. Na usiache jitihada zako za kumwokoa Kecie. Huwezi jua utawaokoa na wakina nani pamoja naye.”
.
.
Ujumbe ulikwisha ukimwacha Brian akidondosha machozi. Kichwa kilikuwa kinamgonga na alijikuta anaumia sana moyoni. Anaumia mno. Alisaga meno yake kwanguvu akiangushia kichwa chake kitandani. .
.
Hakukumbuka aliishia wapi kulia, usingizi ulimsomba kwa pupa sana kumpeleka kwenye ulimwengu wa kiza ila angalau wenye unafuu. .
Read more
Hali hii ikadumu kwa mwaka mmoja tu. Fedheha, lawama, dharau zikachosha familia hii. Walitaraji ...
Media Removed
Hali hii ikadumu kwa mwaka mmoja tu. Fedheha, lawama, dharau zikachosha familia hii. Walitaraji mambo yangekuwa sawa, lakini pengine ilionekana ingechukua muda mrefu kuwa vivyo. Sasa Helo na familia yake wakaanza kuonyesha kucha na rangi zao halisi. . . Wakaapia kuwavuta kwenye ... Hali hii ikadumu kwa mwaka mmoja tu. Fedheha, lawama, dharau zikachosha familia hii. Walitaraji mambo yangekuwa sawa, lakini pengine ilionekana ingechukua muda mrefu kuwa vivyo. Sasa Helo na familia yake wakaanza kuonyesha kucha na rangi zao halisi.
.
.
Wakaapia kuwavuta kwenye fedheha na aibu wale wote waliokuwa wanawataka wao waishi kwenye shimo hilo. Basi mmoja mmoja akawa anakufa kila uchwao. Hali hii ikatisha sana Boston na hata Massachusetts nzima. Walipokuja kugundua ni Halo na familia yake wafanya vivyo, wakachoma nyumba yao. Wakawakamata na kuwachoma moto mbele ya hadhira.
.
.
Huo ukawa mwisho wa Halo na familia yake. Nyumba yake, iliyokuwa imebakia kuwa ghofu, ikatengwa na hata mpaka sasa imebakia huko ndani ya misitu ikiwa pweke. .
.
Lakini kabla Helo hajafa, wakati moto wamuunguza kula mwili wake, alilia sana na kusema kuwa atarudi kulipiza kisasi. Alikuwa anaamini hakuwa na makosa, aliishi kwa upendo wote na wakazi wa Boston na Massachusetts nzima kabla ya wao kukengeuka.
.
.
Neno lake la mwisho alilitamka kwa kilatini akisema wote mtakuwa wangu. Wote mtasujudia miguuni mwangu. Majivu yake yalienda kutupwa huko msituni na toka siku hiyo mpaka leo hii Helo akageuka kuwa historia ya kuwasimulia watu. .
.
Ni wachache sana waliojali yale maneno yake aliyoyasema wakati anakufa. Ila Helo alisema ukweli. Atarudi tena kwenye mji huu na atafanya kila mtu awe wake.”
.
.
Brian alikuwa ameachama mdomo wake wazi akiskiza mpaka hapo mwisho. Alipoufumba akauliza, “Ina maana yale maneno maana yake ni ‘Helo, kuwa wangu!’ kwa kilatini?”
.
.
“Ndio,” akajibu Dokta, “Hiyo ndiyo maana yake, ndiyo maana nikashangazwa sana na mahali ulipoyatolea hayo maneno. Ebu niambie uliyasikia wapi? Kuwa mkweli, pengine naweza kukusadia.”
.
.
Dkt Hamill alimtazama Brian kwa macho ya kidadisi na hamu. Kabla Brian hajatia neno, akamuuliza, “Umeyasikia maneno hayo ndotoni au msituni?”
.
.
.
.
****
.
.
LAKO JICHO. Ukihitaji simulizi yote njoo whatsapp 0685 758 123. Ada 2,000 tu.
Read more
Basi Brian akashikwa na kigugumizi, akaita na kuuliza, “Olivia, ni wewe?” Olivia akaendelea kulia ...
Media Removed
Basi Brian akashikwa na kigugumizi, akaita na kuuliza, “Olivia, ni wewe?” Olivia akaendelea kulia asijibu. “Olivia, tafadhali niambie, ni wewe?” . . “Nimeumia sana, Brian!” Olivia akalalamika kwa sauti yake ya kike. “Siuhisi uso wangu kabisa. Wote umejawa damu.” . . “Nisamehe, ... Basi Brian akashikwa na kigugumizi, akaita na kuuliza, “Olivia, ni wewe?” Olivia akaendelea kulia asijibu. “Olivia, tafadhali niambie, ni wewe?”
.
.
“Nimeumia sana, Brian!” Olivia akalalamika kwa sauti yake ya kike. “Siuhisi uso wangu kabisa. Wote umejawa damu.”
.
.
“Nisamehe, Olivia,” Brian akasema akisonga. “Sikudhamiria kukuumiza, nilidhani ni mtu mwingine amekuingia.”
.
.
Olivia akaendelea kulia na kugugumia, akivuta makamasi na kuguna. .
.
“Nisamehe, Olivia,” Brian akaendelea kuomba akisonga karibu. Moyo wake ulikuwa wa baridi kwa majuto. Alipomkaribia Olivia, akainama na kumshika bega. Upesi Olivia akaamka na kumzaba Brian kofi kali, Brian akadondokea chini! Kabla hajaamka, Olivia akawa tayari amekaa juu yake, akacheka na kusema kwa sauti yake ya awali, sauti ya ajabu, “We ni mpumbavu, Brian!” kisha akanyanyua mkono wake wenye kisu kumkita, ila ghafla akaganda. Akatazama kushoto na kulia kwake akinusanusa. Mara akanyanyuka na kwenda zake chumbani mwa Brian. .
.
Brian akamtazama akiishilia humo. Macho yake yalikuwa hayaoni vizuri kwasababu ya kofi alilozabwa. Nacho kichwa kilikuwa kinamgonga haswa upande wa kulia alipoadhibiwa. .
.
Olivia alielekea mahali ambapo Brian alikuwa amerundika nguo zake. Hapo kwa chini kulikuwa kuna kaki ‘container’ kadogo ka chuma kalichondoka na kukaa wazi. Kumbe Brian wakati anachukua lile gongo lake, alidondosha kifaa hicho pasipo kujua.
.
.
Olivia akainama na kutwaa mkufu ule alafu akaubania kiganjani mwake na kusema, “Mama.”
.
.
.
.
*****
.
.
Lako jicho!
Read more
ILIPOISHIA . . Olivia alielekea mahali ambapo Brian alikuwa amerundika nguo zake. Hapo kwa ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . Olivia alielekea mahali ambapo Brian alikuwa amerundika nguo zake. Hapo kwa chini kulikuwa kuna kaki ‘container’ kadogo ka chuma kalichondoka na kukaa wazi. Kumbe Brian wakati anachukua lile gongo lake, alidondosha kifaa hicho pasipo kujua. . . Olivia akainama ... ILIPOISHIA
.
