Loading Content...

Prince_anaclet2014 Instagram Photos and Videos

Loading...


prince_anaclet2014 Prince Anaclet II @prince_anaclet2014 mentions
Followers: 6,398
Following: 5,899
Total Comments: 0
Total Likes: 0

. KWA WOTE AMBAO MLIKUWA KWENYE MAHUSIANO HALAFU GHAFLA YULE ULIYEMPENDA AKAKUACHA BILA SABABU ...
Media Removed
. KWA WOTE AMBAO MLIKUWA KWENYE MAHUSIANO HALAFU GHAFLA YULE ULIYEMPENDA AKAKUACHA BILA SABABU YA MAANA: Usimlilie, wala usiuumize moyo wako kwa ajili yake. Usijipe PRESHA bure kwa ajili yake. Huyo aliyekuacha hakuwa mtu sahihi. Mungu amekusaidia kumdhihirisha mapema kwamba alikuwa ... .
KWA WOTE AMBAO MLIKUWA KWENYE MAHUSIANO HALAFU GHAFLA YULE ULIYEMPENDA AKAKUACHA BILA SABABU YA MAANA:
Usimlilie, wala usiuumize moyo wako kwa ajili yake. Usijipe PRESHA bure kwa ajili yake. Huyo aliyekuacha hakuwa mtu sahihi. Mungu amekusaidia kumdhihirisha mapema kwamba alikuwa MBWA MWITU kwenye NGOZI YA KONDOO. Mshukuru sana Mungu, amekuondolea KICHOMI. Ebu fikiri, vipi kama angeendelea kuficha makucha yake, ukaingia naye kwenye ndoa halafu ndo akakugeuka na kudai kukupa talaka? Ingekuwa FEDHEHA kubwa. After all, wako wanawake/ wanaume wacha Mungu kibao ambao kila siku wanakata rufaa kwa Mungu ili wawe na wewe na wako serious, wamemaanisha kuutunza MOYO WAKO. Using'ang'anie VIMEO wakati ORIGINAL wapo! Anza kumpa Mungu utukufu maana anakupenda na amekuepusha na hilo JANGA KUBWA NA ZITO. Huyo mkaka/ mdada alitoka kwako lakini hakuwa wa kwako, Maana kama angalikuwa wa kwako angalikaa pamoja nawe. Lakini ameondoka ili afunuliwe kwamba si wako.
Read more
Loading...
. BARUA YA WAZI KWENU AKINA DADA; Dear Ledizi, tunawaombeni muwe specific. Kama Boyfriend wako ...
Media Removed
. BARUA YA WAZI KWENU AKINA DADA; Dear Ledizi, tunawaombeni muwe specific. Kama Boyfriend wako alikuwa akikucheat na akakuacha usiseme, "Wanaume wote ni mbwa tu". Huyo Boyfriend wako siyo " #wanaume_wote". Wanaume wote siyo yeye. Mdeskraibu huyo jamaa kwa jina lake, utaje anuani ... .
BARUA YA WAZI KWENU AKINA DADA;
Dear Ledizi, tunawaombeni muwe specific. Kama Boyfriend wako alikuwa akikucheat na akakuacha usiseme, "Wanaume wote ni mbwa tu".
Huyo Boyfriend wako siyo " #wanaume_wote". Wanaume wote siyo yeye. Mdeskraibu huyo jamaa kwa jina lake, utaje anuani yake na namba yake ya simu halafu ndio umuite ni mbwa.
Kwamba, 'Lusajo Mwakapulilo wa Buguruni kwa Mnyamani, nyumba namba XX, namba ya simu 071XXXXXXX, wewe ni Mbwa tu."
Kuweni specific ledizi. Hao wapuuzi wachache msifananishe na wanaume wote. Waacheni wanaume wasio na hatia out of this.
Halafu pili, Jisemee hivi, "Mimi Pretty Doreen wa Kigamboni, nyumba namba XX, simu namba 067XXXXXXX, nilikuwa na-date na mbwa.
Kimsingi ndio hivyo.

Wenu; Anayechukizwa na maneno ya waja.
.
#Watu_Wangu_Wa_Mwanza_Nakuja_Kwenu
Read more
NAOMBA NISEME KITU KIMOJA LEO. MNIVUMILIE LAKINI NAWASAIDIA. MAANA MMEZIDI. Kuna hii tabia mumeo/ ...
Media Removed
NAOMBA NISEME KITU KIMOJA LEO. MNIVUMILIE LAKINI NAWASAIDIA. MAANA MMEZIDI. Kuna hii tabia mumeo/ mpenzi anakuambia mpenzi twende out for dinner. Sasa Wewe Mwanamke sijui unakuwa na shida gani. Ukiambiwa dinner maana yake ni utoke sexy, Uvae nguo fulani hivi za kukufanya mwepesi, ... NAOMBA NISEME KITU KIMOJA LEO. MNIVUMILIE LAKINI NAWASAIDIA. MAANA MMEZIDI.
Kuna hii tabia mumeo/ mpenzi anakuambia mpenzi twende out for dinner.
Sasa Wewe Mwanamke sijui unakuwa na shida gani.
Ukiambiwa dinner maana yake ni utoke sexy, Uvae nguo fulani hivi za kukufanya mwepesi, Uvutie.
Maana raha ya Dinner ukirudi home una raha zote, mkifika tu home mnafanya finishing.
Sasa wewe sijui Mwalimu wako nani?
Unaambiwa dinner unaanza kuvaa mjitenge wako wenye stifu kama tausi.
Lemba kubwaa, mara mikono mikubwa kama mwavuli. Limkono la kitenge linaingia kwenye sahani ya chakula.
Wewe; umeambiwa unaenda kwenye mkutano wa Wabunge wa East Africa ama?
UNAINGIA HOTELINI WATU WOTE WANAKUSHANGAA NA MTENGE WAKO KAMA MOVIE YA COMING TO AMERICA.
Mume akinogewa akikugusa mahali anakutana na mstifu mkubwa tena wenye waya, jamaniii.. Duuuh...!!
Akikugusa mgongo anakutana na mjistifu na sponji kubwaa...
Una shida wewe.
Wakipita wake wa wengine unaanza kupata hasira mumeo akigeuka... Unaumia.
Mtoto mdogo wa miaka 27 umevaa mjitenge utafikiri unawakilisha Mashindano ya vitenge Brazil... Kila Vazi na Mahala pake bhana.
Sasa bora basi mtenge tu. Na mjipochi mkubwa.. utafikiri unaenda kuhesabu kura kama Mitomingi... (penzi kitovu cha uzembe)
Hivi hujui dinner ukialikwa ni jambo ambalo liko sexy??
Sasa umealikwa dinner unaanza; ooh naomba tuongee...
Kabla hujaruhusiwa unaanza; "kama kweli unanipenda fungua simu yako". "Nipe password", "Niambie Zulfa ni nani?",
Nataka gari......
Na wewe si umtoe dinner yako ya hizo needs zako.. woiiiiii.
Akipita dada na gauni lake na marashi yake unanuna; unamnunia nani? uliombwa uvae miwaksi yako na mistifu.
MUME ANATAKA KUKUSHIKA KICHWA ETI OOh UTAVURUGA GERE LANGU.
(Yale malemba ya kinaijeria). Dada una shida. Dinner na lemba?
Yale malemba kavae harusini..
