Loading Content...

Siku ya nne tangu

Loading...


Unique profiles
1
Most used tags
Total likes
0
Top locations

Average media age
697.9 days
to ratio
Pengine ulikuwa ni usiku kama usiku mwingine kwako, ila kwa Gabriella, mnamo tarehe 16, mwezi wa ...
Media Removed
Pengine ulikuwa ni usiku kama usiku mwingine kwako, ila kwa Gabriella, mnamo tarehe 16, mwezi wa pili mwaka 2010, haukuwa usiku wa kawaida hata kidogo. Gabriella, mwanamke mwenye nywele rangi ya tangawizi, macho makubwa na vidotidoti shavuni mwake, alikuwa ni mke wa bwana Rodney Wallgate, ... Pengine ulikuwa ni usiku kama usiku mwingine kwako, ila kwa Gabriella, mnamo tarehe 16, mwezi wa pili mwaka 2010, haukuwa usiku wa kawaida hata kidogo. Gabriella, mwanamke mwenye nywele rangi ya tangawizi, macho makubwa na vidotidoti shavuni mwake, alikuwa ni mke wa bwana Rodney Wallgate, afisa wa jeshi ambaye alikwenda kupambania nchi yake vitani.
.
.
Hivyo kwa takribani miaka miwili, Gabriella, akawa anaishi mwenyewe pamoja na watoto wake wawili mapacha, kwa majina Natalie na Paulie. Kwa mwanzoni ilikuwa inamuwia vigumu sana kuishi pasi na mume wake, ila kadiri na muda ulivyokuwa unasonga akajikuta anazoea hali hiyo.
.
.
Aliishi vema kabisa japo kuna muda alijihisi mnyonge na upweke. Angalau watoto wake walikuwa wanamfariji ingawa hakuwapo wa kuondoa baridi kitandani kwake.
.
.
Akiwa anaishi vivyo, Gabriella alikuja kugundua kuwa, ikiwa ni kama miezi mitatu tangu mume wake aende vitani, kila alipokuwa anaamka asubuhi, angekuta ‘missed calls’ toka namba mpya. .
.
Hakuwa anajua ni nani anampigia, na kila alipojaribu kupigia namba hiyo isingepatikana kabisa akijibiwa kuwa namba anayopiga haipo! Kwa takribani siku tatu, akawa anakuta ‘missed calls’ vivyo hivyo kila asubuhi. Ikaja fikia kipindi akaona ni kheri kama angeamka katikati ya usiku ili apate kupokea simu hiyo. Mawazo yake akidhani huenda anayempigia ni mumewe.
.
.
Basi siku iliyofuata, yaani ya nne, Gabriella akiwa amelala, kheri kwake akaisikia simu ikiita. Ulikuwa ni usiku wa saa tisa na dakika kumi na mbili kwa mujibu wa saa ya ukutani. Simu yake ilikuwa inaimba na kutetemesha meza ya taa.
Read more
Loading...
Kauli hizo zikanifanya nihofie kidogo, lakini kujazwa na hamu juu ya nini kimemtokea Oliva. Lakini ...
Media Removed
Kauli hizo zikanifanya nihofie kidogo, lakini kujazwa na hamu juu ya nini kimemtokea Oliva. Lakini kwasababu za kutoskizana vema ndani ya basi, tukaona ni vema tuendeleze hiyo soga yetu tukifika nyumbani. . . Tulipofika na kupumzika kidogo yule jamaa yangu akaendeleza kwa kuniambia ... Kauli hizo zikanifanya nihofie kidogo, lakini kujazwa na hamu juu ya nini kimemtokea Oliva. Lakini kwasababu za kutoskizana vema ndani ya basi, tukaona ni vema tuendeleze hiyo soga yetu tukifika nyumbani.
.
.
Tulipofika na kupumzika kidogo yule jamaa yangu akaendeleza kwa kuniambia kwamba Oliva hakuweza kufanya mitihani yake ya kidato cha nne na hivyo basi anatazamia kurudia tena mwaka huu. Ila ni miaka mingi imepita, kwanini hakurudia miaka yote hiyo aje kurudia mwaka huu? Niliuliza.
.
.
Basi hapa ndipo akanieleza kuwa Oliva wakati anakaribia kufanya mitihani yake ya kidato cha nne, aliamua kuhama nyumbani kwao na kwenda kukaa hosteli ili apate muda zaidi wa kujisomea na wenzake.
.
.
Huko alikuwa anakaa ma wasichana wengine wawili na wakawa wanasoma kila siku usiku na hata mchana. Lakini ikiwa ni wiki moja tu tangu Oliva ahamie hapo hosteli, akaanza kupatwa na mambo ya ajabu. Hakuwa anaweza kuamka usiku tena. Kila alipoamshwa kichwa kilikuwa kizito sana, hata kuuma.