.
Olivia alielekea mahali ambapo Brian alikuwa amerundika nguo zake. Hapo kwa chini kulikuwa kuna kaki ‘container’ kadogo ka chuma kalichondoka na kukaa wazi. Kumbe Brian wakati anachukua lile gongo lake, alidondosha kifaa hicho pasipo kujua.
.
.
Olivia akainama na kutwaa mkufu ule alafu akaubania kiganjani mwake na kusema, “Mama.”
.
.
ENDELEA
.
.
Akaubusu mkufu ule na kisha akarejea kule koridoni. Hakumkuta Brian. Kugeuka nyuma, akapigwa kwanguvu na gongo, akadondoka chini akiwa amepoteza fahamu. Brian akatokea nyuma yake na kumtazama. Akampokonya kisu na kumgeuza akimkagua.
.
.
Akamwona mkononi akiwa na ule mkufu. Akauchukua na kuuweka ndani ya mfuko wake kisha akambeba na kumrejesha chumbani. Akamfunga kamba mikono na miguu kisha akamlaza kitandani. Alipomaliza, akaendea ‘first aid kit’ na kujipa huduma ya kwanza. Akajimiminia dawa ya kukata damu na kuua wadudu alafu akajifunga bandeji. .
.
Akarudi chumbani na kujaribu kumwamsha Wisconsin. Bwana huyo akaamka. Brian akamweleza yaliyotokea. Wisconsin akastaajabu. Alah! Yote yametokea akiwa amelala! Akaamka na kwenda kumtazama Olivia kisha akarejea kwa Brian.
.
.
“Utakuwa upo sawa kweli?” akamuuliza. .
.
“Ndio,” Brian akamtoa shaka. “Nipo sawa, asubuhi nitaenda hospitali.”
.
.
**
.
.
Asubuhi ya saa mbili, Brian akiwa kitandani mwa hospitali.
.
.
Mama aliongea kidogo na daktari kisha akaja kukutana na Brian. Akatabasamu na kusema, “Pole sana, mwanangu.” akamshika Brian nywele akitabasamu. .
.
“Daktari amesemaje?” Brian akauliza.
.
.
“Amesema tunaweza kwenda. Jeraha halijasababisha maafa makubwa. Kuna dawa za kutumia … na pia amehasa upumzike ili urudi upesi kwenye hali yako.”
.
.
Brian akaigiza kutabasamu alafu akauliza, “Wisconsin bado yupo?” Mama akatikisa kichwa. “Hapana, ametoka kidogo. Ila alisema atarejea muda si mrefu.”
Read more
Basi Mama akaongeza mwendokasi akielekezea chombo kule alipoambiwa, muda mchache, kama dakika ...
Media Removed
Basi Mama akaongeza mwendokasi akielekezea chombo kule alipoambiwa, muda mchache, kama dakika kumi na tatu, wakawa wamewasili. Wakashuka na kwenda ndani ya ofisi. Pale kwenye ofisi ya mapokezi wakamkuta mwanamke mwingine mwembamba sana mwenye nywele nyingi nyeusi. . . Wakamsalimu ... Basi Mama akaongeza mwendokasi akielekezea chombo kule alipoambiwa, muda mchache, kama dakika kumi na tatu, wakawa wamewasili. Wakashuka na kwenda ndani ya ofisi. Pale kwenye ofisi ya mapokezi wakamkuta mwanamke mwingine mwembamba sana mwenye nywele nyingi nyeusi.
.
.
Wakamsalimu na kumweleza shida yao, “Tumemkuta Karen?” Mama Brian akauliza pasipo kuonyesha shaka usoni. Yule mwanamapokezi akawatazama kidogo alafu akatabasamu na kutikisa kichwa. “Hapana, hayupo!”
.
.
“Atakuja leo?” .
.
“Yah! Atakuja. Ninyi ni wakina nani?”
.
.
“Wageni wake tu, tulikuwa na shida naye. Unaweza kuwasiliana naye kumwambia twamngoja?” .
.
“Nishajaribu hilo, nimeongea naye mara moja, lakini baada ya muda sikumpata,” akasema yule dada na kuongezea, “Nimeshampigia mara tano, hajapokea. Mara ya mwisho simu yake haikupatikana kabisa!”
.
.
“Unajua unapokaa?” akauliza Mama Brian sasa akiwa ametoa macho.
.
.
.
**
.
.
.
Gari lilipiga breki kali na kisha kukata kona kwa fujo. Mama Brian alikuwa amechanganyikiwa? Aliendesha gari upesi sana na hata wale abiria aliowabeba hawakumkataza wala kumwonya.
.
.
Aliyavuka magari mengine kwa haraka, akiwa anabadilisha gia na kukanyagia pedeli ya mafuta, akaadhibu barabara kwa ustadi. Akatembea mithili ya kishada. Uso wake ulikuwa umetambaliwa na mashaka na mikono yake ilikuwa imeshikilia usukani kwanguvu. .
.
Kitu kimoja walichokiamini ni kuwa mwanamke huyo anaweza kuwa mzima, au basi kama sivyo, atakuwa yupo hatarini kwa muda huo, kwani kwa makadirio ya muda ambao aliongea na mwenzake, ilikuwa ni asubuhi hii hii, muda mchache nyuma.
.
.
Lakini kwanini hakuuawa usiku? Sababu wauaji walikuwa wakiwamaliza maafisa wa polisi kama ilivyoonyesha wa mwisho kuuawa, afisa Williamson, kwa mujibu wa makadirio ya maelezo ya daktari, alikata moto majira ya alfajiri.
Read more
Alikuwa anatisha kwa urefu wake. Brian alitetemeka na akatamani kupiga kelele kwanguvu sana. ...
Media Removed
Alikuwa anatisha kwa urefu wake. Brian alitetemeka na akatamani kupiga kelele kwanguvu sana. Mwili ulimuisha nguvu. Mkojo ulimbana, maungio ya mwili yalipata ganzi! . . Kecie alijificha nyuma ya mwili wa mwanaume huyo, naye pia akiwa na uso wa hofu kuu. . . “Unafuata nini kwenye himaya ... Alikuwa anatisha kwa urefu wake. Brian alitetemeka na akatamani kupiga kelele kwanguvu sana. Mwili ulimuisha nguvu. Mkojo ulimbana, maungio ya mwili yalipata ganzi!
.
.
Kecie alijificha nyuma ya mwili wa mwanaume huyo, naye pia akiwa na uso wa hofu kuu. .
.
“Unafuata nini kwenye himaya ya walio wafu?” sauti nzito ikauliza. .
.
Brian hajajibu, akazabwa kofi kali sana. Akapaa juu na kwenda kujikita ukutani na kupoteza fahamu papo hapo! Hakujua tena kilichoendelea. Alipokuja kufungua macho, hajui hata majira, akajiona yu sebuleni kwao. Kichwa kilikuwa kinamuuma sana, haswa upande wake wa kulia. .