Saa ya kucheza muziki ukiambiwa ukacheze na hubby unaona hata aibu kusimama na kitenge chako. (Shona basi hata cha kijanja)
Maana saa ya muziki akishika kiuno akifikie..
NAWAZA MISTIFU YA VITENGE KIUNO ANAKIFIKIA SAA NGAPI. KWELI UNAALIKWA DINNER UNAPASI KITENGE CHA MSHONO WA TAUSI? serious?
Mnajua mnanitani?
Nikikukuta na mtenge wako dinani nakusalimia.
Nakuambia SHIKAMOO. Uache kuitika uone....
Read more
. TUJARIBU HIZI TABIA: . 1. Ukichukua kitu toka mahali fulani kinapotakiwa kukaa jaribu kurudisha ...
Media Removed
. TUJARIBU HIZI TABIA: . 1. Ukichukua kitu toka mahali fulani kinapotakiwa kukaa jaribu kurudisha sehemu ulipokitoa baada ya kutimiza hitaji lako, hata kama ni kitana, kikombe, au dekio kiweke sehemu ulipokitoa. Jizoeze hivi inajenga tabia ya kuwa makini. . 2. Ukikopa pesa rudisha ... .
TUJARIBU HIZI TABIA:
.
1. Ukichukua kitu toka mahali fulani kinapotakiwa kukaa jaribu kurudisha sehemu ulipokitoa baada ya kutimiza hitaji lako, hata kama ni kitana, kikombe, au dekio kiweke sehemu ulipokitoa. Jizoeze hivi inajenga tabia ya kuwa makini.
.
2. Ukikopa pesa rudisha kwa wakati ulioahidi, endapo umekwama kuwa muungwana na ujieleze kwa mhusika kama ulivyojieleza wakati unakopa. Kukaa kimya huku unajua umeahidi kitu mpaka ukumbushwe ni uzwazwa na si ustaarabu.
.
3. Ukiazima kitu kama kitabu, kiatu etc. kitunze na ukirudishe katika hali ile ile kama kilivyokuwa wakati unapewa. Kirudishe mara umalizapo hitaji lako, kujisahaulisha ni tabia ya ovyo sana rafiki unamkwaza mwenye mali hata kama mmezoeana vipi.
.
4. Usichukue kitu cha mtu bila kuomba hata kama mna ukaribu wa bega na kidevu, omba, toa taarifa hata kama ni peni mezani, jizoeze hivyo ni rahisi na inapendeza! Huu ndiyo uungwana ndugu.
.
5. Usinunie watu bila kuwaambia walipokukwaza ukitarajia wataona yaliyokununisha, kwanza unaonekana kituko, pili unajinyima raha ya maisha na tatu, unaweza kuwa unamnunia mtu kimakosa.
.
6. Unapotoa ahadi ya kukutana na mtu, hakikisha unamjulisha mhusika endapo utachelewa au hautofika. Fanya hivi mapema na endapo utashindwa kutoa taarifa, hakikisha baadaye unamjulisha mhusika sababu za kutotimiza ahadi, au kutotokea.
.
7. Ukitumwa kitu na chenji ikabaki, rudisha kwa mhusika. 😂😂😂😂 kubania chenji si tabia nzuri hujui bajeti ya mtu aliyekutuma.
.
8. Unaposemeshwa na mtu weka simu pembeni umsikilize, kujifanya unamsikiliza huku mikono na macho viko busy na simu. NI DHARAU, ni bora umuombe asubiri umalizane na simu kisha umsikilize kiuungwana.
.
9. Unapokuwa kwenye mazungumzo na simu ikaita. Omba radhi hata kwa ishara, ama mjulishe mhusika kuwa unapokea simu, ni kitu kidogo sana lakini chenye maana kubwa kuwa unamjali mzungumzaji/msikilizaji wako.
.
10. Usiwe unalala/ unakula/ unatoka kitandani bila kusali/kuswali.
.
PAMBANA NA TABIA ZAKO 😂😂😂😂
Read more
. 《《NAKUHAKIKISHIA》》 <span class="emoji emoji1f469"></span>🏻‍<span class="emoji emoji1f4bb"></span>- "Ukitaka kukosa furaha katika mahusiano yako, kuwa na tabia ya kuangalia ...
Media Removed
. 《《NAKUHAKIKISHIA》》 🏻‍- "Ukitaka kukosa furaha katika mahusiano yako, kuwa na tabia ya kuangalia angalia simu ya mwenzako. . 🏻‍- Nakupa guarantee bila doubt yoyote ile hata kama huyo mwenzako anayo tiketi ya kwenda Mbinguni, #lazima_utaona_tu_jambo_ambalo_huyo_mwenzako_atashindwa_kulieleza ... .
《《NAKUHAKIKISHIA》》
👩🏻‍💻- "Ukitaka kukosa furaha katika mahusiano yako, kuwa na tabia ya kuangalia angalia simu ya mwenzako.
.
👩🏻‍💻- Nakupa guarantee bila doubt yoyote ile hata kama huyo mwenzako anayo tiketi ya kwenda Mbinguni, #lazima_utaona_tu_jambo_ambalo_huyo_mwenzako_atashindwa_kulieleza na hatimaye kuleta matatizo.
.
👩🏻‍💻- Siyo kwamba anakusaliti, hapana, bali hajui ni namna gani aeleze ieleweke na ukamuelewa. Kama unajua hutaweza kuachana naye usitizame simu yake!" .
.
🤒- Kama huna mpango wa kumuacha usimwekee mitego; maana mafanikio ya mtego wako ni mwiba na mkuki wa maisha yako katika mapenzi yenu..
Read more
. ASILIMIA KUBWA YA WACHEPUKAJI WENGI WANA TABIA HIZI: 1. Hachezi mbali na simu yake kila wakati. 2. ...
Media Removed
. ASILIMIA KUBWA YA WACHEPUKAJI WENGI WANA TABIA HIZI: 1. Hachezi mbali na simu yake kila wakati. 2. Inbox na sending items hufutwa kila wakati. 3. Ukimuomba simu yake ghafla lazima akwambie ebu kwanza ili ajiwekee mazingira ya usalama. 4. Kamwe haiiti always anaweka vibration. 5. ... .
ASILIMIA KUBWA YA WACHEPUKAJI WENGI WANA TABIA HIZI:
1. Hachezi mbali na simu yake kila wakati.
2. Inbox na sending items hufutwa kila wakati.
3. Ukimuomba simu yake ghafla lazima akwambie ebu kwanza ili ajiwekee mazingira ya usalama.
4. Kamwe haiiti always anaweka vibration.
5. Namba nyingi ha save na hata akisave inakuwa na majina tofauti.
6. Kuna simu hapokei hata iweje, anapenda sms zaidi.
7. Majina mengi kwenye simu yameseviwa kwa majina ya kufikirika.
8. Muda mwingi ni mtu wakujihami.
9. Anapenda password na anabadili mara kwa mara.
10. Akiazima simu yako, akitumia tu anafuta namba zake haraka sana ili usizikariri.
11. Always yuko na simu hadi bafuni ikibidi.
12. Ana jazba ukimuuliza chochote kuhusu simu, anajishtukia.
13. Akiwa anachati anakuangalia mara kwa mara kiwiziwizi.
14. Hana jeuri ya kukuweka profile picture na akikuweka humalizi Lisaa anakudampu huko tena anaweka status napenda sana Ndugu zangu..
.
Niwatakieni USIKU mwema.
.
NB: Picha_Haihusiani_Na_Mada_Iliyotajwa.