.
.
Na endapo akijilazimisha asome tu, damu huvuja puani na kuumwa na kichwa pasi na mfano! Hivyo basi akawa anatumia muda wa mchana kusoma japo ulikuwa finyu kutokana na ratiba zingine.
.
.
Alijaribu kwenda hospitali kutazama tatizo. Akapewa dawa lukuki lakini wapi! Hazikumsaidia hata kidogo. Mwishowe akaamua kurudi tu nyumbani kwani maisha ya hosteli yamemshinda, lakini kabla hajaondoka, rafiki yake aitwaye pili akamkabidhi mdoli kama zawadi, "utakuwa unanikumbuka ukiuona mdoli huu." Na kwasababu Oliva na Pili walikuwa ni marafiki sana, basi hakuwa na hiyana kwenda nao.
.
.
Akauweka kitandani na maisha yakaendelea, ila Wiki ya pili, Oliva akarudiwa na hali yake ya kuumwa kichwa! Aliumwa sana mpaka sasa akawa hawezi kwenda shule tena. Damu zilikuwa zikimchuruza puani na kuhisi maumivu makali mno.
.
.
Hakuweza kufanya mtihani.
.
.
Na ikawa hivyohivyo mpaka pale alipokuja kugundua shida ni nini. Shida ulikuwa mdoli aliompa Pili, rafiki yake. Lakini mpaka kufikia huko alikuwa tayari ameshapitia mengi sana. Ameshajibamiza na kujiumiza. Ameshakorofishana na karibia kila mtu! Ameshajichakaza uso na kuwa mtu asiyeeleweka.
.
.
Maneno yake ya mwisho kwa jamaa yangu yalikuwa haya, "Midoli ina roho, Tony."
Read more
Padri Alfonso akatulia kidogo kisha akamuuliza, “Una maanisha Kecie?” . . “Ndio. Nilimuua ...
Media Removed
Padri Alfonso akatulia kidogo kisha akamuuliza, “Una maanisha Kecie?” . . “Ndio. Nilimuua Kecie,” akajibu Mrs Garett akitazama chini na macho yake mekundu. . . “Kwanini ulimuua?” Akauliza Padri. . . “Ni simulizi pana kidogo,” akasema Mrs Garett. Akajipangusa machozi  kisha ... Padri Alfonso akatulia kidogo kisha akamuuliza, “Una maanisha Kecie?”
.
.
“Ndio. Nilimuua Kecie,” akajibu Mrs Garett akitazama chini na macho yake mekundu. .
.
“Kwanini ulimuua?” Akauliza Padri.
.
.
“Ni simulizi pana kidogo,” akasema Mrs Garett. Akajipangusa machozi  kisha akaendelea kuongea …
.
.
Miaka kumi na mbili iliyopita …
.
.
Ulikuwa ni mchana wa saa saba wakati mume wangu aliporejea nyumbani toka kazini. Anafanya kazi kwenye kiwanda hivyo nilistaajabu kwake kuwahi kurudi siku hiyo tofauti na ilivyo kawaida yake. Alikuwa amenuna sana kiasi cha kuogopa hata kuongea naye, ila baadae alipotulia akaniambia nini kinamtatiza.
.
.
Hakuwa anamtaka Kecie pale nyumbani. Nilishangazwa sana na neno lake hilo. Sikuona mahusiano ya yeye kurudi kazini mapema na uwepo wa Kecie. .
.
Akiwa amefura kwa hasira, akanambia kuwa Kecie ni gundu kubwa ndani ya nyumba. Amekuwa ni mtoto wa mikosi na laana. Amekuwa ni mtoto anayemsababishia matatizo sana kazini kwake.
.
.
Nilibaki naduwaa. Nilitaka kujua ni kwanini anasema hivyo lakini hakuniambia abadani. Kitu pekee alichoniambia ni kwamba amefukuzwa kazi. Aliponiambia hivyo akaenda zake ndani, na tangu hapo hatukuwa na mahusiano mazuri baina yangu na yeye.
.
.
Basi siku zikapita. Mahusiano baina yake na Kecie yakawa mabaya sana sana. Hakuwa anataka kumwona kabisa. Na muda mwingine angempiga nusura kumuua. Alikuwa na chuki kubwa sana juu yake. .
.
Na kwakuwa hakuwa na kazi, tukawa tunaishi kwenye umasikini mkubwa sana. Nakumbuka siku nne zilipita tukiwa hatuna kitu mfukoni, tukiomba tu kwa majirani. Mume alikuwa anatafuta kazi, akizunguka huko viwandani na hata kuomba vibarua, akawa hapati ata cha ndani ya masaa.
.
Read more
Loading...