.
“Mama!” akaita.
.
.
“Brian!” mama yake akamjongea upesi kumtazama. “Brian, mwanangu. Unaendeleaje?”
.
.
“Kichwa kinaniuma sana …” Brian akatazama kushoto na kulia kwake, akamwona Mrs Garett na Olivia. Akaita, “… Olivia.” kabla hajaongeza neno, kichwa kikamgonga sana, akakunja uso wake kus’kizia. .
.
“Pumzika, Brian,” mama yake akamsihi. “ulipoteza fahamu ghafla.”
.
.
“Mlikuta Olivia?” Brian akauliza.
.
.
“Ndio. Olivia alikuwa ndani. Tulistaajabu kukuona wewe ukikimbia kwenda huko nje.”
.
.
“Alikuwa ndani? Mbona sikumwona? Wote hatukumwona!”
.
.
“Sisi tulimwona, alikuwa amelala kitandani. Tulikuambia lakini hukutuelewa. Tulistaajabu unakimbilia nje. Tulipokufuata tulikukuta ukiwa umezirai, umelala barabarani!”
.
.
Brian akaduwazwa na hayo maelezo. Yule hakuwa Olivia? Mbona alimwona vivyo? Basi na ilikuwa ni njia ya Kecie kumpeleka kule kwenye ulimwengu mwingine. Ulimwengu ambao Helo aliuita wa wafu. .
.
Hakuwa anaota. Ulimwengu huo ni wa dhati. Maumivu ya kofi zito alilozabwa, bado alikuwa anayasikia sana yakiathiri sikio lake la kulia. Akawaza, atamwokoaje Kecie kule? Na je baada ya yeye kuondoka huko, Helo atamfanya nini Kecie?
Read more
Olivia akacheka. Ila punde akanyong’onyea, akapoteza nguvu zote na kufunga macho yake, alafu ...
Media Removed
Olivia akacheka. Ila punde akanyong’onyea, akapoteza nguvu zote na kufunga macho yake, alafu akadondokea chini. Brian hakuelewa nini kimetokea. . . Alipotazama koridoni, akamwona Wisconsin akiwa amesimama. Mara upesi Wisconsin akamkimbilia na kumuuliza, “Brian, upo sawa?” ... Olivia akacheka. Ila punde akanyong’onyea, akapoteza nguvu zote na kufunga macho yake, alafu akadondokea chini. Brian hakuelewa nini kimetokea.
.
.
Alipotazama koridoni, akamwona Wisconsin akiwa amesimama. Mara upesi Wisconsin akamkimbilia na kumuuliza, “Brian, upo sawa?” kabla Brian hajajibu, akamtazama Olivia aliyekuwa pembeni. Alikuwa amelala kama mtu asiye na ufahamu. .
.
“Nipo sawa,” akajibu, alafu akanyanyuka na kusimama. “Nini kimetokea?” Wisconsin akauliza.
.
.
**
.
.
“Alikuwa amebadilika,” alisema Brian aliyekuwa anatazama dari akiwa amejilaza kitandani. Pembeni yake alikuwa amelala Wisconsin naye akiwa anatazama dari huku akimsikiza Brian kwa umakini. Bado ni usiku, muda mchache baada ya Brian kutoka kupambana na Olivia.
.
.
“Macho yake yalikuwa yanawaka. Alikuwa ni mwenye nguvu ajabu. Sijui ni nini kilimtokea.”
.
.
Kukawa kimya kidogo kabla ya Wisconsin kuuliza, “Nini kilikuamsha, Brian?”
.
.
“Sifahamu,” Brian akajibu. “Nilijikuta nikiwa macho. Baada ya muda mfupi ndiyo nikasikia mlango ukifunguliwa. Nilipoenda kutazama, nikamkuta Olivia akiwa chumbani mwa Karen.”
.
.
Wisconsin akamtazama Brian na kumwambia, “Olivia atakuwa alitumwa kutekeleza ujumbe wa Padri Alfonso. Ametumia mwili wake kutekelezea kazi.”
.
.
Brian akauliza, “Vipi? Kutakuwa na matatizo juu ya hilo?”
.
.
“Sijajua,” Wisconsin akajibu kisha akakaa kimya kwa kama sekunde tatu, alafu akasema, “Sikujua kama kazi hii itakuwa kubwa kiasi hiki. Ni kazi pevu sana. Mategemeo yangu ya kuimaliza ndani ya siku tatu yameshindikana, na hata sasa sijui itakwisha lini. Inabidi nifanye namna Brian.”
.
.
“Namna ipi hiyo?” Brian akauliza. Naye akamtazama Wisconsin kwa macho ya udadisi.
Read more
. “Umejuaje kama nimetoka huko?” Brian akauliza akiketi vema kitini kumtazama mama yake aliyekuwa ...
Media Removed
. “Umejuaje kama nimetoka huko?” Brian akauliza akiketi vema kitini kumtazama mama yake aliyekuwa amesimama hatua kadhaa toka kwake. . . “Amekuja hapa kunambia.” . . “Nani? Brewster?” . . “Ndio. Amekuja hapa akaniambia ulienda kumwona.” . . “Saa ngapi?” . . “Si muda mrefu ... .
“Umejuaje kama nimetoka huko?” Brian akauliza akiketi vema kitini kumtazama mama yake aliyekuwa amesimama hatua kadhaa toka kwake.
.
.
“Amekuja hapa kunambia.”
.
.
“Nani? Brewster?”
.
.
“Ndio. Amekuja hapa akaniambia ulienda kumwona.”
.
.
“Saa ngapi?”
.
.
“Si muda mrefu tangu uondoke. Vipi amekuambia kitu?”
.
.
Kabla Brian hajajibu, alikabwa na mawazo. Brewster amewezaje kufika hapo muda mfupi baada ya yeye kuondoka. Amefanya hilo kwa kasi gani? Mama yake alimshtua kwa kurejea kumuuliza, “Amekuambia nini?”
.
.
“Hajaniambia kitu … hamna kitu alichoniambia,” alimalizia akitikisa kichwa. “Wewe amekuambia nini?” akauliza.
.
.
Mama akaketi na kumtazama Brian, akasema, “Amenisisitizia uache kuyafuatilia hayo mambo.”
.
.
Brian akasonya na kunyanyuka. “Kuna siku utaniambia mambo mengine zaidi ya hilo?” akaenda zake chumbani na kubamiza mlango.
.
.
.
**
.
.
.
“Karibu,” alisema Mrs Garett akiufungua mlango kumkaribisha Padri Alfonso. Padri huyo alikuwa amevalia shati jeusi alilolichomekea vema, shingoni lilikuwa na doa jeupe. Mkono wake wa kuume alikuwa amebebelea Biblia ya zamani.
.
.