Read more
Loading...
. #EWE_MWANAMKE_SIKIA: . SIFA ya Mwanamke ni kujitunza na kuutunza MWILI WAKE. MWANAMKE anayeuthamini ...
Media Removed
. #EWE_MWANAMKE_SIKIA: . SIFA ya Mwanamke ni kujitunza na kuutunza MWILI WAKE. MWANAMKE anayeuthamini mwili wake na kuupenda kamwe huwezi kumuona anakuwa kwenye mahusiano na mwanaume zaidi ya mmoja kwasababu lazima awe na kinyaa. Ukikuta mwanamke ana mahusiano na mwanaume zaidi ... .
#EWE_MWANAMKE_SIKIA:
.
SIFA ya Mwanamke ni kujitunza na kuutunza MWILI WAKE.
MWANAMKE anayeuthamini mwili wake na kuupenda kamwe huwezi kumuona anakuwa kwenye mahusiano na mwanaume zaidi ya mmoja kwasababu lazima awe na kinyaa.
Ukikuta mwanamke ana mahusiano na mwanaume zaidi ya mmoja basi huyo siyo mwanamke anayejitunza na kujiheshimu...
.
#Wale_Wa_Kudanga_Mpo??
Read more
. Mtu ambaye anakupenda kwa dhati, hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi ...
Media Removed
. Mtu ambaye anakupenda kwa dhati, hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, maana wewe ndiye furaha yake..... .
Mtu ambaye anakupenda kwa dhati, hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, maana wewe ndiye furaha yake.....
Loading...
. #SIKIA: Pamoja na ukweli kwamba, siku zote UKWELI humweka mtu huru, lakini kuna ukweli mwingine ...
Media Removed
. #SIKIA: Pamoja na ukweli kwamba, siku zote UKWELI humweka mtu huru, lakini kuna ukweli mwingine unatesa, unauma, unaumiza na kama haitoshi unakera. Hivi ni kwanini ubaki na siri ndani ya MOYO wako kwamba, huna malengo yoyote na uliyenaye kwenye MAHUSIANO, ilhali unajua fika ipo siku ... .
#SIKIA:
Pamoja na ukweli kwamba, siku zote UKWELI humweka mtu huru, lakini kuna ukweli mwingine unatesa, unauma, unaumiza na kama haitoshi unakera.
Hivi ni kwanini ubaki na siri ndani ya MOYO wako kwamba, huna malengo yoyote na uliyenaye kwenye MAHUSIANO, ilhali unajua fika ipo siku siri hiyo itadhihirika wazi kwa mlengwa na atakayeumia zaidi ni yeye na si wewe?
Guys, hakuna kitu kinatesa wengi kwenye MAHUSIANO kama kupotezewa muda.
.
#Picha_Haihusiani_Na_Maelezo
Read more
PAMBANA! . <span class="emoji emoji26ab"></span>Wanafalsafa wanasema "ujinga hauondoki kwa kumchukia mwenye akili, umaskini hauondoki ...
Media Removed
PAMBANA! . Wanafalsafa wanasema "ujinga hauondoki kwa kumchukia mwenye akili, umaskini hauondoki kwa kumchukia tajiri na kuhesabu dhambi za wenzako hakukufanyi kuwa mtakatifu". . Nakuambia kweli kumsema mtu, kumkashfu na kumponda kwa lengo la kumwaribia jina hakuwezi kukupa ... PAMBANA!
.
⚫Wanafalsafa wanasema "ujinga hauondoki kwa kumchukia mwenye akili, umaskini hauondoki kwa kumchukia tajiri na kuhesabu dhambi za wenzako hakukufanyi kuwa mtakatifu".
.
⚫Nakuambia kweli kumsema mtu, kumkashfu na kumponda kwa lengo la kumwaribia jina hakuwezi kukupa mafanikio. Kupata mafanikio kwa kumsema mwingine ni sawa na kusubiri mimba ya shoga (it's impossible).
.
⚫Mara nyingine chuki dhidi ya mtu inaweza kujijenga kwenye moyo wako bila ya wewe kutaka; ila nakushauri jaribu kuilazimisha nafsi kumpenda. Tambua hata jogoo akizeeka sana anataga.
.
⚫Jaribu kuacha unafiki, tambua hakuna faida wala malipo ya mnafiki zaidi ya jihanam ya moto. "ni heri kupigwa na mwenye hekima gizani kuliko kusifiwa na mpumbavu hadharani". Acha upumbavu.
.
⚫Kama ulitegemea kufanikiwa kwa kumsema vibaya mwenzako BADILISHA FORMULA, acha kusema watu, tumia akili yako kukufanikisha, weka mipango mizuri kwa kile ulicho fikiria, weka imani mtangulize Mungu alafu fanya na utafanikiwa.
.
▪Nilishawahi kuambiwa; "watu wanaosema wengine vibaya kwenye jamii siyo kwamba wanawachukia! Hapana!, bali uchukia mafanikio yao". Nataka nikuambie kweli Ukiona wanakuchafua tambua wanakuchafua kwasababu una kitu ambacho wao hawana. Usikate tamaa PAMBANA.
.
▪Mara nyingine unaweza kukata tamaa kwasababu watu wanakusema sana,ila mimi nakuambia kweli ukikata tamaa kwasababu ya kusemwa na watu unastahili hukumu ya moto. Acha mikato ya tamaa PAMBANA.
Read more
. Wakati mwingine tusilalamike sana; Ndo wanavyosemaga......... Wahenga walisema; "Ukiona ...
Media Removed
. Wakati mwingine tusilalamike sana; Ndo wanavyosemaga......... Wahenga walisema; "Ukiona Manyoya Ujue Kashaliwa".. . #ukweli_unauma_lakini_upokee .
Wakati mwingine tusilalamike sana; Ndo wanavyosemaga.........
Wahenga walisema; "Ukiona Manyoya Ujue Kashaliwa"..
.
#ukweli_unauma_lakini_upokee
. Kabla hujamuamini Mwanaume kwa maneno yake matamu na ahadi nyingi kuliko Ilani ya CCM mwaka 2020 ...
Media Removed
. Kabla hujamuamini Mwanaume kwa maneno yake matamu na ahadi nyingi kuliko Ilani ya CCM mwaka 2020 itakavyokuwa kabla ya Uchaguzi; FANYA MAMBO HAYA MAWILI: 1. Jiulize ni mara ya ngapi unaambiwa maneno hayo hayo matamu na ukawa excited hivi hivi na wanaishia tu kukuvua nonihino na kuondoka ... .
Kabla hujamuamini Mwanaume kwa maneno yake matamu na ahadi nyingi kuliko Ilani ya CCM mwaka 2020 itakavyokuwa kabla ya Uchaguzi;
FANYA MAMBO HAYA MAWILI:
1. Jiulize ni mara ya ngapi unaambiwa maneno hayo hayo matamu na ukawa excited hivi hivi na wanaishia tu kukuvua nonihino na kuondoka bila kutekeleza walichoahidi AU kutekeleza kwa muda mfupi tu wakiwa wanakulia timing uchanue waweke muhuri halafu basi?
.
2. Muulize hayo maneno matamu anayokwambia yanatoka moyoni au kwenye Ncha ya Zipu yake ya Suruali?
Wanaume tuna Uongo ule ule, Maneno yale yale, Style zile zile miaka 800 lakini bado na wewe unadanganywa kwa Style zile zile na unaishia kulia machozi kwa vitu vile vile.
Tumechoka kusikia Stori zile zile, Danganywa kwa vitu vipya. "Oh Aliniahidi kunioa kanipa Mimba kaikataa". Nakuwamba na Vibao kabisa; Stori kanipa Bibi yangu na wewe unaitumia? WAKE UP GIRLS; Usiwe na moyo wa Ajuza wakati una miaka 24.
Read more
Loading...
 #MBU: Mbu ni kiumbe kidunchu, chembambaaaa, Ila kinatambua uwezo wake. Binadamu huwa wamwonapo ...
Media Removed
#MBU: Mbu ni kiumbe kidunchu, chembambaaaa, Ila kinatambua uwezo wake. Binadamu huwa wamwonapo mbu humdharau. Ila wakipata maradhi wanajua Mbu kawatenda pamoja na udogo wake. Unaweza kudharaulika kwa kuwa hujawahi kumwonesha anayekudharau uwezo wako. Tatizo wengi wetu tunadhani ... #MBU:
Mbu ni kiumbe kidunchu, chembambaaaa, Ila kinatambua uwezo wake. Binadamu huwa wamwonapo mbu humdharau. Ila wakipata maradhi wanajua Mbu kawatenda pamoja na udogo wake. Unaweza kudharaulika kwa kuwa hujawahi kumwonesha anayekudharau uwezo wako. Tatizo wengi wetu tunadhani uwezo wetu utaonekana tukifanya mambo mazito kama kunyanyua Gari; La hasha. Jiulize Mbu amewahi kuua wangapi kimya kimya?
Usiku mmoja unatosha sana Mbu kufanya mtaa mzima uwe na misiba kadhaa. Sisi tunashindwa nini kumchapa mwenyekiti wa mtaa anayejiviringisha kwenye mtaa wetu kama vile kaununua?
Hivi kweli tunaweza kuzidiwa kete na Mbu? Yaani Mbu ambaye kofi moja linapelekea umauti wake, kofi ambalo hata ukimpiga nalo mtoto wa mwaka mmoja halii. Anatushindaje?
Mbu bwana; na udogo wake ule ila ana kelele huyo, na ana ujasiri wa ajabu. Mvua, jua, kiangazi, masika. Mbu hajawahi kushindwa; Weka neti, puliza dawa akikuotea usiku mmoja; Unalazwa hospitalini wiki nzima.
**TAFAKARI**
Nini kinakushinda katika BIASHARA, katika MASOMO yako, katika KAZI, katika NDOA, katika IMANI, katika MAISHA, katika TABIA. Nini?
TUNAWEZA KUPAMBANA NA HALI YETU
Wahenga walisema, mtembea bure si sawa na mkaa bure. Unaweza kuokota hata 50/=
Read more
 #SIKIA: Mtu anapokufanya wewe kama wa akiba, msaidie kupunguza akiba yake kwa kumuondoa kwenye ...
Media Removed
#SIKIA: Mtu anapokufanya wewe kama wa akiba, msaidie kupunguza akiba yake kwa kumuondoa kwenye maisha yako. . Muda mwingine wewe nawe lazima uwe na ujasiri wa kuonyesha kuwa haujali, bila ya kuangalia ni kwa kiasi gani unajali! . Kwa sababu inatokea muda mwingine mtu anakuona huna ... #SIKIA:
Mtu anapokufanya wewe kama wa akiba, msaidie kupunguza akiba yake kwa kumuondoa kwenye maisha yako.
.
Muda mwingine wewe nawe lazima uwe na ujasiri wa kuonyesha kuwa haujali, bila ya kuangalia ni kwa kiasi gani unajali!
.
Kwa sababu inatokea muda mwingine mtu anakuona huna lolote wakati wewe unamuona ni kila kitu kwako!
.
Kufanya hivyo siyo kwamba unajisikia au unaringa, Hapana. bali ni kwamba unajiheshimu na zaidi unarudisha hadhi, thamani na utu wako!
.
Usitarajie kuona mabadiliko yoyote chanya katika maisha kama bado umezungukwa na watu wenye mawazo hasi juu yako na wasioongeza thamani katika maisha yako!!
.
Usiwape nafasi watu wa muda mfupi katika maisha yako. Fahamu thamani uliyonayo, na usikubali kupokea kidogo au kutopokea kabisa wakati unastahili kupokea vikubwa...
.
#Nawasilisha
Read more
 #Kwenu_Akina_Dada Kabla ya kubeba mimba ya mume wa mtu jua kuwa; Hata mkewe alikuwa anampenda ...
Media Removed
#Kwenu_Akina_Dada Kabla ya kubeba mimba ya mume wa mtu jua kuwa; Hata mkewe alikuwa anampenda kama wewe; Usidhani kama alimuoa mkewe akiwa anamchukia, alikuwa anampenda na kumuonyesha mapenzi kabla ya kumuoa na kumzalisha na sasa kamtelekeza. Najua unajihisi spesho lakini ukweli ... #Kwenu_Akina_Dada
Kabla ya kubeba mimba ya mume wa mtu jua kuwa; Hata mkewe alikuwa anampenda kama wewe; Usidhani kama alimuoa mkewe akiwa anamchukia, alikuwa anampenda na kumuonyesha mapenzi kabla ya kumuoa na kumzalisha na sasa kamtelekeza. Najua unajihisi spesho lakini ukweli ni kuwa wewe si spesho; mko wengi kama yeye na hata mkewe alikuwa hivyo hivyo. Sasa ukishamzalia na wewe utakuwa kama mkewe tu; kuwa si mchepuko tena binti bali Mama watoto wake!
.
Najua unajihisi uko spesho na nina uhakika kwa mambo aliyokuambia ushajisemea “Mkewe ana matatizo!” Ila niamini mimi nishasikia hizi stori nyingi, huna uspesho wowote; tena inawezekana wewe una matatizo kuliko mkewe, hivyo usidhani kama ukishazaa na kuanza kuomba matumizi atakuvumilia, hapana atakimbia majukumu na utakuja kulea mwenyewe hivyo ebu jiandae kwa hilo.
.
#Ni_rahisi_kulea_Mchepuko_kuliko_Mchepuko_Na_Mtoto; Sasa hivi mambo anayofanya kwako anaamua, ni starehe na mnafurahia wote ndiyo maana anafanya. Lakini ukilogwa ukabeba mimba tu unaacha kuwa starehe unageuka na kuwa majukumu kama mkewe, kwamba hafanyi tena kwa kuwa anataka bali kwa kuwa ni lazima na unakuwa kero kuomba matumizi kama mkewe!
.
Labda nikupe mfano sasa hivi; kama mchepuko anaamua kukununulia gauni, anaamua kukutoe out na kukupa hela ya saluni. Hivyo kama siku hana basi anaweza kukuambia hana na ukamuelewa. Lakini akishakuja mtoto basi jua kuwa mtoto hawezi kuacha kula, hawezi kuacha kuumwa eti kwa kuwa Baba hana pesa, nakuambia kuwa ukizaa naye utakuwa majukumu sawa na mkewe; watu hukimbia majukumu na si starehe atakukimbia.
Read more
Loading...
 #JIFUNZE: Pale unapotoka kumsaliti mwenza wako kaa chini na kutafakari haya moyoni mwako; "ni ...