“Ahsante,” akasema kwa tabasamu, akazama ndani na kuketi kwenye kiti. Naye Mrs Garett akaketi akimwita Olivia ambaye alimwagiza alete chai kwa ajili ya mgeni.
.
.
Padri akautazama uso wa Mrs Garett uliokuwa umeharibika kwa majeraha, akamuuliza mwanamke huyo, “Ni mume wako?”
.
.
Mrs Garett akatikisa kichwa pasipo kutia neno. Macho yake yalikuwa mekundu, mdomo wake ulikuwa umevimba na upande wa juu wa shavu lake la kushoto kulikuwa kumevilia damu.
.
.
“Pole sana.”
.
.
“Nashukuru, usijali,” Mrs Garett akasema akijitahidi kutabasamu.
.
.
“Yupo wapi sasa?”
.
.
“Ameondoka. Alisema anasafiri hivyo atarejea kesho asubuhi.”
.
.
Padri akatikisa kichwa. Baada ya muda mfupi mlango ukagongwa, akaingia mwanadada aliyekuwa amevalia sare ya mtawa wa kike rangi nyeusi na nyeupe. Mwanamke huyo mrefu mwembamba alikuwa amebebelea chupa mkononi mwake na sanamu ya msalaba yenye ukubwa wa wastani.
Read more
“Brian! Brian! Tih-tih!-tih!” alikuwa anaitwa na mlango unagongwa. Ni kama takribani dakika ...
Media Removed
“Brian! Brian! Tih-tih!-tih!” alikuwa anaitwa na mlango unagongwa. Ni kama takribani dakika ishirini tangu alipozolewa na usingizi. Alihisi huenda anaota, ila ilikuwa ni uhalisia. Alikuwa anaitwa. . . Mama yake alikuwa amesimama mlangoni akiwa ameshikilia kiuno chake kwa mkono ... “Brian! Brian! Tih-tih!-tih!” alikuwa anaitwa na mlango unagongwa. Ni kama takribani dakika ishirini tangu alipozolewa na usingizi. Alihisi huenda anaota, ila ilikuwa ni uhalisia. Alikuwa anaitwa. .
.

Mama yake alikuwa amesimama mlangoni akiwa ameshikilia kiuno chake kwa mkono wa kushoto, wa kulia akibondea mlango.
.
.
Mara punde mlango unafunguliwa Brian akiwa anafikicha macho yake. Alimtazama mamaye na kumuitikia kilevi.
.
.
“Uko sawa?” mama akauliza akifinyanga uso wake kwa hofu.
.
.
“Ndio … niko sawa!” Brian akaongea kivivu. Macho yake bado yalikuwa mekundu ila kwakuwa alitoka kulala, mama yake hakujali sana. Alishani ni usingizi.
.
.
“Mbona umelala pasipo kula?”
.
.
“Mama sisikii njaa.”
.
.
“Umekula wapi?”
.
.
Brian kimya. Mama akamtazama na kutaka kumuuliza tena kama yupo sawa, ila akasita. Akadaka kiuno chake kwa mikono yote alafu akamwambia, “Una mgeni wako sebuleni. Anataka kukuona hivi sasa.”
.
.
“Nani?”
.
.
“Mrs Garett. Fanya uje haraka.”
.
.
Mama aliposema hivyo akaenda zake kurudi sebuleni. Mama Kecie aliyekuwa ameongozana na Olivia walikuwa wameketi kwenye kochi la kwanza kabisa upande wa kulia wa mlango, akawaambia kuwa Brian yuaja muda si mrefu.
.
.
“Kweli hamtahitaji kitu?” mama Brian akauliza wageni huku akiwapatia tabasamu.
.
.
“Hapana,” Mrs Garett akasema akitikisa kichwa. “Tupo tu sawa, usijali.”
.
.
“Hata chai? Ni baridi jamani.”
.
.
“Sawa, tutashukuru.”
.
.
Mama Brian akaenda jikoni na kurejea na vikombe viwili vya chai, akawapatia Mrs Garett na Olivia. Taratibu wakawa wanavuta kimiminika hicho cha moto kumngoja Brian.
.
.
Punde Brian akafika sebuleni na kuwasalimu..
.
.
“Pole kwa usumbufu.,” Mrs Garett alisema akimtazama Brian. Kwa kumtazama tu mama huyu hakuwa sawa. Sauti yake ilikuwa ajabu na uso wake ulikuwa ulioganda. Hakuwa na lepe la furaha. Ungelitabiri vema hakukuwa na kitu kilichomfurahisha siku nzima ya leo.
Read more
** . . "Brian, amka! Brian, Brian, amka!" Sauti hiyo ya kike ilikuwa inanong'ona kwenye masikio ...
Media Removed
** . . "Brian, amka! Brian, Brian, amka!" Sauti hiyo ya kike ilikuwa inanong'ona kwenye masikio ya Brian. Hakuwa anajitambua yupo wapi. Alikuwa gizani. Tangu, dubwana lile lilipomkita tumboni kule kwenye ulimwengu wa waliohai, alipoteza nguvu na fahamu. . . Sasa anaanza kurejea ... **
.
.
"Brian, amka! Brian, Brian, amka!" Sauti hiyo ya kike ilikuwa inanong'ona kwenye masikio ya Brian. Hakuwa anajitambua yupo wapi. Alikuwa gizani. Tangu, dubwana lile lilipomkita tumboni kule kwenye ulimwengu wa waliohai, alipoteza nguvu na fahamu.
.
.
Sasa anaanza kurejea kwenye hali yake. Bado akiwa kwenye ulimwengu wa kiza! Ule wa waliokufa. Na mtu yule aliyekuwa anamhisi yupo nyuma yake, ameshamteka! Mguu wake wa kuume umedakwa na anaburuzwa.
.
.
Akafungua macho yake na kuangaza, alikuwa hajui anapelekwa wapi. Alichokiona ni mwanaume jabali akimburuza kana kwamba kiroba. .
.
Akaangaza kushoto na kulia kwake, bahati akajigongoa kwenye jiwe. Akalibeba jiwe hilo pasipo kulalamika kwa maumivu. Alivumilia. Alipoweka vema mkononi akalirusha kumbamiza yule aliyemshika, naye akageuka na kumtazama.
.
.
Alikuwa ni Helo!
.
.
Alimdaka Brian kwanguvu, na mara kule kwenye ulimwengu wa waliohai, mwili wa Brian ukaanza kuchuruza damu puani!
.
.
Puh! Brian akatupwa chini. Kabla hajakaa sawa, akazabwa teke kali la kichwa. Akahisi kupoteza fahamu. Akiwa ameshajua ameshakwisha, hajui tena alipo, akasikia tena sauti ya kike ikimwambia, "amka! Brian, amka!"
.
.
Akafungua macho yake kuangaza, akaona akiwa ameshakaribia kwenye makazi yale yaliyokuwa na mwanga hafifu aliouona kwa mbali. Akajikakamua. Kidogo,  bwana yule akamshtukia. Akamwapua na kumbeba kuzama naye ndani. Akiwa amebebwa, Brian akasikia sauti za funguo mfukoni mwa Helo.