Media Removed
#JIFUNZE: Pale unapotoka kumsaliti mwenza wako kaa chini na kutafakari haya moyoni mwako; "ni kweli nimemsaliti mme/mpenzi wangu kwa kuwa hanijali, hanigharamii, hanitimizii, kwa kuwa hanipi hiki na kile?'...'ni kweli nimemsaliti mke/mpenzi wangu kwa kuwa hana wowowo, kwa kuwa ... #JIFUNZE:
Pale unapotoka kumsaliti mwenza wako kaa chini na kutafakari haya moyoni mwako; "ni kweli nimemsaliti mme/mpenzi wangu kwa kuwa hanijali, hanigharamii, hanitimizii, kwa kuwa hanipi hiki na kile?'...'ni kweli nimemsaliti mke/mpenzi wangu kwa kuwa hana wowowo, kwa kuwa hana sura nzuri, kwa kuwa havutii, kwa kuwa hana hiki na kile ambacho mwanamke mwenye mvuto anatakiwa kuwa navyo, kwa kuwa hajui kupika, kwa kuwa hanijali, kwa kuwa hanitimizii, kwa kuwa ana gubu n.k?'.
.
Endelea kutafakari;
- Je ni kweli kuwa kama mke wangu angekuwa mzuri kama Cleopatra na mtiifu kama Malaika nisingemsaliti?
- Je ni kweli kuwa kama mume wangu angekuwa ananipatia na kunitimizia kila hitaji nisingemsaliti?'
.
Kama majibu yako yatakuwa ni ya kusitasita basi ni wazi kuwa haukuwa na chochote cha kukufanya kusaliti bali ni kukosekana tu kwa upendo wa dhati dhidi ya mwenza wako (simaanishi kwamba kuna sababu zinazokuruhusu wewe kusaliti, no justification for cheating) na hapo utaendelea kusaliti tena na tena, kwa maana 'haujitambui' na pengine ni hulka yako, vinginevyo, utaumia, utajuta, utatubu, utamuomba mwenza wako ajirekebishe kama 'unaamini' yeye ndiye amepelekea wewe kusaliti.
.
Basi, pasipo upendo wa dhati na kujitoa, ndoa na mahusiano yote ni ubatili mtupu, hata upewe dunia utasaliti tu hata uwe na mke mrembo na wa kuvutia kushinda Cleopatra bado utasaliti, tusitumie mapungufu ya wenza wetu kuhalalisha na kuwa kinga ya mabaya...
Read more
. "Having the money to buy it, doesn't mean you can afford it. There is a huge difference between ...
Media Removed
. "Having the money to buy it, doesn't mean you can afford it. There is a huge difference between affordability and resource management". . "Kuwa na fedha na kuwa na uwezo wa kununua kitu fulani ni vitu viwili tofauti. Ipo tofauti kubwa kati ya kuwa na fedha na kuwa na uwezo wa kununua. Usipoelewa ... .
"Having the money to buy it, doesn't mean you can afford it. There is a huge difference between affordability and resource management".
.
"Kuwa na fedha na kuwa na uwezo wa kununua kitu fulani ni vitu viwili tofauti. Ipo tofauti kubwa kati ya kuwa na fedha na kuwa na uwezo wa kununua. Usipoelewa utapata shida sana".
Read more
You make ordinary moments extraordinary. It's an opportunity to let you know how special you are ...
Media Removed
You make ordinary moments extraordinary. It's an opportunity to let you know how special you are to me. **Guys let come together and wish this beautiful girl of mine a Happy Birthday** . #Happy_Birthday_My_Only_One_Rosey @rosekido21 @rosekido21 @rosekido21 You make ordinary moments extraordinary. It's an opportunity to let you know how special you are to me.
**Guys let come together and wish this beautiful girl of mine a Happy Birthday**
.
#Happy_Birthday_My_Only_One_Rosey @rosekido21 @rosekido21 @rosekido21
Loading...
. INAVYOSEMEKANA ETI; Kama kuna Mtu umekosana naye au unachukiana naye hakikisha mnayaweka ...
Media Removed
. INAVYOSEMEKANA ETI; Kama kuna Mtu umekosana naye au unachukiana naye hakikisha mnayaweka mambo yenu sawa kwasababu muda mwingine kuna mambo katika maisha yako hayasongi wala kufanikiwa kwasababu wale ambao una chuki nao au wale ambao umegombana nao ndio wenye msaada mkubwa wa kukusogeza ... .
INAVYOSEMEKANA ETI;
Kama kuna Mtu umekosana naye au unachukiana naye hakikisha mnayaweka mambo yenu sawa kwasababu muda mwingine kuna mambo katika maisha yako hayasongi wala kufanikiwa kwasababu wale ambao una chuki nao au wale ambao umegombana nao ndio wenye msaada mkubwa wa kukusogeza mbele zaidi, kwahiyo unavyochelewesha kupatana nao ndivyo unavyochelewesha mambo yako kufanikiwa na kufika mbali zaidi. Chuki haina maana kama upendo ulivyo na maana katika maisha yako.
.
#Bado_Najifunza
Read more
. #NDUGU_ZANGU_NIACHENI_NILIE: "Huenda nilifanya makosa kukupenda. Lakini ungezihukumu ...
Media Removed
. #NDUGU_ZANGU_NIACHENI_NILIE: "Huenda nilifanya makosa kukupenda. Lakini ungezihukumu hisia zangu na siyo moyo wangu. Mateso ninayopitia, ni zaidi ya yale aliyoyapata Doctor Louis Shika alipotekwa Urusi. Umenisababishia hitilafu kwenye switch iwashayo taa ya furaha ndani ya ... .
#NDUGU_ZANGU_NIACHENI_NILIE: "Huenda nilifanya makosa kukupenda. Lakini ungezihukumu hisia zangu na siyo moyo wangu. Mateso ninayopitia, ni zaidi ya yale aliyoyapata Doctor Louis Shika alipotekwa Urusi. Umenisababishia hitilafu kwenye switch iwashayo taa ya furaha ndani ya nafsi yangu. Ona sasa Moyo wangu unavyoteketea kwenye jekhanamu ya maumivu!!. Na mbaya zaidi sizijui namba za simu za watu wa fire.

Nahisi nimetengwa na kila mtu hadi kivuli changu. Yamkini dunia haijawai kuufurahia uwepo wangu. Na ninapozitazama mbingu naona ni kama zinanizomea. Machozi niliayo leo siyo kiashiria cha kwamba mimi ni mwanaume dhaifu sana. Machozi haya ni mahususi kwa ajili ya kuua na kutoa sumu iliyotapakaa katikati ya kifua changu.

Maumivu ya mapenzi yamefanya ubongo wangu ujenge chuki na sayari iitwayo dunia. Natamani siku zirudi nyuma niitwe mimba ili nijifiche kwenye tumbo la mama yangu. Kwanini umeniacha peke yangu kwenye mochwari iliyobeba wafu wa fikra?! Sina tena ujasiri, afya imeyumba na mwili umedhohofu sana. Nimekata tamaa ya kuibuka na ushindi katika hii vita ya kukusahau. Natembea taratibu peke yangu katikati ya nyika. Ukiniona utalia. Mwili umebaki mifupa mitupu. Hata Simba mwenye njaa hawezi kunidhuru. Natia huruma hadi neno huruma nalo linanionea huruma. Najua kuna siku tutaonana, hilo naomba tambua.

Laiti kama ningepata nafasi ya kusimama juu ya kilele cha safu za mlima mrefu kuliko yote ulimwenguni #Mlima_Everest ningeipaza sauti kuijulisha dunia kiasi gani ~NAKUPENDA.~ Ili hata kama nakuongopea. Mwangwi wa sauti yangu ukasimame kama shahidi siku ya mwisho kwenye kiti cha hukumu."