.
.
Walipofika kwenye chumba fulani, Brian akatupiwa humo na kisha Helo akasimama akimuuliza ni nini amekuja kufanya huko kwenye ardhi ya wafu. .
.
"Kwanini waja huku na hutaki kusikia?" Na akahitimisha, ".. yanipasa nikuue ile uje kutuama huku kabisa maana unapapenda!"
.
.
Akamsogelea Brian amnyake, ila ghafla akasikia sauti za watu wakiwa wanagongagonga mlango. Akanguruma kuguna na kutoka humo ndani kwenda huko aliposikia sauti. Ilikuwa ni kwenye chumba ambacho amewafungia mateka wake. Mateka wa kiroho anaowatumikisha. Humo ndani alikuwapo pia na Kecie.
.
.
Akafoka, "mnataka nini? Kufa mara ya pili!"
Read more
Brian akashika tama, "ilinipasa niende naye, tumempa mzigo mku--" akakatishwa na sauti ya gari ...
Media Removed
Brian akashika tama, "ilinipasa niende naye, tumempa mzigo mku--" akakatishwa na sauti ya gari huko nje. Upesi wakatoka kuelekea huko. Alikuwa ni Wayde! . . Alishuka kwenye gari upesi na kumkimbilia Brian akiwa analia. "Pole, Wayde." Brian akambembeleza. "Usijali, yatakuwa sawa." . . Wayde ... Brian akashika tama, "ilinipasa niende naye, tumempa mzigo mku--" akakatishwa na sauti ya gari huko nje. Upesi wakatoka kuelekea huko. Alikuwa ni Wayde!
.
.
Alishuka kwenye gari upesi na kumkimbilia Brian akiwa analia. "Pole, Wayde." Brian akambembeleza. "Usijali, yatakuwa sawa."
.
.
Wayde akalia kwa kama sekunde sita, alipojibandua toka kwenye bega la Brian akajifuta machozi kwa kutumia mikono ya sweta alilovaa, kisha akasema, "nimefanikisha!"
.
.
"Kweli?" Brian akatahamaki. Wayde akatikisa kichwa, "kweli Brian." .
.
"Hongera sana!" Wisconsin akampongeza, "sasa twende ndani haraka!" Wakazama ndani na upesi wakaelekea chumbani kwa Brian kuchukua kile kitabu cha Wisconsin. Ajabu walipofika, hawakukiona!
.
.
"Kilikuwa hapa!" Alisema Wisconsin akiangaza kwenye kabati dogo linalopakana na kitanda. Akafungua droo zote, hamna kitabu!
.
.
"Atakuwa kachuku--" Wisconsin alisema na kusita. Haraka akanyanyuka na kwenda chumba cha Olivia, huko wakakuta kamba zikiwa kitandani, hamna mtu. .
.
"Tumtafute Olivia!" Wisconsin akasihi akiwa aliyechanganyikiwa. Kidogo, wakasikia mlango ukibamizwa. Wakatazamana. Upesi wakatoka chumbani kuelekea huko. Walipofika, wakamwona Olivia kwa mbali akiwa anakimbia! Mkononi alikuwa amebebelea kitabu.
.
.
"Yule kule!" Wisconsin akapayuka. Basi haraka Brian akaanza kutupa miguu yake kwa fujo kumkimbiza Olivia. Kasi ya Wisconsin na Wayde ilikuwa hafifu kwake. Alikuwa anakimbia mno karibia visigino viguse kisogoni!
.
.
Akawa anamkaribia Olivia zaidi na zaidi, na huku akiwa amewaacha wenziwe huko nyuma wasionekane kabisa. Kidogo, Olivia akazama msituni na kuanza kupotelea humo. Naye Brian alipopiga kwanja, akazama mitini. Huyo! Huyo! Akimkimbiza Olivia anayepepea kama kishada.
.
.
Akaruka viunzi, matawi na vichaka, akaendelea kukimbia! Akazidi kumsogelea Olivia zaidi na zaidi ya zaidi. Kwa makadirio isingepita sekunde nne angekuwa ameshamtia Olivia mkononi, ila ghafla, mguu wake ukadakwa na mzizi wa mti, akachumpa na kudondoka chini kama kifurushi!
Read more
Wayde akasema, “Nadhani unaweza ukawa unamjua mwanamke huyo.” Brian akatikisa kichwa. “Simfahamu. ...
Media Removed
Wayde akasema, “Nadhani unaweza ukawa unamjua mwanamke huyo.” Brian akatikisa kichwa. “Simfahamu. Wewe unamjua?” . . Wayde akaendea kabati dogo lililokuwepo ndani ya chumba hicho akatoa picha aina ya ‘passport’ na kumkabidhi Brian. . . “Bado haujamjua?” Wayde akauliza akimtazama ... Wayde akasema, “Nadhani unaweza ukawa unamjua mwanamke huyo.” Brian akatikisa kichwa. “Simfahamu. Wewe unamjua?”
.
.
Wayde akaendea kabati dogo lililokuwepo ndani ya chumba hicho akatoa picha aina ya ‘passport’ na kumkabidhi Brian. .
.
“Bado haujamjua?” Wayde akauliza akimtazama Brian aliyekuwa anaikodolea macho picha ile. Punde akasema, “Hii sura si ngeni.”
.
.
“Umewahi kuiona wapi?” Wayde akauliza. Kidogo, Brian akapata kumbukumbu. “Niliiona kwenye ofisi ya mkuu wa - ni mke wa Dkt Hamill!”
.
.
Wayde akatikisa kichwa. “Ndio, ni yeye.”
.
.
“Baba yako alikuwa anatembea na mke wa Dkt Hamill?” Brian akauliza kana kwamba haamini alichopata kuelewa.
.
.
“Ndio,” Wayde akajibu. “Kipindi hiko kabla sijazaliwa, miaka mingi iliyopita.” Wayde akaketi kwenye kiti na kuendelea kusema, “Inaelekea baba alikuwa anampenda sana Magreth, hata leo hii hakutoa picha wala barua zake kwenye hifadhi. Najiuliza sana yu wapi huyu mwanamke?”
.
.
“Amekufa,” Brian akamjibu na kuongezea, “Dkt Hamill alimuua mkewe. Ameandika hivyo kwenye diary.”
.
.
“Kweli?” Wayde akatahamaki.
.
.
“Ndio,” Brian akajibu. “Nadhani ni kwasababu ya mahusiano ambayo Magreth alikuwa nayo na baba yako, na huo mkufu ambao Magreth anauongelea kutoka kwa baba yako, itakuwa ndiyo kitu kilichomfanya Dkt Hamill akahakiki mahusiano baina yao. Hata kwenye diary ya Dkt Hamill, mkufu huo ameuweka kwenye karatasi inayokiri kuwa amemuua kwa kumchoma kisu.”
.
Wayde akashangazwa sana na hizo habari, lakini Brian hakuwa amemaliza kueleza. Akasema pia kuwa Dkt Hamill aliua watoto wake watatu, wote kwa kuwachoma kisu. Hapa kila mmoja akawa na maswali. Hakuna aliyekuwa anajua kwanini Dkt Hamill alifanya tukio hilo la kinyama.
. “Naomba niende, Wayde,” akasema Brian. “Tuonane kesho, nadhani nitakuwa na cha kukuambia zaidi.”
.
.
“Sawa, acha nikusindikize.” Wayde akafunga kila kitu na kutoka Brian mpaka kwenye usafiri wake, akampeleka kijana huyo nyumbani kwao.
.
.
**
Read more
“Ziko wapi sasa?” Wisconsin akadadisi. . . “Zilipeperushwa na upepo wa ajabu tukiwa safarini ...
Media Removed
“Ziko wapi sasa?” Wisconsin akadadisi. . . “Zilipeperushwa na upepo wa ajabu tukiwa safarini kuja kule kwako,” Brian akaeleza. Kidogo Wisconsin akatulia, akavuta tena kiko chake akiwaza alafu akamtazama Brian na kumwambia, “pengine ungesoma na kuzimaliza nyaraka hizo ungekuwa ... “Ziko wapi sasa?” Wisconsin akadadisi. .
.
“Zilipeperushwa na upepo wa ajabu tukiwa safarini kuja kule kwako,” Brian akaeleza. Kidogo Wisconsin akatulia, akavuta tena kiko chake akiwaza alafu akamtazama Brian na kumwambia, “pengine ungesoma na kuzimaliza nyaraka hizo ungekuwa umebadilisha mawazo juu ya Dkt Hamill.”
.
.
Kauli hiyo ikamtia Brian hamasa ya kutaka kujua zaidi. “Kwanini unasema hivyo?” akauliza. .
.
Wisconsin akakuna kidevu chake na kusema, “Dkt Hamill aliua familia yake. Kwa mkono wake, alimmaliza mkewe na watoto akitumia kisu kirefu chenye ncha kali.”
.
.
“Kwanini afanye hivyo?” Brian akastaajabu.
.
.
“Labda kabla hatujajua kwanini alifanya hivyo, inabidi kwanza ujue kuwa Dkt Hamill alikuwa na familia ya watoto watatu, wawili walikuwa wa kiume na mmoja akiwa wa kike. Alifanikiwa kuwapata watoto hao akiwa kwenye enzi za ujana wake. .
.
Pengine aliwapenda sana, mimi na wewe hatufahamu maana hatukuwapo. Ila tulilo na uhakika nalo ni kuwa alikuja kuwaua pamoja pia na mkewe. Nililikuta hilo kwenye ‘diary’ yake.”
.
.
Wisconsin akazamisha mkono ndani ya koti lake na kutoa kijitabu kidogo chenye jalada gumu jeusi, akampatia Brian.
.
.
Brian akakikagua na huku Wisconsin akiendelea kunena. “Sijajua kwanini aliua familia yake, kutakuwa na sababu kubwa nadhani. Lakini kwenye karatasi ambayo alikuwa ameeleza ya kuwa amehusika na kuua familia yake, alikuwa ameweka hapo mkufu wenye kidani cha kito cha kijani, kito cha duara.”
.
.
Wisconsin akazamisha tena mkono wake ndani ya koti lake na kutoa mkufu huo. Akautazama kwa muda kidogo alafu akamkabidhi Brian.
.
.
“Shida si kwamba amewaua familia yake. Tunaweza tukapuuzia juu ya hilo, ila tatizo ni kwamba, makaburi ya wanawe sikuyaona isipokuwa lile la mkewe tu. Ukifungua kwenye diary yake, utaona ameelekeza juu ya wapi alipomzika mkewe, lakini kuwahusu watoto wake, hamna anayejua. Hajaeleza wapi walipo.”
Read more
Alipofika nyumbani, baada ya kula na kupumzika kidogo, akatoka pasipo kuaga. Akaenda nyumbani ...
Media Removed
Alipofika nyumbani, baada ya kula na kupumzika kidogo, akatoka pasipo kuaga. Akaenda nyumbani kwa Brewster, mwanaume mzee ambaye alimweleza mama yake juu ya safari yake ya kwenda nyumbani kwa wakina Faris, na pia kumtahadharisha asifanye tena hilo jambo. . . Alitumai atapata mawili ... Alipofika nyumbani, baada ya kula na kupumzika kidogo, akatoka pasipo kuaga. Akaenda nyumbani kwa Brewster, mwanaume mzee ambaye alimweleza mama yake juu ya safari yake ya kwenda nyumbani kwa wakina Faris, na pia kumtahadharisha asifanye tena hilo jambo.
.
.
Alitumai atapata mawili matatu kwa mzee huyo. Alikuwa na maswali kadhaa ya kumuuliza.
.
.
Basi kwa mwendo wa robo saa, akawa amefika nyumbani kwa mzee huyo. Ilikuwa ni nyumba ndogo iliyojitenga. Kulikuwa ni kimya sana. Nje ya nyumba kulikuwa kumejawa na majani makavu ya miti. Kibaraza hakikuwa kisafi, pia na vioo vilikuwa vimebadilisha rangi.
.
.
Juu ya paa kulikuwa na kunguru wawili wakimtazama Brian kwa macho ya pembeni kabla hawajalia mara mbili na kupeperusbha mbawa zao. .
.
“... kuna yeyote ndani?” Brian aliita baada ya kugonga mara tano pasipo majibu. Aliacha kugonga akazunguka nyuma ya nyumba. Huko akakuta banda la nguruwe wawili wadogo. Akapumbazwa kuwatazama rangi zao na namna wanavyokula kwa kufakamia. Ila ghafla akasikia sauti kavu nyuma yake.
.
.
“Hey! We mvulana.”
.
.
Alipogeuka akamwona Brewster. Alikuwa amevalia shati refu na suruali pana. Uso wake ulikuwa mtulivu ila macho yake ya kizee ameyakodoa. Mashavu yake yaliyoanza kudondoka yalikuwa yamemezwa na vinyweleo vya ndevu vilivyosimama. Mdomo wake mwembamba ulikuwa unaonekana kwa hafifu kwasababu ya mustachi.
.
.
“We ni nani na unafanya nini hapo kwa nguruwe wangu?” akauliza Brewster. Brian akamsogelea na kujitambulisha, akamwambia ya kwamba amekuja kumtembelea kwani kuna maneno mawili matatu anataka kuyaongea naye.
.
.
“Ni wewe, Brian!” akastaajabu Brewster. Alikuwa ana tatizo la kuona mbali hivyo Brian alivyosogea karibu na kuongea ndipo akamtambua.
Read more
Koti jeusi la kumbana, suruali iliyoshika mapaja na nyonga zake kisha kubwaga huko chini. Miguuni ...