.
#NajifunzaKuandikaScript #MovieInakuja #KaaTayari
Read more
. #Ukiwa_mtu_mzima_utajua_si_kila_kitu_lazima_ushindane; . Usishindane na EX wako 😇 Ukiwa ...
Media Removed
. #Ukiwa_mtu_mzima_utajua_si_kila_kitu_lazima_ushindane; . Usishindane na EX wako 😇 Ukiwa kwenye mahusiano na mwenzako akaamua kuyakatiza kwa kuwa kapata chombo kipya na hukumkosea! Basi usishindane naye 😇 . Usiingie kwenye mahusiano mapya ili umkomoe, eti usionyeshe kuwa ... .
#Ukiwa_mtu_mzima_utajua_si_kila_kitu_lazima_ushindane;
.
Usishindane na EX wako 😇
Ukiwa kwenye mahusiano na mwenzako akaamua kuyakatiza kwa kuwa kapata chombo kipya na hukumkosea! Basi usishindane naye 😇
.
Usiingie kwenye mahusiano mapya ili umkomoe, eti usionyeshe kuwa unaumia, maumivu ni maumivu tu hayaishi kwa kuigiza! Mwache afurahie kitu kipya na wewe pambana kuponya moyo kwanza ili uwe na uhakika wa usalama pale utakapokanyaga 😇
.
Trust me ni vema hata asijue mambo yako yanaendaje! Mwache atumie kitu kipya kikianza kuchoka ndipo atakapotambua hakukuwa hata na haja ya kukimbilia mbele wakati usafiri umeuacha nyuma.
.
Kwa wakati huo hatoona maana penzi jipya ni tamu unasahau kila kitu mpaka condom, muda atakaopoteza kwenye penzi jipya na wewe huku utazidi kusahau maumivu na huenda utakuwa umepata mtu sahihi, hii inaitwa "kumpiga adui kwenye mchezo wake mwenyewe" na hapa ndipo atakapogundua alianzisha mchezo na kujiweka starring ila hakujua mwisho wake starring anaweza kufa😂 wengi hawasemagi ila ukweli majuto huwa wanayo hata kama wakioa au kuolewa, utakuwa kama mwangwi mioyoni mwao.
.
NB: Kama nakuchosha na mambo ya mapenzi na mahusiano! Usijichoshe kusoma maana ndiyo nimechagua huku badala ya mambo ya "HOW TO BE RICH" hii yote ni kwa kuwa sina pesa hivyo nitakuwa nawamezesha uongo tu labda mkienda kwa akina Mengi, Bakhresa mnaweza jifunza mambo ya pesa.
.
#Kwa_hisani_ya_watu_wa_Nanjilinji
Read more
*NAOMBA DAKIKA YAKO MOJA TU* . PUNGUZA: Ukitaka kuachana na nzi tupa kwanza mzoga ulionao, Namaanisha ...
Media Removed
*NAOMBA DAKIKA YAKO MOJA TU* . PUNGUZA: Ukitaka kuachana na nzi tupa kwanza mzoga ulionao, Namaanisha Ukitaka mafanikio punguza kwanza marafiki hewa, wanafiki na watu wasio na maana kwenye maisha yako. . KUMBUKA: Usaliti siyo bahati mbaya, ni makusudi. Kumpa nafasi ya pili msaliti ... *NAOMBA DAKIKA YAKO MOJA TU*
.
PUNGUZA: Ukitaka kuachana na nzi tupa kwanza mzoga ulionao, Namaanisha Ukitaka mafanikio punguza kwanza marafiki hewa, wanafiki na watu wasio na maana kwenye maisha yako.
.
KUMBUKA: Usaliti siyo bahati mbaya, ni makusudi. Kumpa nafasi ya pili msaliti ni kujitesa mwenyewe.
.
NAKUAMBIA KWELI: Ukihisi wanakusema ujue ujiamini ila ukiona wanakusema ujue una akili.
.
NAKUSISITIZA: Mheshimu mjinga uokoe muda na kuepukana na balaa.
.
NAONGEA NA VIJANA WENZANGU: Acha akili za kicheche kila saa wewe kufikiria mapenzi tu, Think deeper fanya mambo yenye malengo kwenye maisha yako.
.
NAONGEA NA WADADA: Facebook siyo dampo la kupost picha zako zisizo na maana, uheshimu na kuusitiri mwili wako, wanaume tunataka mtu anayejiheshimu siyo mtu anayetupa presha mitandaoni (mithali 31-30).
.
UTAFANIKIWA: Acha ujuaji (much know) hakuna anayejua kila kitu hapa duniani, sikiliza ushauri ufanikiwe.
.
SIKILIZA MAMA YANGU: Familia haijengwi kwa umbea wa mtaani, shirikiana na mumeo utaijenga familia imara.
.
SIKILIZA KAKA YANGU: Mke mzuri atafutwi messanger, instagram wala kwenye group la whatsapp, mke mzuri anapatikana kwa kumshirikisha Mungu siyo kwa matamanio ya macho.
.
ACHA DHARAU: Kufika mbili kunahitaji kuanza moja, stage after stage, kamwe huwezi toka stage moja kwenda mwingine kama una chuki, dharau wala kujiona daima utabaki mkia tu.
.
NINA UHAKIKA: Hofu na woga ndiyo chanzo cha kurudi nyuma kimaendeleo, punguza hofu.
.
HALIPINGIKI: Kumpenda asiye kupenda ni sawa na kutegemea jasho kwenye ulimi, na kumsahau uliye mpenda ni sawa na kumkumbuka usiyemjua.
.
KIMPANGO WAKO: Ufupi na urefu ni mpango wa Mungu, kama una simu yako kubwa sijui iphone sijui sumsang sijui nini sijui nini bado unategemea like na comment ya TECNO 340 tu hakuna sababu ya kujiona mkwasi sana.
"Dawa ya mnafiki ni kuwa mnafiki zaidi yake"
.
NAKUKUMBUSHA TU BEST: Mithali:6.32
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 
___________**________**__________
NAKUHESHIMU NA NINAKUPENDA NO MATTER HOW YOU ARE.
Read more
KUMBUKUMBU YA KIFO YA MAREHEMU BABA YETU MPENDWA NGOYI LUYA NESTOR: Ni miaka mitatu imepita tokea ...
Media Removed
KUMBUKUMBU YA KIFO YA MAREHEMU BABA YETU MPENDWA NGOYI LUYA NESTOR: Ni miaka mitatu imepita tokea ulipotuacha. Tokea ulipotoweka hakuna siku inayopita ambapo haupo katika mioyo na akili zetu. Enzi za uzima wako matendo yako yaligusa mioyo mingi kwa namna ya kipekee ambayo wewe tu uliweza.  Roho ... KUMBUKUMBU YA KIFO YA MAREHEMU BABA YETU MPENDWA NGOYI LUYA NESTOR:
Ni miaka mitatu imepita tokea ulipotuacha. Tokea ulipotoweka hakuna siku inayopita ambapo haupo katika mioyo na akili zetu. Enzi za uzima wako matendo yako yaligusa mioyo mingi kwa namna ya kipekee ambayo wewe tu uliweza. 