Media Removed
Koti jeusi la kumbana, suruali iliyoshika mapaja na nyonga zake kisha kubwaga huko chini. Miguuni ana viatu vyenye visigino virefu na kuchongoka kwa mbele. Mikononi amevalia glovu nyeusi malighafi ya ngozi. . . Vitu vyote hivyo ambavyo vimetajawa vilikuwa vyametameta kana kwamba ... Koti jeusi la kumbana, suruali iliyoshika mapaja na nyonga zake kisha kubwaga huko chini. Miguuni ana viatu vyenye visigino virefu na kuchongoka kwa mbele. Mikononi amevalia glovu nyeusi malighafi ya ngozi.
.
.
Vitu vyote hivyo ambavyo vimetajawa vilikuwa vyametameta kana kwamba nyota angani!
.
.
“Helo!” Brian akajikuta ananong’ona mwenyewe akistaajabu. Mbele ya macho yake alikuwapo mwanaume ambaye amekuwa akisikia tu simulizi zake. Mwanaume aliyewahi kutikisa Boston na Massachusetts nzima!
.
.
Bado mwanaume huyo alikuwa amevalia nguo zake alizokuwa anatumbuiza nazo, hata picha zake huko ukutani zilikuwa zamwonyesha hivyo.
.
.
Hakika alipendeza na basi ungetamani umwone akiwa anatumbuiza. Lakini endapo ungekumbuka kuwa mtu huyu ni mfu, ungepoteza hamu yote! Mtu aliyechomwa moto miaka iliyopita na hata nyumba yake kutiwa pia motoni, leo yu hai, mzima na anacheza!
.
.
Pembeni yake kulikuwa na santuri ya kale iliyokuwa inamimina muziki wa bluzi. Hakika muziki huu ulikuwa unamkonga moyo wake, alikuwa akiimba pamoja nao na muda mwingine akijikuta anapiga kelele kali za nguvu!
.
.
Lakini sura yake haikuwa inaonekana. Alikuwa amempa mgongo Brian. Kichwa chake anakitikisatikisa na mkono wake uliopo ndani ya glovu unatengeneza ala kwa vidole. .
.
Brian atamfanya nini mtu huyu? Akatazama nyuma, akakutana uso kwa uso na Kecie. Kecie hakusema jambo, bali akaendelea kumnyooshea kidole huko mbele, yaani sebuleni. Brian alipotazama tena kule sebuleni, Helo hakuwapo! Kiti pekee kilikuwa kinachecheza.
.
.
Moyo wa Brian ukalipuka kwa woga sana. Akapepesa macho yake kule na kule, hakumwona Helo. Hakujua wapi ameenda, tena ‘hafla hivyo! Kurudisha uso kwa Kecie, hapo akamwona mwanaume mrefu akiwa amesimama! Mwanaume mzito aliyeshiba. .
.
Uso wake haukuwa unaonekana kwa kufichwa na kivuli cha kofia. Nguo zake zilikuwa zametameta, zang’aa, kana kwamba vito vya almasi vimeshikiziwa kwenye shuka.
Read more
Hapa sasa ndiyo akatamani kupiga kelele. Haraka akamrejeshea Wisconsin kile kikaratasi kisha ...
Media Removed
Hapa sasa ndiyo akatamani kupiga kelele. Haraka akamrejeshea Wisconsin kile kikaratasi kisha akamshtua Mama yake kumtaka waende nyumbani haraka iwezekanavyo! . “Yupo nyumbani!” Brian alisema akiwa amekunja ndita, macho yamejawa na woga. Nyumbani alikuwa amebakia Olivia pekee. . . Basi ... Hapa sasa ndiyo akatamani kupiga kelele. Haraka akamrejeshea Wisconsin kile kikaratasi kisha akamshtua Mama yake kumtaka waende nyumbani haraka iwezekanavyo!
. “Yupo nyumbani!” Brian alisema akiwa amekunja ndita, macho yamejawa na woga. Nyumbani alikuwa amebakia Olivia pekee.
.
.
Basi wakatoka upesi na kwenda kwenye gari. Mama akatia ufunguo na kuwasha chombo, ila kabla hawajaondoka, akamwona Padri Alfonso kwa mbali akiwa amesimama na watu watatu wanateta!
.
.
Akauliza akistaajabu, “si yule?” wote wakatazama. Kweli alikuwa ndiye. Wakiwa kwenye buwazo hilo, Padri Alfonso akawapatia mkono watu wawili aliokuwa amesimama nao, kisha akaanza kutembea kulifuata gari walilopo wakina Brian.
.
.
“Mama, twende!” Brian akasema akimpigapiga mama yake begani, lakini Wisconsin akasema, “Hapana.” wote wakamtazama kwa nyuso za kushangaa. .
.
“Ngoja tuone atafanya nini mbele za watu!”
.
.
Basi punde Padri Alfonso akawafikia na kutabasamu. Akawasalimu na kuwakaribisha kwa ukarimu. .
.
“Kuna tatizo lolote?” akauliza.
.
.
Mama Brian akawahi kutikisa kichwa na kusema, “Hamna!”
.
.
“Una uhakika?” Padri Alfonso akauliza.
.
.
“Ndio, hamna!” Mama akasihi. “Nashukuru, padri.”
.
.
Padri akamtazama na kumuuliza kwa mara nyingine, “Una uhakika?” sasa hivi macho yake alikuwa ameyakodoa. Mama Brian akasihi baridi na moyo wake waenda mbio.
.
.
Ghafla Padri akatabasamu na kusema, “Msijali.” kisha akaenda zake.
.
.
.
****
.
.
Lako jicho!
Read more
ILIPOISHIA . . “Una uhakika?” Padri Alfonso akauliza. . . “Ndio, hamna!” Mama akasihi. “Nashukuru, ...
Media Removed
ILIPOISHIA . . “Una uhakika?” Padri Alfonso akauliza. . . “Ndio, hamna!” Mama akasihi. “Nashukuru, padri.” . . Padri akamtazama na kumuuliza kwa mara nyingine, “Una uhakika?” sasa hivi macho yake alikuwa ameyakodoa. Mama Brian akahisi baridi na moyo wake waenda mbio. . . Ghafla ... ILIPOISHIA
.
.
“Una uhakika?” Padri Alfonso akauliza.
.
.
“Ndio, hamna!” Mama akasihi. “Nashukuru, padri.”
.
.
Padri akamtazama na kumuuliza kwa mara nyingine, “Una uhakika?” sasa hivi macho yake alikuwa ameyakodoa. Mama Brian akahisi baridi na moyo wake waenda mbio.
.
.
Ghafla Padri akatabasamu na kusema, “Msijali.” kisha akaenda zake.
.
.
ENDELEA
.
.
Wakamtazama Padri akiishia na kisha Mama akaondoa chombo hapo msibani kurudi zao nyumbani. Walipomfika wakamkuta Olivia akiwa ameketi sebuleni anatazama runinga akila.
.
.
“Uko sawa, Olivia?” Mama akauliza. Olivia akatikisa kichwa chake na kumjibu kiufupi, “Ndio.” kisha akaendelea kutazama runinga kana kwamba hamna mtu. .
.
Badae , baada ya kupumzika, ikiwa ni majirani ya jioni, Wisconsin akamwita Brian na kumtaka watoke kidogo kwani ana maongezi naye. Wakitumia usafiri wa Mama, wakaenda kwenye moja ya bustani inayopatikana katikati mwa mji wa Boston, hapo wakatulia kwenye mojawapo ya viti vinavyopatikana kwenye maeneo hayo, alafu Wisconsin akasema,
.
.
“Niambie machache unayoyajua kuhusu Hamill, Dkt. Hamill.”
.
.
Brian akamtazama kwanza Wisconsin kabla hajasema jambo. Kwa kiasi fulani alikuwa ameshangazwa na hilo swali. Aliwatazama watoto waliokuwa wanacheza bustanini alafu baada ya muda kidogo, akasema, “Sina mengi ya kusema juu yake. Alikuwa ni mmoja wa watu wazuri ninaowajua, mwenye upendo na haja ya kusaidia wengine. Japo maisha yake yaligubikwa na upweke.”
.
.
Wisconsin akaingiza mkono wake ndani ya mfuko wa koti, humo akatoa kiko chake na kibiriti, akawasha na kuanza kuvuta. Akavuta mapafu manne alafu akasema sasa kwa kinywa chake kikavu, “Hakuna kitu chochote alichowahi kukwambia juu ya familia yake?”
.
.
“Kidogo,” Brian akajibu. “Mke na watoto wake walifariki na kumwacha mkiwa.”
.
.
“Nini kiliwaua?” Wisconsin akauliza. “Alikwambia nini kimewaua?”
.
.
Brian akatikisa kichwa. “Hapana,” akasema. “Hakuwahi kunambia, ila …” Wisconsin akamtazama kwa jicho la udadisi. “Aliniachia nyaraka zake tatu nizipitie. Zilikuwa zinahusu maisha yake, lakini sikupata muda wa kuzimaliza kusoma.”
Read more
Alipomalizia hiyo kauli yake, Brian akamwona Wisconsin akiwa amesimama dirishani. Alikuwa tayari ...
Media Removed
Alipomalizia hiyo kauli yake, Brian akamwona Wisconsin akiwa amesimama dirishani. Alikuwa tayari amesharejea. Mama akaenda kuongea naye na muda mfupi, Wisconsin akaingia ndani kukutana na Brian. . . “Unaendeleaje, mshindi?” . . “Niko sawa. Nadhani nastahili tu kurudi nyumbani.” ... Alipomalizia hiyo kauli yake, Brian akamwona Wisconsin akiwa amesimama dirishani. Alikuwa tayari amesharejea. Mama akaenda kuongea naye na muda mfupi, Wisconsin akaingia ndani kukutana na Brian.
.
.
“Unaendeleaje, mshindi?”
.
.
“Niko sawa. Nadhani nastahili tu kurudi nyumbani.” Wisconsin akatabasamu. “Mama yako anaona uendelee kubaki hapa mpaka upone kabisa.”
.
.
“Haitawezekana,” Brian akatikisa kichwa, Wisconsin akaangua kicheko. “Mimi siwezi kulala humu hospitali, unajua Wisconsin. Tuna mambo mengi ya kufanya. Inabidi umwambie Mama hilo.”
.
.
“Usijali,” Wisconsin akamtoa hofu. “Kila kitu kitakuwa sawa, Brian. Unajua nini?”
.
.
Brian akamtazama Wisconsin kwa kuitikia. .
.
“Kama ingekuwa ni kufa, basi ungeshakufa Brian. Tena muda sana. Mungu yupo upande wako.” akamshika Brian mkono na kumtazama machoni. “Utashinda hata na hili.”
.
.
Brian naye akamshika mkono na kumwambia, “Tutashinda wote.” Wisconsin akatabasamu pasipo kutia neno. Brian akamuuliza, “Kuna lolote ambalo umegundua?”
.
.
Wisconsin akakuna pua yake na kushusha pumzi ndefu kisha akajitengenezea pale kitandani alipokuwa amekaa. Akaita, “Brian.” Brian akaitikia kwa kuguna. “Olivia ndiye yule mtoto wa mwisho wa Dkt Hamill.”
.
.
Habari hizi hazikumshangaza sana Brian. Ni kama vile alikuwa anazitarajia. Matukio ya Olivia, na zaidi juu ya ule mkufu yalimtia mashaka. Akauliza, “Sasa tunafanyaje? Kutakuwa na shida yoyote?”
.
.
“Ndio, shida ipo tena kubwa,” Wisconsin akajibu na kuongeza, “Olivia, Brewster pamoja na Alfonso, wote ni mali ya Helo. Wote walitolewa sadaka kumtumikia mdhalimu huyo. Nadhani utakuwa ushajua ni shida kiasi gani.”
.
.
“Hatuwezi kulibadili hilo?” Brian akauliza. Wisconsin akabinua mdomo wake na kusema, “Haiwezekani, Brian. Pumzi yake, maisha yake ni mali ya Helo. Wapo hapa duniani kutimiza maagizo hayo. Laiti Helo angelikuwa hajaamka, basi wangelikuwa sawa. Wangeweza kuendelea na maisha yao pasipo bughudhi ya watu.”
Read more
** . . Brian akakohoa. . . "Ameamka!" Mama akalipuka kwa furaha. Akamkumbatia mwanaye kwanguvu ...
Media Removed
** . . Brian akakohoa. . . "Ameamka!" Mama akalipuka kwa furaha. Akamkumbatia mwanaye kwanguvu na kumbusu kwenye paji la uso. Wayde naye akamkumbatia na kisha Wisconsin. Walikuwa wamemaliza na kufaulu mtihani! . . Walijawa na furaha tele. Punde Karen akajiunga nao, wakafanya ... **
.
.
Brian akakohoa. .
.
"Ameamka!" Mama akalipuka kwa furaha. Akamkumbatia mwanaye kwanguvu na kumbusu kwenye paji la uso. Wayde naye akamkumbatia na kisha Wisconsin. Walikuwa wamemaliza na kufaulu mtihani!
.
.
Walijawa na furaha tele. Punde Karen akajiunga nao, wakafanya tafrija fupi. Kesho yake Wayde akarejea kwao na kupewa taarifa kuwa baba yake alikuwa hospitalini akiendelea vema.
.
.
Alipomweleza baba yake kilichotukia akiwa kitandani amelazwa, baba yake akamshika mkono kwanguvu na kumwambia, "umefanya kile ambacho sisi tulishindwa." Kisha akatabasamu na kumbusu, "hauna haja ya kuomba msamaha. Najivunia kuwa nawe."
.
.
.
**MWISHO**
Read more
Loading...