Roho yako ya huruma bado ipo pamoja nasi na mara kwa mara hugusa mioyo na akili zetu na kutupa sababu ya kutabasamu. Umejitwalia nafasi yako miongoni mwa nyota za mbinguni na shime ung’ae milele. Unakumbukwa sana na kila mtu hapa duniani. Ulitoweka kwa uchungu sana bila  hata ya kutuaga. 
Tunakufikiria sana kimya kimya. Hakuna jicho linaloweza kutushuhudia tukiomboleza, ila machozi mengi yanatiririka ndani kwa ndani. Tunafarijika kwa kutambua kuwa ipo siku tutakutana na wewe tena. Unakumbukwa sana na mkeo, watoto wako, wakwe zako na wajukuu zako.
"RAHA YA MILELE UMPE EEH BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI.. AMINA"
Read more
. #NAONGEA_NA_WEWE; 🔀Kama unajijua umeolewa, umeoa, au upo kwenye mahusiano basi jitahidi ...
Media Removed
. #NAONGEA_NA_WEWE; 🔀Kama unajijua umeolewa, umeoa, au upo kwenye mahusiano basi jitahidi uonekane upo hivyo. : 🔀Kama upo kwenye ndoa basi act kama upo kwenye ndoa na kama unajua umeshachukuliwa basi onekana kweli kama umechukuliwa. : 🔀Siyo umeolewa au umeoa halafu unajifanya ... .
#NAONGEA_NA_WEWE;
🔀Kama unajijua umeolewa, umeoa, au upo kwenye mahusiano basi jitahidi uonekane upo hivyo.
:
🔀Kama upo kwenye ndoa basi act kama upo kwenye ndoa na kama unajua umeshachukuliwa basi onekana kweli kama umechukuliwa.
:
🔀Siyo umeolewa au umeoa halafu unajifanya upo single. Au upo kwenye mahusiano halafu unajifanya upo single.
:
🔀Watu walio single hawana muda na "watu walioko kwenye ndoa" au "waliopo kwenye mahusiano".
:
🔀Kama hauna furaha kwenye ndoa yako, ndio hivyo, ulishafanya maamuzi, sasa tafuta namna ya ku-deal nayo. Aidha nenda kwa wataalamu wa councelling na psychology au kutana na kiongozi wako wa dini na mwombe sana Mungu.
:
🔀Kama hauna furaha na mahusiano yako, hujachelewa sana. Unaweza kuyavunja kama hayana tija kabla hujaingia kwenye ndoa. Lakini kabla ya hapo usianze kujibebisha kwa watu walioko single ukijidai na wewe upo single kumbe upo kwenye mahusiano.
:
🔀Watu 'walio' single wana issues zao tofauti na nyie. Aidha wanangoja Mungu awape wale walio sahihi, wana-run careers na biashara zao na wanajenga maisha yao ya kiroho. Huwa hawana muda na wanaume au wake za watu!
:
🔀Sifahamu kwa watu wengine, ila kwa wale singles wanaojielewa hawana muda na watu ambao wako TAKEN, hivyo kama unajua "you are TAKEN", then act TAKEN.
:
🔀Acha wenye ndoa waonekane kama wanandoa,
:
🔀Acha waliokuwa 'taken' waonekane kama 'taken',
:
🔀And let single people act single,
:
Pambana na hali yako. Kila mwenye sikio na asikie, this is 2018 mwaka unaogawanyika kwa 2.
Read more
. AINA TATU ZA MARAFIKI: 1) Marafiki ambao wapo kwa ajili yako na si kwa ajili ya kitu fulani; - ...
Media Removed
. AINA TATU ZA MARAFIKI: 1) Marafiki ambao wapo kwa ajili yako na si kwa ajili ya kitu fulani; - Hawa ni ambao unaweza kuzungumza nao, kuwaamini, umekuwa nao na wapo wazi sana kwako, ni watu ambao hutakiwi kujibadilisha baadhi ya tabia pindi utakapokuwa, ukikwama wanakwama na wewe, ukilia ... .
AINA TATU ZA MARAFIKI:
1) Marafiki ambao wapo kwa ajili yako na si kwa ajili ya kitu fulani;
- Hawa ni ambao unaweza kuzungumza nao, kuwaamini, umekuwa nao na wapo wazi sana kwako, ni watu ambao hutakiwi kujibadilisha baadhi ya tabia pindi utakapokuwa, ukikwama wanakwama na wewe, ukilia wanalia na wewe, kwa kifupi ni ambao hawatokuacha mpaka mwisho.
.
2) Marafiki ambao wapo na wewe sababu ya kitu fulani na si kwa ajili yako;
- Wapo kwa sababu tu unawasaidia kufikia malengo yao, au wanapenda kitu unachofanya, wanajifunza kitu kupitia wewe, wanakutumia kutimiza baadhi ya mipango yao, hivyo hawa wanakuja na kuondoka, hawatokuwa na wewe mpaka mwisho, lipo wazi wakikamilisha malengo yao tu wanaondoka, kitu cha kufurahisha ni kwamba kati ya Rafiki namba moja na namba mbili wote watafanya vitu vilevile, utatoka nao out, mtafurahi pamoja na watafanya vitu vyote anavyotakiwa kukufanyia rafiki.
.
3) Marafiki ambao kwa kifupi siyo marafiki zako bali ni team ambayo ipo na wewe kwa sababu tu wote mnafanya jambo linalofanana au mpo kinyume na jambo moja yaani kama ni kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya n.k, wanachukia kitu ambacho wewe pia unakichukia, kama unamchukia mtu fulani na wao wanamchukia basi watakuwa na wewe kwa sababu hiyo tu, watakusaidia kumshusha huyo MTU, au kupinga kitu ambacho unapinga pia, hivyo unaweza hisi ni marafiki zao, lakini hawa watu wakitimiza lengo tu basi huwaoni tenaa.
.
#Ni_Aina_Gani_Ya_Marafiki_Ulionao??
#Are_They_Helpfully_To_You??
Read more
. TOFAUTI KATI YA MKE NA MCHEPUKO. <span class="emoji emoji1f602"></span> <span class="emoji emoji2747"></span> Mke ni kama TV na Mchepuko ni kama Simu. <span class="emoji emoji21aa"></span> Nyumbani unaangalia ...
Media Removed
. TOFAUTI KATI YA MKE NA MCHEPUKO. Mke ni kama TV na Mchepuko ni kama Simu. Nyumbani unaangalia TV lakini ukitoka unatoka na simu. . Mara chache unafurahia TV lakini muda mrefu unacheza na simu yako. . TV ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia/ kununua vocha hupati ... .
TOFAUTI KATI YA MKE NA MCHEPUKO. 😂 ❇ Mke ni kama TV na Mchepuko ni kama Simu.
↪ Nyumbani unaangalia TV lakini ukitoka unatoka na simu.
.
↪ Mara chache unafurahia TV lakini muda mrefu unacheza na simu yako.
.
↪TV ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia/ kununua vocha hupati huduma.
.
↪TV ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.
.
↪Gharama za huduma za TV ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.
.
↪TV ina remote lakini Simu haina.
.
↪Kitu muhimu zaidi simu ina njia tatu za kuwasiliana unatuma ujumbe, unaongea na unasikiliza lakini TV unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.
.
↪Unaweza kununua TV mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.
.
🔁Ya mwisho na ya kuzingatia🔁
............................................................... 🔀TV haina VIRUSI lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.
Read more
. KUBISHA NI MAAMUZI YAKO ILA UKWELI USEMWA: Mpenzi wako mpya ni Mpenzi wa Mwenzako wa Zamani, ...
Media Removed
. KUBISHA NI MAAMUZI YAKO ILA UKWELI USEMWA: Mpenzi wako mpya ni Mpenzi wa Mwenzako wa Zamani, Usibishe! Yaani ni sawa na Nguo Chakavu ndio Dekio Jipya!! .
KUBISHA NI MAAMUZI YAKO ILA UKWELI USEMWA:
Mpenzi wako mpya ni Mpenzi wa Mwenzako wa Zamani, Usibishe! Yaani ni sawa na Nguo Chakavu ndio Dekio Jipya!! 😂😂😂
SOMA HAPA <span class="emoji emoji1f447"></span>: Kuna mtu amekosana na mpenzi wake kipindi hiki kisa nguo za sikukuu......<span class="emoji emoji1f602"></span><span class="emoji emoji1f602"></span><span class="emoji emoji1f602"></span>smh!! ...
Media Removed
SOMA HAPA : Kuna mtu amekosana na mpenzi wake kipindi hiki kisa nguo za sikukuu......smh!! Like seriously baby gal😀 . "eti oh mimi tu ndo nitavaa nguo za zamani rafiki zangu wamenunuliwa na wapenzi wao", then kama vipi na wewe nenda kwa hao wapenzi wao!! . Kuna wakaka mmeambiwa ... SOMA HAPA 👇:
Kuna mtu amekosana na mpenzi wake kipindi hiki kisa nguo za sikukuu......😂😂😂smh!! Like seriously baby gal😀
.
"eti oh mimi tu ndo nitavaa nguo za zamani rafiki zangu wamenunuliwa na wapenzi wao", then kama vipi na wewe nenda kwa hao wapenzi wao!!😡
.
Kuna wakaka mmeambiwa "usinitafute mpaka ununue hizo nguo na sitoki na wewe usiponunua! Waninunulie wengine we utoke na mimi" 😂😂😂 wadada mna maneno makali sometimes bora hata maneno ya anko magu😂 yaani kaka ukiona hivi hupendwi wanatafuta sababu tu hapo! Uko na mwanamke ila akifungua mdomo tu unapata stress ataongea nini leo😴 utasema wafanyakazi wa mashirika ya umma 😂😂
.
Sasa ukiambiwa hivyo we usijitese, siku ya sikukuu kuna mabinti wengi ambao nao watakuwa wameachwa kisa wapenzi wao wapo kwenye michepuko kama huyo wa kwako, andaa pesa ya kutosha muombe out mtoto mzuri halafu toka naye (sijasema umle, acheni zinaa vijana😏) mwambie tu yule binti ukweli like "me nina mtu ila i just feel like taking u out so No strings attached!", Mpige picha update kwenye status andika mahali mlipo😂😂 nakwambia hazipiti dakika kumi mpenzi wako atakuwa ashafika na hayupo uchi halafu kapendeza hatari! Yaani hata kama alikuwa na mchepuko hatoguswa kabisa.....🙆akimind muulize hizo nguo katoa wapi? Na hukumcheck coz hukuwa na hela ya nguo mpya so ulisubiri upate kwanza 😎, thank me later coz hatorudia tena utoto.
.
ANGALIZO: Sijasema msinunulie wapenzi wenu nguo na vitu vizuri siku hizi za sikukuu, kama una uwezo why usimnunue? Spoil ur gal lakini kama huna usijiumize fanya unapoweza😌 sasa isijekuwa una wanawake wengi so huyu ndo umemuona boya hujampa ila wengine umewapa, hapo namshauri akwambie maneno mazito kama walimu wa arts kwenye serikali ya viwanda 😂
.
Anyways hiki kipindi ni mwendo wa kukabana hata mpenzi awe wapi mfuate, akisema atakuwa home kaa naye mpaka kieleweke 😇
.
Nitoe pole kwa wale wenye wapenzi waliooa na kuolewa! Msijali hiyo ni sehemu ya kuwa mwizi wa mali za watu!! 😉 utapewa elfu kumi au hamsini kabisa japo i doubt! Lakini kumbuka ataspend na mkewe mara kumi ya hiyo, polen sana sana i feel your pain 😂😂.
Read more
 #SIKIA; Siyo udhaifu kumwona msichana mzuri halafu ukamwacha bila kumtongoza, japo uwezo na ...
Media Removed
#SIKIA; Siyo udhaifu kumwona msichana mzuri halafu ukamwacha bila kumtongoza, japo uwezo na nafasi ya kufanya hivyo ulikuwa navyo. . Actually ni ushujaa, inaonyesha unajua kutofautisha tamaa ya mwili na kupenda. . Mara nyingi huwa tunamsifia Mungu kwa kuumba anga kwa vile linaonekana ... #SIKIA;
Siyo udhaifu kumwona msichana mzuri halafu ukamwacha bila kumtongoza, japo uwezo na nafasi ya kufanya hivyo ulikuwa navyo.
.
Actually ni ushujaa, inaonyesha unajua kutofautisha tamaa ya mwili na kupenda.
.
Mara nyingi huwa tunamsifia Mungu kwa kuumba anga kwa vile linaonekana zuri, lakini haina maana lazima tumiliki hilo anga, unaweza fanya vivyo hivyo umwonapo msichana mzuri.
.
Msifu Mungu kwa uumbaji halafu nenda zako kwa amani, wala usigeuke nyuma!
.
Tuna moyo mmoja tu wa kupenda na wanawake wapo zaidi ya 3,500,000,000.
Read more
UJUMBE MAALUMU: . Unapopendwa haina maana kuwa wewe ni bora kuliko wote, haina maana kuwa wewe ...
Media Removed
UJUMBE MAALUMU: . Unapopendwa haina maana kuwa wewe ni bora kuliko wote, haina maana kuwa wewe ni mzuri zaidi au handsome kuliko wote bali tambua umebahatika tu kuwa CHAGUO BORA kwake kuliko wote aliowaona, hata wale wenye vigezo kukuzidi wewe kwahiyo usivimbe kichwa na kuanza dharau ... UJUMBE MAALUMU:
.
Unapopendwa haina maana kuwa wewe ni bora kuliko wote, haina maana kuwa wewe ni mzuri zaidi au handsome kuliko wote bali tambua umebahatika tu kuwa CHAGUO BORA kwake kuliko wote aliowaona, hata wale wenye vigezo kukuzidi wewe kwahiyo usivimbe kichwa na kuanza dharau na mashauzi mshukuru Mungu kwa bahati hiyo ya kuwa chaguo lake la pekee.

Ni matumaini yangu kwamba umejifunza kitu kupitia ujumbe huu,
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda.
Read more
. SIKIA: Mwanamke yeyote anaweza kukupa mwili wake ili uburudike nao kitandani lakini Mwanamke ...
Media Removed
. SIKIA: Mwanamke yeyote anaweza kukupa mwili wake ili uburudike nao kitandani lakini Mwanamke awezaye kukuhurumia kwenye maisha yako, akakuombea na ukapokea BARAKA ni mkeo peke yake.. #Kitu_Kikubwa_Kinakuja_Kaa_Chonjo .
SIKIA:
Mwanamke yeyote anaweza kukupa mwili wake ili uburudike nao kitandani lakini Mwanamke awezaye kukuhurumia kwenye maisha yako, akakuombea na ukapokea BARAKA ni mkeo peke yake.. #Kitu_Kikubwa_Kinakuja_Kaa_Chonjo

Loading...